Dah! Anatia huruma sana.
Imetosha sasa. Nadhani kama ni somo watakuwa washalipata.
Wao [Hamas] ni non-state actors. Ni wanamgambo tu. Hawana tofauti na sungusungu.
Hawawezi kupambana na jeshi la Israel linalobebwa na Marekani, Uingereza, Ufaransa, na nchi zingine za magharibi.
Waislamu wenzao wa Misri, Saudia, na kwingineko, hawawaungi mkono vile ambavyo Israel inaungwa mkono na nchi za magharibi.
Taswira za vitoto vidogo vilivyolipuliwa na mabomu huko Gaza zinasononesha sana.
Mji wa Gaza umebaki kuwa magofu tu.
Waisraeli takribani 1,300 na ushee waliuliwa hiyo Oktoba 7, 2023.
Mpaka kufikia sasa, zaidi ya Wapalestina 40,000 wamekufa toka hii vita ianze.
Ni mpaka Wapalestina wangapi wafe ili Isael iridhike?
Wengi wa hao marehemu, si ajabu hata hawana uhusiano wowote ule na Hamas.
Enough is enough. This carnage has to end immediately.