Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Baada ya kusita kidogo kwa ule moto wa mabomu mazito kwa wiki moja. Tangu jana usiku mabomu mazito ya kuporomosha majengo yamejirudia. Na si kaskazini peke yake bali mpaka kusini watu walikotakiwa waende kwa usalama wao.
Inajulikana hapo juzi Jeshi la Israel liliingia ndani ya Hospitali kuu ya Alshifa. Pamoja na kutangaza hapo awali kuwa Alshifa ndipo ilijpo command nodule ya Hamas. Maneno hayo yalirudiwa na Rais wa taifa kubwa duniani la Marekani, Joe Biden.
Madaktari ambao wengine wala si waislamu au wapalestina walisisitiza hakuna vitu hivyo. Hatimae Jeshi la IDF lililiingia ndani na hakuna kitu cha maana walichokiona. Kwa aibu wamehojiana na wagonjwa kuhusu habari za Hamas bila kujali majeraha waliyowasababishia.
Kurudia kwa mashambulio hayo na vipeperushi vya kuhofisha watu kuna maana nyingi. Kwanza ni kupata aibu kubwa ya kushindwa kuwapata Hamas na mateka kutoka mahospitali manne makubwa walizozivamia na kuzikalia.
Kwa upande mwengine kunaweza kuwa na maana ya kutaka kumaliza haraka uvamizi wake wa Gaza na kutangaza ushindi kabla mambo hayajazidi kuharibika kwa upande wao.
Washirika na waungaji mkono wa Israel kwa sasa wameonekana kuanza kuligeuka taifa hilo jeuri lisiliosikiliza ushauri wa hata marafiki zake wala kutekeleza azimio lolote la umoja wa mataifa.