Itachukua Miaka Mingi Kumpata Rais Samia Mwingine Mwenye moyo wa upendo, uvumilivu, Hekima, Busara, Unyenyekevu, Subira, Usikivu na uzalendo

Itachukua Miaka Mingi Kumpata Rais Samia Mwingine Mwenye moyo wa upendo, uvumilivu, Hekima, Busara, Unyenyekevu, Subira, Usikivu na uzalendo

Moyo wa ufisadi siku hizi unaitwa kuwa ni moyo wa upendo,uvumilivu,hekima,busara,unyenyekevu,usikivu,uzalendo?!
 
Waliokwambia kuwa ingekuwa kipindi cha ukoloni ungekuwa nyapara na kuonea waafrika wenzako hawakukosea, it's just a matter of time haijalishi majibu ya unachokifanya humu ndani ya jukwaa yatakufanya uiache hii ID yako kwa aibu.

Kwa akili kama hii ikitawala kwa kijana wa kitanzania tunamiaka 200 ya kupata maendeleo.

NB: Chukua ushauri wa Pascal Mayala aliokupa ukiwa unaisema CHADEMA itakusaidia sana.
 
Moyo wa ufisadi siku hizi unaitwa kuwa ni moyo wa upendo,uvumilivu,hekima,busara,unyenyekevu,usikivu,uzalendo?!
View attachment 2427614
Hapo mh Rais alikuwa anawaasa kuwa wazalendo kwa Taifa letu na waridhike na like wakipatacho kwa mujibu wa sheria. Wasipatwe na Tamaa ya kujipatia vipato vikubwa kinyume na sheria
 
Ndugu zangu Ni viongozi wachache Sana wenye moyo Kama alionao Rais mama Samia, Wenye uwezo wa kuvumilia kukosolewa na kila mtu na yeyote, mwenye uwezo wa kumsikiliza kila mtu bila kujari itikadi za kisiasa,mwenye uwezo wa kukaa mezani na yeyote kujadili masuala ya kitaifa,mwenye uwezo wa kusoma maandishi ya kila mtu bila kujali aina ya maandishi na mtu aliyeandika ,mwenye uwezo wa kusikiliza sauti zote bila kujari aina ya sauti na mahali zilikotoka

Ni wachache Sana wenye kifua Cha uongozi na ngozi ya kiuongozi Kama aliyonayo Rais Samia, Mama yetu anatambua mamlaka aliyonayo kikatiba na kisheria namna yalivyo makubwa, Rais Samia Anafahamu nguvu aliyonayo katika ulimi wake na mikononi mwake kupitia kalamu ya maagizo, anafahamu yeye ndiye Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama lakini huwezi ukamsikia akijivunia madaraka na mamlaka hayo aliyonayo kikatiba na kisheria.

Huwezi kumsikia akitoa lugha za vitisho kwa raia wake Wala maneno ya dharau au kuwakatisha Tamaa watu, Ni mama anayezungumza ukweli muda wote,Ni mama na kiongozi anayeongea uhalisia wa kinachoendelea katika serikali yake,Moyo wake umejaa upendo uvumilivu uzalendo unyenyekevu ujasiri Subira hekima na busara. Ni kiongozi anayetoa maneno katika kinywa chake yakiwa hayana ukakasi Wala kutisha au kukatisha Tamaa au kuwagawa watu

Tanzania Ina amani utulivu na upendo miongoni mwa watanzania kwa kuwa Rais Samia amekuwa kiunganishi Cha Taifa na Mfariji wa Taifa, kiongozi wa wote.karuhusu kutamalaki na kushamiri kwa Uhuru,watu wapo huru kuzungumza na kukosoa,watu wapo huru kueleza dukuduku zao bila hofu,hakuna mwenye Hofu Wala wasiwasi katika kutoa na kueleza hisia zao.Hii ndio sababu hata upinzani hauna ushawishi kwa watanzania kwa kuwa watu wanajisemea wenyewe kwa vinywa vyao na serikali yao inawasikiliza na kufanyia kazi maoni yao,hii yote Ni kwa kuwa Rais Samia Ni Msikivu na mvumilivu na kuwafanya watanzania kuwa na amani katika mioyo Yao,Hakuna aliyebeba sumu kinywani Mwake,Watanzania wanazungumza amani na upendo,Subira na uvumilivu, kuvumiliana na kuheshimiana, kupendana na kushirikiana.

