Israel yafanya mambo ya aibu na uwendawazimu.Yatengwa na mataifa karibu yote duniani

Acha kusoma sana propaganda, au ukiwa unasoma soma pia na upande wa pili wa hoja ndo utoe maamuzi...Israel itamaliza vita muda imejiridhisha, na nchi zote zitatengeneza mahusiano nao...hiyo ndio given
 
Walishasema hata wakitengwa na ulimwengu wote watajilinda wenyewe na wajibu wao siyo wa Taifa lolote lile. Hao wapo duniani kote ,
 
Unaongea nonsense watu walivamiwa ...wakauawa mamia ya watu wamebackfire nyie mnalalamika Kama HAMAS walijua Israel ni makatili kwa Nini waliwachokoza? Acha wapambane kiume
 
Ina maana hao waarabu hawajapita dar es salaam hawajapita tanga hawajapita visiwani zanzibar na mafia na kama walipita vp nako ni jangwa au?
 
Kwani wanaouwawa nibmagaidi au wanawake na watoto?
Au hao wanawake na watoto ndio magaidi?
 
Israel alishanusa harufu ya unafiki wa nchi za kiarabu, anatumia kanuni ya fittest for survival, ameshambuliwa October 7 nchi za kiarabu wakafanya maandamano ya kuunga mkono uuaji wa wayahudi, wameteka na kuondoka na mateka, halafu wanataka Israel atulie na kusalimu amri mbele ya HAMAS. Hawana hata aibu, mbona hawasemi Hamas waachie mateka ili vita iishe? Ila wanataka Israel asitishe vita! Je akisitisha vita na huku Hamas wanasema wayahudi watoke middle East nini hatima ya Israel?
 
IDF walishashindwa vita siku nyingi sana, sasa Vita gani tena isimamishwe?
 
Tumefikia huku? Hali yetu ni mbaya. Sasa tunatafuta huruma 🤣
 
Tumefikia huku? Hali yetu ni mbaya. Sasa tunatafuta huruma 🤣
Hahaha inashangaza sana maana hawa ma reporter wa Hamas humu ndani kuanzia Alwaz bibi Faiza na mwanae malaria Kila siku wanawapamba Hamas walivyo very competence kwenye battlefield Cha ajabu wanalilia ceasefire inashangaza sana

Out of topics Chizi unajua Kuna mwamba kakufungulia thread 🧵 uko?😂
 
Israeli hatishiki kwa lolote lile hata akitengwa na ulimwengu mzima,

Huu ni unafiki wa mataifa tu na wala hakuna chochote, ni taifa moja la Marekani hapo jana balozi wake wa UN ndiye aliyelaani na kuyataka mataifa pia kulaani kitendo cha 7 October kilichofanywa na Hamas

Je mlitaka Israel ifanye nini after 7th October?

Ni akili za kuku tu ndo zinaweza mpinga Israel na kusapoti ugaidi wa Hamas
 
Alikuwa ametulia zake mkabugia matende yenu mkavimbewa mkaona mkamchokoze, pambaneni na Hali yenu. Linapokuja suala la raia wake huwa Hana simile hufuta kizazi chote kilichomwaga damu ya kiyahudi kumbuka Mungu huwaunga mkono kwenye harakati zao tangu kale hivyo mpaka muombe poo, hata mkiungana
 
Mimi na hawa wenzangu tulikubaliana kuwapiga vita humu JF hao Israel mpaka wafe. Naona kama wenzangu wamebadili gear hewani? Sielewi tena jamaa anaanzaje kuonesha kama huruma huruma. Tulisema Israel ameingia kwenye mtego atauliwa hadi bata. Sasa jamaa kama wananiachia peke yangu?

Yule dogo bwege sana. Nimeshamchana kuwa asituone hivi sisi tupo tuna sogoza humu tumeoa. Na wake wetu wana wivu sana.
 
Ule hauwezi kuitwa ugaidi.
Ugaidi halisi ni huu unaofanywa na Israel na wafadhili wake.

Wamefanya ugaidi na wenyewe wanajibiwa kijeshi. Hata sisi huku Tz Jw ilifyagia Kibiti na mkuranga kipindi kile cha matishio ya ugaidi.

Sasa kwanini Israeli aonekane mbaya anapolinda raia wake?!
 
Mnataka aache kupigana ili watumwa wa Allah kina Abdul wavamie tena Kibutz>
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…