Israel: Netanyahu akabiliwa na upinzani wa jeshi kwa ukaliaji kamili Gaza

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
838
Israel lazima "iwashinde kabisa" Hamas huko Gaza, Benjamin Netanyahu amesisitiza siku ya Jumanne, Agosti 5. Mkuu wa majeshi ya Israeli, kama sehemu kubwa ya uongozi wa juu wa kijeshi, anapinga ukaliaji mpya kamili wa eneo la Palestina. Waziri Mkuu wa Israel anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa jeshi.
Israel inaelekea moja kwa moja kwa mashambulizi ya kuvizia huko Gaza, anasema mkuu wa jeshi Eyal Zamir. Hata hivyo, Benjamin Netanyahu bado anashinikiza kukaliwa kabisa kwa Ukanda wa Gaza, hasa Mji wa Gaza na kambi zilizo katikati mwa eneo la Palestina.

Siku ya Jumanne jioni, jeshi la Israel limebainisha upinzani wake kwa operesheni ya ardhini katika maeneo yenye wakazi wengi wa Ukanda wa Gaza, ambako kuna uwezekano wa kuwepo mateka wanaoshikiliwa na Hamas, na wanapendelea kuendelea kugawanya eneo hilo kwa kuunda barabara mpya na kufanya mashambulizi ya kuvizia.

Mkuu wa majeshi ameonya kwamba kuenea kwa mapigano hayo kunaweza kusababisha baadhi ya mateka kutopatikana. Vitisho vya kujiuzulu kutoka kwa Jenerali Zamir, mkuu wa majeshi, tayari vimetajwa. Mkuu wa jeshi anaonya kwamba kuenea kwa mapigano kunaweza kusababisha baadhi ya mateka kutopatikana. Wawili hao, Netanyahu na Zamir, walikabiliana siku ya Jumanne wakati wa mkutano wa usalama, ambapo ofisi ya Waziri Mkuu ilitoa taarifa fupi ikisema kwamba "jeshi la Israel liko tayari kutekeleza uamuzi wowote utakaochukuliwa na baraza la usalama."

Kwa kongamano la familia za mateka, kukaliwa kwa jumla kwa Ukanda wa Gaza ni wazi kuwa ni hukumu ya kifo kwa mateka 22 ambao bado wanafikiriwa kuwa hai. Hatua inayofuata itafanyika kesho, Alhamisi, saa 12 jioni saa za ndani. Baraza la usalama la Israel, ambalo linajumuisha mawaziri wenye msimamo mkali, litalazimika kufanya uamuzi huo. Baraza hilo la usalama peke yake, kimsingi, ndilo linaloweza kufanya uamuzi wa kuongeza mashambulizi
 
Israel atamegua kipande Kwa kipande, Kila kipande cha ardhi atakachoona kinafaa atakichukua Kwa gharama yoyote Ile, anafanya "Ethnic Cleansing" kile kile alichofanya Hitler ndo Israel anafanya Kwa version mpya kabisa, sijajua kama ninavyoona Mimi ni sawa na wanavyoona wale Masheikh wa kiarabu.
 
Israel lazima "iwashinde kabisa" Hamas huko Gaza, Benjamin Netanyahu amesisitiza siku ya Jumanne, Agosti 5. Mkuu wa majeshi ya Israeli, kama sehemu kubwa ya uongozi wa juu wa kijeshi, anapinga ukaliaji mpya kamili wa eneo la Palestina. Waziri Mkuu wa Israel anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa jeshi.
Israel inaelekea moja kwa moja kwa mashambulizi ya kuvizia huko Gaza, anasema mkuu wa jeshi Eyal Zamir. Hata hivyo, Benjamin Netanyahu bado anashinikiza kukaliwa kabisa kwa Ukanda wa Gaza, hasa Mji wa Gaza na kambi zilizo katikati mwa eneo la Palestina.

Siku ya Jumanne jioni, jeshi la Israel limebainisha upinzani wake kwa operesheni ya ardhini katika maeneo yenye wakazi wengi wa Ukanda wa Gaza, ambako kuna uwezekano wa kuwepo mateka wanaoshikiliwa na Hamas, na wanapendelea kuendelea kugawanya eneo hilo kwa kuunda barabara mpya na kufanya mashambulizi ya kuvizia.

Mkuu wa majeshi ameonya kwamba kuenea kwa mapigano hayo kunaweza kusababisha baadhi ya mateka kutopatikana. Vitisho vya kujiuzulu kutoka kwa Jenerali Zamir, mkuu wa majeshi, tayari vimetajwa. Mkuu wa jeshi anaonya kwamba kuenea kwa mapigano kunaweza kusababisha baadhi ya mateka kutopatikana. Wawili hao, Netanyahu na Zamir, walikabiliana siku ya Jumanne wakati wa mkutano wa usalama, ambapo ofisi ya Waziri Mkuu ilitoa taarifa fupi ikisema kwamba "jeshi la Israel liko tayari kutekeleza uamuzi wowote utakaochukuliwa na baraza la usalama."

Kwa kongamano la familia za mateka, kukaliwa kwa jumla kwa Ukanda wa Gaza ni wazi kuwa ni hukumu ya kifo kwa mateka 22 ambao bado wanafikiriwa kuwa hai. Hatua inayofuata itafanyika kesho, Alhamisi, saa 12 jioni saa za ndani. Baraza la usalama la Israel, ambalo linajumuisha mawaziri wenye msimamo mkali, litalazimika kufanya uamuzi huo. Baraza hilo la usalama peke yake, kimsingi, ndilo linaloweza kufanya uamuzi wa kuongeza mashambulizi
Mtanzania mwenzio huyo aliuawa na Waislamu wa Gaza

View: https://x.com/israelnewspulse/status/1953191878347899335
 
Back
Top Bottom