Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Israel ilifanya shambulio lake la mwanzo kwa Yemen na kuiharibu vibaya bandari ya Hodeida nchini humo kwenye eneo linalodhitiwa na Houth.
Waziri wa ulinzi wa Israel,Yoav Gallant amesema shambulio hilo si kwa Houth pekee bali ni onyo kwa wote wenye uadui na Israel.Akaongeza kusema kuwa moto unaowaka Hodeada unashuhudiwa na watu wote wa mashariki ya kati.
Kinachoshangaza ni jinsi mataifa hayo ya mashariki ya kati wanavyochukulia kuwa shambulio hilo ni kwa Houth pekee wakati mayahudi wanakusudia kuwatisha wote.
Israel imeanza Gaza na ukingo wa magharibi,imeingia Yemen na itafanya kwengine kwa ubabe bila hao watawala wa mashariki ya kati kuzinduka.
Hata hivyo kauli hiyo inaweza kuleta mabadiliko kwenye akili za watawala hao na kutamkwa kwake ni kipimo cha kibri cha Israel ikikaribia kuangamia kama ilivyotokea kwa firauni wakati alipozidi uadui na Mungu muda mfupi kabla ya kushikwa na kuangamizwa.
Baadhi ya wachambuzi wenye kufuatilia mizozo ya mashariki ya kati wamesema maamuzi ya Israel kuishambulia Yemen yanaweza kuwa sababu ya kuyapa nguvu makundi yanayopingana nayo na si kinyume chake.