Ukitaka kulia machozi yasiyokwisha agiza hiyo Isuzu Bighorn.
Ni gari comfortable, fuel consumption nzuri,four-wheel gear ya uhakika unapita popote.
Tatizo kubwa ni injini na mfumo wa umeme, gari hii ilinifanya mimi mwenyewe niwe fundi, mzigo ukiwa mikoa ya barid hata Dar, ikishapoa tuu kuiwasha mtiti yaani mpaka ujufunze kuchoma heater direct (nishaungua sanaaa mikono).
Spea zake ni ghaliii sana,turbo lake bovuuu na haina mwendo hyo ni mdogo mdogo mzee.
Niliinunua mwaka 2011 ikanitesa sanaaa,haiuziki nimeitelekeza mkoani mbeya mpaka leo hii halina mteja.
Narudia tena ni bovu bovu bovu sanaaaa,mimi ni mtunzaji sana wa magari lakini hapo nilikwama.
Ukija kwenye grand vitara,nayo ni nzuri ila tatizo lake kubwa ni kula oil ndio maana wengi wanakaanga injini zake deile,nilipata kuinunua mwaka 2015 ikanifia mwaka huo huo,niliweka oil ya BP kwenye service lakini ngoma ilienda arusha ile kurudi nishakaanga wakati nilipima oil nikaona ipo vizuri,hii nayo vipuri vyake ni ghari sana,nikafanya overhaul ya injin nikaiuza.
Nikaamua kuhamia Toyota ambako sikudumu sana nikahamia magari ya ulaya ndio nimepata pumziko la moyo