Ukitaka ufahamu namna mh Rais mama Samia alivyomvumilivu na mwenye kifua Cha kiuongozi angalia namna ambavyo watanzania wengi wanavyokosa uvumilivu pale wanapokosolewa,unakuta mtu kwenye Ukurasa wake wa kijamii Kama vile Twitter au Facebook hata humu jamii forum akikosolewa kidogo unakuta anapolomosha matusi utafikiri Kuna mishipa ya fahamu imekatika kichwani,au unakuta ana wa block wote wanaomkosoa

Sasa Kama mtu siyo kiongozi na Hana mamlaka yoyote Yale lakini anakosa uvumilivu je Ni vipi atawavumilia watu wanaomkosoa pale Atakapokuwa na madaraka makubwa ya kutoa Amri? Ni vipi atakaa meza moja na mpinzani wake mkuu kutafuta suluhu na kujenga nchi kwa pamoja Kama afanyavyo mama yetu mpendwa mama Samia? Mtu wa namna hii akipewa madaraka makubwa ya kiuongozi Ni lazima atawaumiza wakosoaji wake kwa namna yoyote Ile atakayoona inafaa na itakayomhakikishia usalama masikioni mwake.

Ndio maana nasema kuwa itatuchukua miaka mingi Sana kumpata Rais Samia Mwingine Mwenye moyo Wa upendo uvumilivu Hekima Busara Unyenyekevu Subira Usikivu Na uzalendo , Mwenye uwezo wa kusikiliza sauti zote na kusoma maandishi yote bila kumuumiza mtu zaidi ya kuhubiri HAKI tu katika kinywa chake Msamiati ambao Ni mgumu na mchungu kutoka katika vinywa vya Baadhi ya Viongozi wa kiafrika waliopo Madarakani.

Watanzania Tuendelee kumwamini Rais wetu na Tuendelee kumuunga mkono Mama yetu na Tuhakikishe kuwa Tunamwombea uzima na Afya njema na kuhakikisha kuwa Uchaguzi ujao anapata Nafasi ya Kuendelea kuliongoza Taifa letu na kututumikia watanzania kwa moyo wa uzalendo na upendo Kama alio uonyesha kwa Sasa katika kuijenga nchi yetu na kuipeleka mbele kimaendeleo

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu:0742-676627
"You can fool some people some times but you cant fool all the people all the time"

Bob Marley
 
Waliokwambia kuwa ingekuwa kipindi cha ukoloni ungekuwa nyapara na kuonea waafrika wenzako hawakukosea, it's just a matter of time haijalishi majibu ya unachokifanya humu ndani ya jukwaa yatakufanya uiache hii ID yako kwa aibu.

Kwa akili kama hii ikitawala kwa kijana wa kitanzania tunamiaka 200 ya kupata maendeleo.

NB: Chukua ushauri wa Pascal Mayala aliokupa ukiwa unaisema CHADEMA itakusaidia sana.
Jibu hoja kwa hoja na siyo hoja kwa vihoja,Mimi Kama mtanzania nawasilisha mtizamo wangu juu ya kile nachokiona na kukishuhudia katika uongozi wa Rais Samia
 
Wakati wa Nyerere uliona nini? wakati wa mwinyi uliona nini? Wakati wa Mkapa Uliona nini? Wakati wa Kikwete uliona nini? Wakati wa JPM uliona nini?
Kila Zama na kitabu chake na kila Ukurasa na habari take,Hizi Ni Zama za mh Mama Samia zilizo has matumaini kwa watanzania ambapo kila mtanzania anaona fursa ya kuinuka kiuchumi katika uongozi huu wa Rais Samia,kwa kuwa katoa nafasi ya watanzania kupiga hatua za kimaendeleo kwa kuweka mazingira wezeshi.mfano Tumeona namna alivyowawezesha wakulima katika kilimo kwa kutoa mbolea za Ruzuku
 
Narudia tena, acha sifa za kijinga.
Rais Samia Anastahili sifa na pongezi kwa kazi kubwa na ya kutukuka aliyoifanya katika kulitumikia na kulijenga Taifa letu ambalo kwa Sasa kinaheshimika kila mahali utakapokwenda
 
Lucas unaishi wapi mwezetu maana unasifu vitu ambavyo mtaani havipo umeme tabu, maji tabu, mfumuko wa bei juu, any way inafaa nikuweke ignore tu mkuu
 
Daah asitokee mwingine tena.

Please GOD!!!!
 
Rais Samia Anastahili sifa na pongezi kwa kazi kubwa na ya kutukuka aliyoifanya katika kulitumikia na kulijenga Taifa letu ambalo kwa Sasa kinaheshimika kila mahali utakapokwenda

Anastahili pongezi toka kwanyie chawa wake.
 
Anastahili pongezi toka kwanyie chawa wake.
Anastahili pongezi kutoka kwa watanzania Ambao kwa macho yao wameona namna mh Rais alivyoiheshimisha Tanzania na kuwa Taifa la kupigiwa mfano na chaguo namba moja kwa wawekezaji na watalii kutoka kila pembe ya Dunia
 
Anastahili pongezi kutoka kwa watanzania Ambao kwa macho yao wameona namna mh Rais alivyoiheshimisha Tanzania na kuwa Taifa la kupigiwa mfano na chaguo namba moja kwa wawekezaji na watalii kutoka kila pembe ya Dunia

Chaguo la wawekezaji kwa huu mgao wa umeme?!
 
Back
Top Bottom