Issue kubwa ni watu kutaka kutimiza ndoto zao za urais 2025 baada ya Mwendazake kuondoka

Issue kubwa ni watu kutaka kutimiza ndoto zao za urais 2025 baada ya Mwendazake kuondoka

Huyu Mama kufika 2025 kila mtu atakuwa amemgeuka,Kwa ujumla kama Chadema wakijipanga,plus huruma za wananchi na kupitia Viongozi wa Dini na Asas Zisizokuwa za kiserikali wanachukua inchi kiulaini.Maana mpaluano ulioko huko CCM sio wa kitoto,hata mda wa kuiba kura watakosa
Subiri uone Ccm watakavyoungana ktk uchaguzi huwa wanasambalatika kabla na baada ya uchaguzi wale
 
Mbeleko ipo pale kwa ile katiba chakavu c lingne
Bado sana. TANU ilifanikiwa sana kupandikiza mbegu flan ya woga wa mabadiliko vichwani mwa Watanzania. CCM ikarithi na matokeo yake yake sasa inahama kutoka kizazi hadi kizazi. Hili ndilo eneo ambalo Mwalimu pengine alifanikiwa kuliko maeneo yote. CCM ilitikiswa na Mrema sote tukaamini kwamba Kachero Lyatonga anatinga Ikulu. Wakati huo Mrema alitokea kuwa kati ya watu 5 maarufu nchini asingekosekana.Ikaja enzi ya CUF ngangari.Unakumbuka amshaamsha ya wafuasi wa Lipumba kipindi kile wakisafiri huku na kule kwa kutumia malori.Unakumbuka mafuriko ya Lowasa?Jiulize kwa nini kote huko upinzani ulidondokea pua. Nitajie chama kimoja tofauti na CCM barani Africa kilichoasisi Uhuru na bado kiko na uhakika wa kubaki mamlakani kwa asilimia 100?Nitajie kimoja tu.Mwalimu alipiga msumari mbaya sana.
 
Yatasemwa mengi na mtasikia mengi, ila issue kubwa ni watu kuutaka urais wa nchi hii mwaka 2025.

Wakati Magu yuko hai, walikosa ujasiri wa kuonyesha hadharani mtatamani yao na kwa Mama, bado hawajaanza, ila ili wapate hiyo fursa(waanze) ni lazima Mama asigombee (bahati mbaya alishasema atagombea), hivyo wamebaki na option moja tu ya kumpinga au kutafuta sababu aonekane hatoshi.

No wonder hata waandamizi ndani ya chama na serikali wako kimya ingawa walipaswa wamtetea Boss wao kulingana na utamaduni wao.

Kwa maneno mengine,waandamizi nao wanautaka urais wa 2025 na ndio maana wametulia kama maji kwenye mtungi.

Kwa sasa, wanaweza kuungana kwa hoja ya uzanzibari na utanganyika, na wakishatimiza azima yao, hawa watanganyika wataingia tena katika vita ya makundi huku kila kundi likiwa na mgombea/Mtia nia wao na hapo ndio ile dhambi ya ubaguzi aliyoiongelea Baba wa Taifa itapoanza kuwatafuna.

2025 patakuwa hapatoshi na si ajabu yale ya JK na EL yakajirudia na safari wanaweza wasivuke salama.
Ndo tunaingia 2022, Mungu atunusuru. Tuna a full 2023 na 2024, na miezi 10 almost ya 2025. In between yatakokea mengi, misimamo itabadilika, watajitokeza ambao hatutegemei. Tusubiri
 
Kwa kusubiri loose ball watakuwa pending mpaka sisi sote tutaondoka duniani
Hawana nia ya kuwasaidia watanzania. Wangekuwa na nia wangeishaleta msukosuko wa maana. Wakati mwingine huwa nawaza kuwa Chadema na wengine ni mpango wa kuwahadaa washirika wetu wa maendeleo.
 
Huyu Mama kufika 2025 kila mtu atakuwa amemgeuka,Kwa ujumla kama Chadema wakijipanga,plus huruma za wananchi na kupitia Viongozi wa Dini na Asas Zisizokuwa za kiserikali wanachukua inchi kiulaini.Maana mpaluano ulioko huko CCM sio wa kitoto,hata mda wa kuiba kura watakosa
unajidanganya, ccm itoke madarakani kwa Sanduku la kura?
 
🤣🤣🤣👇
16413170897720.jpg
 
Back
Top Bottom