Isuzu Bighorn vs Suzuki Grand Escudo?

Isuzu Bighorn vs Suzuki Grand Escudo?

Wakuu nataka kuagiza Gari SUV Japan. Katika kuperuzi nimeangukia katika Gari hizo 2 naombeni ushauri wenu Isuzu Bighorn (Diesel 3000cc) vs SUZUKI GRAND ESCUDO (Petrol 2730cc). Nichukue ipi? Ukizingatia barabara off-road na spea Tanzania. Mafuta usihofu nayamudu

View attachment 1928570

View attachment 1928571

View attachment 1928573

View attachment 1928574
Maisha bila gari Mjini Lazima uonekane mvivu tu. Yaan lofa

big_beautiful_heart_20200611_233424_0.jpg
 
Ukitaka kulia machozi yasiyokwisha agiza hiyo Isuzu Bighorn.

Ni gari comfortable, fuel consumption nzuri,four-wheel gear ya uhakika unapita popote.

Tatizo kubwa ni injini na mfumo wa umeme, gari hii ilinifanya mimi mwenyewe niwe fundi, mzigo ukiwa mikoa ya barid hata Dar, ikishapoa tuu kuiwasha mtiti yaani mpaka ujufunze kuchoma heater direct (nishaungua sanaaa mikono).

Spea zake ni ghaliii sana,turbo lake bovuuu na haina mwendo hyo ni mdogo mdogo mzee.

Niliinunua mwaka 2011 ikanitesa sanaaa,haiuziki nimeitelekeza mkoani mbeya mpaka leo hii halina mteja.

Narudia tena ni bovu bovu bovu sanaaaa,mimi ni mtunzaji sana wa magari lakini hapo nilikwama.

Ukija kwenye grand vitara,nayo ni nzuri ila tatizo lake kubwa ni kula oil ndio maana wengi wanakaanga injini zake deile,nilipata kuinunua mwaka 2015 ikanifia mwaka huo huo,niliweka oil ya BP kwenye service lakini ngoma ilienda arusha ile kurudi nishakaanga wakati nilipima oil nikaona ipo vizuri,hii nayo vipuri vyake ni ghari sana,nikafanya overhaul ya injin nikaiuza.

Nikaamua kuhamia Toyota ambako sikudumu sana nikahamia magari ya ulaya ndio nimepata pumziko la moyo
Bwana mkubwa njoo pm unipe iyo gari endapo tu ina engine code UBS73 4jx1 ila kama ni UBS69 4JG2 hapana.
2816355_e.jpeg
[emoji107]
 
Hii bighorn tuzungumze,nife nayo.
Usije tamani kunirudishia mzee haaa haa na hela nikawa nishakula,ile ngoma kuna siku nashuka chimala nikitokea matamba ile milima ya kule hata kitonga na sekenke inasubiri mbali sanaaa,taa zikazima ghafla na brek zikapotea nikazima gari na kuiwasha ikiwa bado imechanganya ikakubali kuwaka nikatembea nayo bila taa mpaka brek zilipokubali,siku hiyo ndio nilijua kuna Mungu aisee
 
Tupe experience ya SUZUKI
Siku 1 nitafte nikupeleke pale ilala mtaa wa shauri moyo,kuna mwamba 1 amezikusanya pale za kutosha ukifika pale half engine J20 inauzwa 9 milion na jamaa hapunguzi bei,halafu yeye ndio anaanza kukubembeleza wewe umuuzie chuma yako kama wenzio walivozitelekeza hapo kabla haijaoza.

Nilitamani kulia yaani ndio ilikua gari yangu ya kwanza ghari zaidi nililipa milion 37 japani
 
Back
Top Bottom