Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

Wangekuwa wanawatoa ambao hawataki vita, mi naona huruma kwa watoto wasiojua lolote..!!

Hivi haiwezekani wakatafutiwa uwanja wa vita wazipige mpaka wachoke. Hii ya kupiga kokote sio nzuri..!! 😥
Hii vita ya nchi na nchi madhara hayatakua makubwa kama yale ya Israel na Hamas, Hii vita target itakua Miundombinu ya kijeshi, nishati, pro regime wa Ayatollah Khamenei, wakubwa wa jeshini na njia za kiuchumi.
 
Out of topic
Huwa najiuliza, pengine Wapalestina ndio Waisrael wa Mussa (Taifa Teule) kwani pia wapo lile eneo la Israel kwa Asili; Inakuwaje wanao jiita Waisrael na manguvu yao yote wanapigana vita na Palestina tangu miaka ya 1970, ambao hawana hata silaha ila wanaojiita waisrael wanachoka na kuomba vita iishe na chap unakuta palestina imejengeka? Ninawasisi, taifa teule ni Wapalestina.

Turudi kwenye Historia;
Baada ya vita kuu ya Pili, mwaka 1945, Marekani iliwazawadia mamluki walio isaidia kwenye Vita ambao wengi wao walikuwa ni Wajerumani; wale waliokuwa weupe (Wazungu) wakazawadiwa eneo la Palestina, tunalolitambua kama Israel kwa sasa na wale weusi (Waafrica) wakazawadiwa eneo la Africa magharibi linalo tambulika kwa sasa kama Ivory cost.
Ni mtazamo tu!
 
Ile miji ya Bethlehem na galilaya haiko Israel biblia waongo?
Hiyo miji iko kwenye Biblia lakini Israel siyo nchi ya wakristo. Ukristo ulianzishwa na mitume wa Yesu,na haukukubalika tangu mwanzo ndio maana hao mitume walipitia mateso makali ikiwemo kuuwawa mfano Stefano. Baada ya kuwa Ukristo haukubaliki nchini Israel,mitume waliamua kupeleka injili sehemu nyingine ikiwemo maeneo ya Ulaya ya leo kama vile Ugiriki na Italia. Ndio maana makao makuu ya Kanisa Katoliki yako Roma - Italia na sio Israel. Ndio maana hata nyaraka za Paulo ziliandikwa kwa wakazi wa maeneo ambayo yapo Ulaya ( Efeso,Korinto,Filipi,Thesalonike) na sio maeneo ya Waisrael. Ingawa kuna Waraka kwa Waebrania ambao haujulikani hasa uliandikwa na nani lakini Paulo alikubalika kwa watu wengine nje ya Israel tofauti na alivyokubalika na Waisrael wenzake. Hadi leo,Israel imeukataa Ukristo na sio nchi ya Kikristo. Ila Mkristo akiamua kutembelea maeneo matakatifu yaliyotajwa kwenye Biblia,serikali ya Israel haikatazi
 
Taarifa nzuri sana kwa wachimbaji na wafanya biashara ya dhahabu na mafuta...usiwahi kuuza mzigo, soon bei inapaa
 
Israel kashatangaza wanje wanjee na wandani wandani( Go to the bunker) Iran nayeye kashawaambia raia wake ,raia wote ingia ndani (all civilians get inside).Na mimi niko na maji mengiii na kindoo cha mihogo .Nikitoka X narudi JF nazungukia aljazeera ,bbc,sky na mzunguko utaendelea hivyo mpaka saa moja kwenye mualiko wa futari.
 
Hili suala limeongelewa mara nyingi na watu wengi. Inaonekana kama hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya Waisrael wa sasa na wale waliotajwa kwenye maandiko matakatifu. Pia inaonekana uanzishwaji wa taifa la sasa la Israel ni mkakati tu wa nchi za magharibi kutawala eneo la Mashariki ya kati. Hata Kanisa Katoliki lilipinga uanzishwaji wa taifa la sasa la Israel.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…