Montserrat
JF-Expert Member
- Sep 9, 2011
- 10,938
- 14,745
Mkuu sidhani kama China na Iran kupeleka hizo silaha basi kutajumuisha mvutano mkubwa baina ya nchi hizo mbili.
CHINA
Miezi michache ya nyuma, China ilipiga mkwara mzito wa kuivamia kijeshi Taiwan endapo aliyekuwa Spika wa Bungu sijui ni makamu wa Rais, anaitwa Peros akiingia ndani ya Taiwan basi China haitasita kuchukua maamuzi magumu.
Mwisho tukaona US ikapeleka kiongozi wake hapo Taiwan na mpaka sasa China hakuna ilichokifanya.
Sio rahisi China kufanya muujiza wowote ktk huu mzozo na hata hizo meli sidhani kama zitakuwa na impact kubwa sababu China kuitetea tu Taiwan ameshindwa, ndo akawe mkombozi Palestina?
IRAN
Hakuna unyama ambao Israel hajaufanya mpaka sasa ndani ya Palestine, kama angekuwa na la kufanya basi angeshafanya muda mrefu.
Wazir wa mambo ya nje sijui wa ulinzi yule, alipotaka atue Syria dakika tu Israel akalipua ule uwanja na Iran akaufyata, akakaa kimya.
- Binafsi sioni nchi ya Kiislamu ambayo ina ubavu wa kuingia 100% ktk huu mgogoro kama tunavyoona mataifa ya magharibi yanavyoingia Israel.
Inawezekana Marekani amewachoka waislamu; anataka kupunguza kizazi chao