zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 24,661
- 40,890
Kwahiyo wasabato marejeo nao wakija na maandiko yao kuidai Tanzania pia tuwaachie?Ndiyo, kabla ya Abraham, Kanaani ilikuwa na wafalme wengi (Salem, Sodom, Gomorra n.k.). Leo kama Wacanaan wangetokea na kudai ardhi hiyo kwa haki ya kihistoria, wengi hawangekubali kuwapa kwa sababu ya mabadiliko ya wakati na historia ndefu.Kibiblia, ahadi maalum ilipewa Isaka kisha Yakobo (sio kwa Ismael, Esau wala wengine), kwa sababu Mungu alichagua line moja ya agano (si warithi wote wa Abraham). Hivyo ni chaguo la Mungu, si wingi wa watoto
Kwahiyo Mungu alipomuahidi Abraham kuwa atampa uzao mkubwa na baraka kwa uzao wake alikua anamdanganya? Kwahiyo alikua anambariki mjukuu mmoja tu na sio MATAIFA na UZAO wake kama biblia inavyosema!!Ndiyo, kabla ya Abraham, Kanaani ilikuwa na wafalme wengi (Salem, Sodom, Gomorra n.k.). Leo kama Wacanaan wangetokea na kudai ardhi hiyo kwa haki ya kihistoria, wengi hawangekubali kuwapa kwa sababu ya mabadiliko ya wakati na historia ndefu.Kibiblia, ahadi maalum ilipewa Isaka kisha Yakobo (sio kwa Ismael, Esau wala wengine), kwa sababu Mungu alichagua line moja ya agano (si warithi wote wa Abraham). Hivyo ni chaguo la Mungu, si wingi wa watoto
Mungu yupi huyo? Yesu ni Mungu hicho wayahudi wanapinga sasa Mungu gani huyo ambaye hahusiki na Yesu wala imani ya kikristo? Ukisoma hizo vitu umeandika hapo juu vina contradict sana na Bible unayodai wanaiamini so vyote viwili haviwezi kuwa sahihi kwa wakati mmoja it's either bible ndio ya kweli au hizo Jewish Talmuds n.k ziko sahihi!!Wayahudi wengi wanaamini kwamba agano hili (covenant) kati ya Mungu na Waisraeli (kupitia Abrahamu, Musa n.k.) bado linaendelea na halijabadilishwa au kuondolewa.
Kwanini Israel haijawahi kuidai Saudi Arabia kama issue ni kufuata ahadi ya Abraham? Ndio hapa utapeli unapoanzia. Kumbuka biblia hiyo hiyo inaruhusu ukoloni je ina wakristo tulikosea kupinga kuuzwa utumwani?unazungumzia ahadi ya awali kwa Abrahamu na maono ya Mungu ya mwisho, tumia Mwanzo 15 (eneo kubwa la Middle East).
Yuda na Israeli walishapigana, Yuda ilikuwa maeneo ya kusini katika milki ya kabila za Yuda na Benjamini, Israeli ilikuwa kaskazini maeneo ya makabila tisa, kabila moja la Walawi hawakuwa na urithi wa eneo, wengiwao walienda kusini.nitajie wafalme wa yudea unaowajua, je yudea na israel hizo falme hazikuwahi kupigana? Ainisha maeneo ya utawala wao. Je samaria ilikuwa upande wa ufalme upi?