Kibosho1
JF-Expert Member
- Dec 12, 2017
- 2,621
- 4,293
Hakuna kitu kinauma kama majuto,majuto yanauma zaidi sababu yanakuja baada ya muda kupita. Hakuna aliewahi kurudisha nyuma muda akafanikiwa. Nyakati za Yesu alipingwa sana japo alisaidia wengi, aliponya wengi lakini bado alionekana si kitu. Baada ya kufa ndio walijua kuwa hakika alikua mwana wa Mungu.
Toka nipate akili sikuwahi kuona kiongozi mwenye uthubutu kama Magufuli, hakuwa muoga, alikua mkali na aliogopeka na kila mtu. Mwaka 2015 kabla ya ufunguzi maoni ya Watanzania wengi walitaka kiongozi mkali, ili asimamie vizuri mali zao na aache kucheka na wezi.
Magufuli alijitahidi sana kutimiza hilo, serikalini kulikuwa na nidhamu ya kweli, mnyonge alipata furaha lakini kama ujuavyo katika dunia hii hutaweza kumridhisha kila mwanadamu. Magufuli hakuwa malaika asiwe na kasoro, pamoja na kasoro yake alimizia mengi kuliko matarajio ya wengi.
Harakati za kumpiga vita mitandao ni kubwa sana kuliko mitaani, hali ya kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja sio powa sana lakini ameimarisha miundombinu. Online Tanzania hatakiwi wakati Wakenya waliomba awe rais wao.
JK akitukanwa sana lakini alikumbukwa baada ya muda mfupi. Magufuli ni jiwe walilolikataa waashi lakini litakuwa jiwe kuu la pembeni muda si mrefu.
Miradi kama SGR, mwendo kasi Mbagala, kujenga mji mkuu Dodoma n.k vinaweza kusimama au kuchukua muda mrefu kama kiongozi anaeingia hatavaa viatu vyake vizuri. Binafsi naamini Magufuli atakumbukwa zaidi ya marais wote Tanzania.