Christopher Cyrilo
Member
- Oct 5, 2015
- 90
- 482
ISRAEL vs IRAN -01
Nimetamanani kuleta makala hii kutoka kwenye kitabu changu cha ISTILAHI ZA UHALIFU NA USALAMA, ili watu wajifunze na kujadili wakiwa na taarifa ambazo naamini awaki hawakuwa nazo.
Dr. Chris Cyrilo
Sehemu ya I
Ndani ya jengo la makao makuu ya shirika la kijasusi la Mossad, ghorofa ya tatu ni rahisi kuona kibao kilichoandikwa Ramsad, neno ambalo ni kifupi cha maneno ya kiebrania - Rosh ha Mossad, yaani 'Mkuu wa Mossad'. Chini ya kibao hicho kuna mlango wa kuingia ndani ya ofisi ya mkuu wa Mossad, ofisi ambayo kuta zake zilipambwa na picha kadhaa zenye ujumbe maalumu kwa Meir Dagan aliyeongoza shirika la Mossad kuanzia mwaka 2002 hadi 2010. Picha moja kati ya chache zilizopo ndani ya chumba hiko, iliibua kumbukumbu na hisia za kutisha kila ilipotazamwa. Picha hiyo ilimuonesha mzee wa kiyahudi akiwa amepiga magoti, mkononi ameshika kitambaa maalum cha kufanyia ibada za kiyahudi kiitwacho Talllit, huku amezungukwa na askari wa chama cha Nazi cha Ujerumani.
Mzee huyo wa kiyahudi alikuwa babu mzaa mama wa Meir Dagan, aliyeitwa Ber Ehrlich Sloshny na picha hiyo ilipigwa katika mjini mdogo wa Lokov, nchini Ukraine muda mchache kabla ya mzee huyo na maelfu ya wayahudi wengine kuuawa mikononi mwa askari wa Nazi. Ni kwa namna gani aliipata picha hii! Dagan anahadithia namna baba yake alivyosafiri hadi mjini Lokov ili kuwatafuta ndugu wa kiyahudi waliosalia, lakini hakukuwa na myahudi aliyebaki hai katika mji huo. Isipokuwa, mtu mmoja asiye myahudi alibaki kwa kazi ya kuzika miili ya wayahudi, amri aliyopewa na askari wa Nazi. Mtu huyo, alikuwa na picha za wayahudi wengi ambazo pia alizichukua kwa amri ya askari wa Nazi, mojawapo ikiwa ni picha ya mzee Sloshny. Baba yake Dagan alichukua picha hizo na kurudi nazo Israel.
Dagan aliibeba picha hii kila alipohama ofisi, na sasa akiwa Mkuu wa Mossad ameitundika ukutani na kuitazama kila siku. Ilikuwa ni kumbukumbu ya namna jamii ya kiyahudi lilivyoponea chupuchupu kutoweka juu ya uso wa dunia kutokana na mateso na mauaji dhidi ya wayahudi yaliyopamba moto huko Ulaya wakati wa vita kuu ya pili ya dunia. Picha hiyo pia ilitoa funzo mujarabu, ya kwamba binadamu anaweza kugeuka kirahisi na kuwa mnyama katili dhidi ya binadamu wengine, na hilo laweza kutokea kwa kila mtu.
Meir Dagan, akiwa Mkuu wa Mossad aliamini kuwa jukumu la kuhakikisha usalama, ustawi na uwepo jamii ya kiyahudi duniani upo mikononi mwake.
Moja kati ya majukumu makubwa aliyokuwa nayo, ni kudhibiti maadui wa Israel, hasa Majirani zake kumiliki silaha za maangamizi, kwa namna yoyote inayowezekana. Mwaka 2004, miaka miwili baada ya kubeba cheo cha ukuu wa Mossad, Meir Dagan aliamua kwamba jukumu namba moja ni kupambana na Iran ambayo ilidhamiria kwa dhati kumiliki silaha za kinyuklia, chini ya uongozi wa kishia wa Ayatollah Ruhollah Khomeini.
Dhamira ya kumiliki silaha za kinyuklia nchini Iran ilikuwapo tangu miaka ya 1950 wakati wa utawala wa Shah Mohammad Reza Pahlavi, aliyewekwa madarakani kwa nguvu za CIA na kufanywa kuwa kiranja wa eneo la mashariki ya kati. Wakati huo Iran iliweza kununua vinu vya kuzalishia nguvu za kinyuklia kutoka Marekani, kwa ajili ya kuzalisha umeme, kufanyia tafiti za kitabibu lakini pia, utawala wa Iran haukuficha dhamira yake ya kutumia teknolojia hiyo kwa manufaa ya kijeshi, jambo ambalo lingeongeza ushawishi zaidi kwa Majirani, maadui na marafiki wa mbali.
Wakati Iran ikinufaika kwa Teknolojia hiyo ya Marekani, Israel nayo ilitamani kupata chochote kutoka Iran, na hivyo kuunga urafiki wa karibu. Ingawa Israel ilikuwa ikipambana mara kwa mara na mataifa ya kiarabu, Iran iliyokuwa chini ya uongozaji wa ukoo wa Shah ilibaki kuwa rafiki wa Israel na kuhatarisha mahusiano yake na nchi za kiarabu, Saudia na Misri. Katika mashirikiano hayo, Intelijensia ya Israel iliweza kutoa mafunzo kwa kikosi cha siri ndani ya jeshi la polisi la Iran kilichoitwa Savack, na kwa upande wa Israel ilinufaika kwa kupata upendeleo wa kutumia ardhi ya Iran kwa shuguli zake za kiintelijensia dhidi ya mataifa mengine ya karibu, hususani Iraq. Ndani ya Iran, Intelijensia ya Israel iliweza kupanga mipango yake, kutekeleza misheni zake na kuwasajili mawakala wapya wa ushushushu wa kwenda kuiba taarifa katika nchi za kiarabu. Serikali ya Iran iliyoa hata nyaraka zake rasmi kwa ajili ya kusaidia shughuli za Irael. Kwa upande wa biashara Iran iliiuzia mafuta Israel na Israel iliiuzia Iran silaha, zaidi wakati Iran ikipigana vita dhidi ya Iraq.
Mradi wa pamoja wa nyuklia uliopewa jina la siri la 'Flower' ulilenga kuzipatia Iran Israel silaha za Nyuklia, huku Israel ikitoa msaada wa kiteknolojia na kuishawishi Iran itumie urafiki wake na Marekani kwa ajili ya kupata nyenzo zaidi ili zisaidie mradi huo. Lakini utawala wa Shah wa Iran ulikataa mpango huo, na endapo mradi huo ungekubalika basi leo hii Israel na Iran wangekuwa marafiki wakubwa au maadui wakubwa zaidi kuliko ilivyo sasa. Utawala wa Iran ulitamani kuwa na silaha za kinyuklia lakini haukuhitaji msaada kutoka Israel, kwakuwa Iran ilikuwa na marafiki wenye nguvu na teknolojia kubwa zaidi; Marekani, Ufaransa na Uingereza. Kwa hiyo, kwa Iran ilikuwa ni suala la muda tu kuweza kupata silaha za nyuklia. Israel, baada ya kukataliwa mpango huo iliamua kufanya operesheni yake binafsi kuelekea umiliki wa silaha za kinyuklia.
Inaendelea...