Israel ni nchi ya Wayahudi, soma Hesabu 34:1-15

Israel ni nchi ya Wayahudi, soma Hesabu 34:1-15

Ndiyo, kabla ya Abraham, Kanaani ilikuwa na wafalme wengi (Salem, Sodom, Gomorra n.k.). Leo kama Wacanaan wangetokea na kudai ardhi hiyo kwa haki ya kihistoria, wengi hawangekubali kuwapa kwa sababu ya mabadiliko ya wakati na historia ndefu.Kibiblia, ahadi maalum ilipewa Isaka kisha Yakobo (sio kwa Ismael, Esau wala wengine), kwa sababu Mungu alichagua line moja ya agano (si warithi wote wa Abraham). Hivyo ni chaguo la Mungu, si wingi wa watoto
Kwahiyo wasabato marejeo nao wakija na maandiko yao kuidai Tanzania pia tuwaachie?

Kama issue ni biblia basi achaneni na kusema ooh hakukuwa na taifa la palestina wala sijui Israel alikuwepo pale kihistoria nyie komaeni na BIBLIA yaani semeni tunachinja wapalestina sababu biblia ilituruhusu sio kuokoteza justification za uongo..
 
Ndiyo, kabla ya Abraham, Kanaani ilikuwa na wafalme wengi (Salem, Sodom, Gomorra n.k.). Leo kama Wacanaan wangetokea na kudai ardhi hiyo kwa haki ya kihistoria, wengi hawangekubali kuwapa kwa sababu ya mabadiliko ya wakati na historia ndefu.Kibiblia, ahadi maalum ilipewa Isaka kisha Yakobo (sio kwa Ismael, Esau wala wengine), kwa sababu Mungu alichagua line moja ya agano (si warithi wote wa Abraham). Hivyo ni chaguo la Mungu, si wingi wa watoto
Kwahiyo Mungu alipomuahidi Abraham kuwa atampa uzao mkubwa na baraka kwa uzao wake alikua anamdanganya? Kwahiyo alikua anambariki mjukuu mmoja tu na sio MATAIFA na UZAO wake kama biblia inavyosema!!

Si aliitwa baba wa mataifa kumbe tulidanganywa?
 
Wayahudi wengi wanaamini kwamba agano hili (covenant) kati ya Mungu na Waisraeli (kupitia Abrahamu, Musa n.k.) bado linaendelea na halijabadilishwa au kuondolewa.
Mungu yupi huyo? Yesu ni Mungu hicho wayahudi wanapinga sasa Mungu gani huyo ambaye hahusiki na Yesu wala imani ya kikristo? Ukisoma hizo vitu umeandika hapo juu vina contradict sana na Bible unayodai wanaiamini so vyote viwili haviwezi kuwa sahihi kwa wakati mmoja it's either bible ndio ya kweli au hizo Jewish Talmuds n.k ziko sahihi!!

Ni baadhi ya vitabu tu kama vile vya Musa plus joshua hivi ndio vinakubaliana the rest wamechomekea commentary zao na interpretation zao ambazo zinapinga sio tu ujio wa Yesu bali hata Uungu wa yesu ambayo ndio Central theme ya biblia.
 
unazungumzia ahadi ya awali kwa Abrahamu na maono ya Mungu ya mwisho, tumia Mwanzo 15 (eneo kubwa la Middle East).
Kwanini Israel haijawahi kuidai Saudi Arabia kama issue ni kufuata ahadi ya Abraham? Ndio hapa utapeli unapoanzia. Kumbuka biblia hiyo hiyo inaruhusu ukoloni je ina wakristo tulikosea kupinga kuuzwa utumwani?
 
nitajie wafalme wa yudea unaowajua, je yudea na israel hizo falme hazikuwahi kupigana? Ainisha maeneo ya utawala wao. Je samaria ilikuwa upande wa ufalme upi?
Yuda na Israeli walishapigana, Yuda ilikuwa maeneo ya kusini katika milki ya kabila za Yuda na Benjamini, Israeli ilikuwa kaskazini maeneo ya makabila tisa, kabila moja la Walawi hawakuwa na urithi wa eneo, wengiwao walienda kusini.

Samaria ulikuwa mji mkuu wa utawala wa kaskazini

Yerusalem ukawa mji mkuu wa utawala wa kusini
 
Back
Top Bottom