Israel ni nchi ya Wayahudi - Netanyahu

Israel ni nchi ya Wayahudi - Netanyahu

Hao waarabu wanafaida gani kuendelea kuwepo huko?

Waondoke kama hawataki wapelekewe moto usiku na mchana.
baadae utasikia account ilikuwa hacked [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Naomba nieleweshwe kdgo, wanasema waisrael ni taifa takatifu la Mungu na wao ni wana wa Mungu(according to the bible), swali-inamana mauaji wanayoyafanya yote yana baraka zote za Mungu? Naomba nijibiwe.
 
Ukienda kwenye dini mvamizi ni Myahudi alitoka Misri akaenda hapo alipo na aliwakuta watu ,kabla ya kwenda Misri Kwa njaa Wayahudi walikuwa wanaishi wapi? Walikotoka kabla ndio kwao ila sio hapa Kwa Wapalestina huu ni uongo.
Hata kabla ya kwenda uhamiji misri walitokea hapo hapo kaanani au israel ya leo.
 
Netanyahu aache January janja. Babu zao walipotoka masri utumwani.wakakoswa koswa na firauni pale kwenye bahari. Walipokosea njia.wakaenda njia ya baharini mungu akawasaidia kwa kuachanisha bahari wakamkwepa firauni.na firauni akafa na majeshi yake.baada ya hapo walimsumbua sana musa mpaka musa anakufa.anachukua uongozi yoshua.anazunguka zunguka nao kwa miaka 40.wanavamia nchi za watu.nchi waliyoahidiwa sio hapo israel.hawajawahi kufika kwenye hyo nchi sababu ya uj
WW ni mjinga samahani sana kwa hilo
 
sehemu Israel ilipoenda kuanzisha nchi hapakua na makazi ya waarabu....waarabu walikua sehem za miinuko na waisrael walikua tambarare na walipoanzisha mashamba waarabu ndo walikuja kuomba kazi kwenye hayo mashamba na baadae wakaanza kusema ni ardhi yao....
Sio kweli maana walipigana kuondoa wenyeji soma vizuri historia
 
Hizo story mnazitolea wapi,kwani Tanganyika lilikuwa eneo la nani,Mwingereza au Mtanganyika?

Eneo lote hilo lilikuwa la Palestina kabla ya
Balfour Declaration ( nenda kasome) 1917,ambao waliigawa ardhi ya Palestina.

Na still bado pamoja na kupewa ardhi ya Palestina, kila siku wanaimega ardhi kwa miaka zaidi ya 75 Wapalestina wanaendelea kuteseka,mlitaka wafanye nini?

Baada ya kugawanywa na kupewa mipaka wapalestina wakashawishiwa na waarabu wenzao wakatae mipaka ya UN,roho mbaya imewakost.
 
"Wayahudi wameishi katika ardhi ya Israel, ambayo sasa ni nchi ya Israel, kwa takriban miaka 3,500. Tumetawaliwa na Warumi, tumetawaliwa na Wa-Byzantini, wametufanyia mambo mabaya, lakini hawakutufukuza, tofauti na vile watu wanavyofikiria. Upotevu wa ardhi yetu ulitokea wakati wa uvamizi wa Kiarabu katika karne ya saba.

Wa-Arabu waliingia kutoka Arabia na kufanya kitu ambacho hakijawahi kutokea kabla, si Warumi, Wa-Byzantini, si Wagiriki kabla yao, wala Alexanda the great, hakuna aliyewahi kufanya hivyo. Walianza kuchukua ardhi ya mkulima Myahudi. Walileta makoloni ya kijeshi ambayo yalichukua ardhi. Kadri muda ulivyopita, Wayahudi wakawa wachache katika ardhi yetu. Kwa hivyo, ni chini ya uvamizi wa Kiarabu ambapo Wayahudi walipoteza ardhi yao.

Wa-Arabu walikuwa wakoloni, Wayahudi walikuwa wenyeji. Hii ndivyo ilivyokuwa kwenye historia. Wayahudi walipokonywa ardhi yao. Tuliachwa tukitawanyika katika pembe za dunia, tukiteseka kwa sababu hatukuwa na nchi yetu, lakini hatukutoweka na kamwe hatukukata tamaa ya kurudi katika ardhi yetu ya kiasili.

Wa-Arabu, ambao walitawala ardhi, hawakuwahi kuifanya kuwa yao. Ilikuwa ardhi isiyo na watu. Katika karne ya 19, wazo la kurudi Yerusalemu likawa ukweli, na kwa sehemu kubwa, ilikuwa kutokana na msaada wa Wakristo Wakizayuni.

Kwa wazo la kurudi, Wayahudi waliendelea kurudi katika ardhi ya Israel katika karne ya 19. Matokeo ya kurudi huku ni kwamba tukaanza kujenga mashamba, viwanda, na maeneo ya ajira. Wa-Arabu, ambao walikuwa wamehamia katika karne zilizotangulia, sasa wanajiita Wapalestina. Waliibua upya historia na kusema wamekuwepo kwa karne nyingi.

Hawana haki ya kuwa hapa. Ardhi hii ni yetu. Imekuwa yetu kwa miaka 3,500. Ikiwa unachukua nyumba ya mtu, kuwafurusha na kuwapokonya, na hawakukataa madai yao, na wanasema ni madai yetu, na wewe unaiacha kama eneo lisilo na watu.

Na familia na uzao wa watu waliotimuliwa wanarudi, wanajenga nyumba, huna haki ya kuwakataza kuwa hapa. Tunawaambia, mnaweza kuishi hapa, sisi pia tunaweza kuishi hapa, lakini ardhi hii ni yetu, ni nchi yetu.

Na sababu hii ya mzozo inaendelea ni kwa sababu Wapalestina, wanaowakilisha wakoloni wa Kiarabu, uvamizi wa Kiarabu, katika Mashariki ya Kati na maeneo mengine, wanadai kuwa hatuna haki ya kuwa na nchi ya Kiyahudi. Lakini tunayo haki. Kama kuna watu wenye haki ya kuwa na nchi, kama kuna watu ambao hawajawahi kukataa ndoto yao ya kurudi katika nchi yao ya kiasili, basi Wayahudi wanamiliki ardhi hii. Ardhi hii ni ya Wayahudi.

Wapalestina wana uhuru wa kuishi hapa karibu nasi, miongoni mwetu, lakini hawana haki ya kudai kuvunjwa kwa nchi ya Kiyahudi. Hiyo si haki. Hiyo ni dhuluma." Alisema Benjamin Netanyahu alipohojiwa na chombo kimoja cha Habari.

Check video 👇🏾👇🏾
That says Benjamin
 
Anayebisha Israel ni nchi ya wayahudi atabisha kila kitu
 

Attachments

  • 20231112_103053.jpg
    20231112_103053.jpg
    151.2 KB · Views: 3
Back
Top Bottom