Itachukua muda mrefu sana kupata jiwe hili wajenzi walilolikataa

Itachukua muda mrefu sana kupata jiwe hili wajenzi walilolikataa

Kaka Watanzania wengi ufahamu wao ni mdogo sana kumambanua Mambo. Muda mwingi tumekua watu wa Majuto.

Mimi niseme ukweli 2015 siku mpigia Ndugu Magufuli. Kutokana na Siasa za Upinzani na waliyotuaminisha kwamba nchi yetu inaibiwa sana na serikali ya chama cha Mapinduzi imeshindwa kudhibiri wizi na ufisadi unaopelekea Umaskini na mateso mengi kwa wananchi wake.

Na kumbuka siku huyu bwana Alipotangazwa ulikua Msiba mzito sana kutokana na Matokeo kutoka tofauti na Matarajio yetu.

Lakini Na kumbuka baada ya kuanza kuona jitihada za dhati kabisa Ambazo huyu Mzalendo wa ukweli kabisa kuanza kufanya Taratibu nilianza kumpenda na kumwelewa.

Maana wale Ambao walituaminisha Ufisadi ndio wakageuka wapinga mema Aliyoyafanya Huyu Mzalendo wa Kweli kabisa.

Kaka Mimi nimekaa nikawaza sana juu ya jambo hili kwa nini Mungu Ameliruhusu?

Nikapata jibu 1
Watanzania wameikanyaga Lulu Ambayo Mungu Alitupatia. Hawa kuona Thamani Yake na wamekufuru hivyo Mungu Ameamua kuchukua Lulu Yake ili tupate tulichokua tunakitaka na kukataa MTU Mwema kama huyu.

Nimalizie kwa kusema
Kila jicho litamwombolezea na kusema heri kama siku za Magufuli zingerudishwa tunge Mzunguka na Kumbariki kwa Matendo Yake Mema Aliyotutendea. Muda utaongea.
[emoji106]
 
Mungu akubariki mkuu.... tuombeane uzima tuliomtukana jana tutamhitaji kesho.

Rais sio Mungu ni binadamu mwenye kasoro zake kama ilivyo kwako na kwangu.

JPM alikuwa na mapungufu yake kama binadamu. Alikuwa mthubutu, mpenda nchi yake na mpenda watu wa hali ya chini.

Muda ni wakati hata miezi sita haipiti tutamhitaji.
[emoji106]
 
Uliyoyaandika hapa hata kwa akina Maalim Seif, Mandela, Nyerere tuliowaanzishia michakato ya uana kheri yanawahusu?

Huyu bwana chini yake wamekufa wengi kwa Corona. Achilia mbali kina Ben na kina Azory.

Huo ndiyo ulio ukweli mchungu.

Tulipo ashukuriwe mola mwanzo mpya barakoa na social distancing ziwe kipaumbele.


Kama umeanza kujitambua katika Magufuli’s regime hakika whatever happened utaona ni vya kustaajabisha!

But in life and in every regime, senile occurrences do happen and they are unfortunately crazy and unbelievable!

Namuombea kheri mwandazake! Muumba ampe pumziko na mwanga wa milele! Ameen!
 
Ni ukosefu tubwa akili kuelekeza nguvu zako katika kumtegemea mtu mmoja swala la yeye kuogopeka halina tija..jambo la msingi ni kuweka mifumo imara ya kiutendaji na utekelezaji maana hadi muda huu tunaweza kurudi square one..kwaio alichokifanya kinakia hakina maana...sababu nguvu nyingi alijiwekezea yeye mwenyewe
 
Mimi ni mchaga alitutenga sana lakini bado,shida inakuja nani atakuwa nafuu? Jibu hakuna waliobaki wote ni mzigo tu.

Ukitanguliza mapenzi binafsi huezi kama ana maana kwako ila angalia faida za pamoja ndio utamuona ni mtu tofauti sana.
Faida zipi za pamoja unazozisema wewe.
Alipotufikisha Kuna tofauti gani na Mtu aliye na pesa nyingi lkn za madawa.hali vzr halali vzr .Mzee katuacha watanzania tumetengana kwaajili ya vyama vya siasa ambavyo yeye ndio alikuwa mlezi lkn akaamua kubezi upande mmoja.leo tuna ndugu zetu wengi tu magereza wanaozea huko kwa sbb ya siasa.kuna sbb gani yakumkubali mtt wa kambo alafu umnyanyase si Bora kumkataa.
 
Huenda anayekuja akawa mkal kuliko pilipil.
ukumbuke tayari utendaj role model umeshaonekana,
viongoz wataooteuliwa huenda wakaomgeza kasi kushind ile ya awal.na hio ndio dira na mtaji wa Ccm.
wakipiga kazi 2025 yan kuteleza utakua ushind wa kishindo
 
Ulipata akili lini?
Hakuna kitu kinauma kama majuto,majuto yanauma zaidi sababu yanakuja baada ya muda kupita. Hakuna aliewahi kurudisha nyuma muda akafanikiwa. Nyakati za Yesu alipingwa sana japo alisaidia wengi, aliponya wengi lakini bado alionekana si kitu. Baada ya kufa ndio walijua kuwa hakika alikua mwana wa Mungu.

Toka nipate akili sikuwahi kuona kiongozi mwenye uthubutu kama Magufuli, hakuwa muoga, alikua mkali na aliogopeka na kila mtu. Mwaka 2015 kabla ya ufunguzi maoni ya Watanzania wengi walitaka kiongozi mkali, ili asimamie vizuri mali zao na aache kucheka na wezi.

Magufuli alijitahidi sana kutimiza hilo, serikalini kulikuwa na nidhamu ya kweli, mnyonge alipata furaha lakini kama ujuavyo katika dunia hii hutaweza kumridhisha kila mwanadamu. Magufuli hakuwa malaika asiwe na kasoro, pamoja na kasoro yake alimizia mengi kuliko matarajio ya wengi.

Harakati za kumpiga vita mitandao ni kubwa sana kuliko mitaani, hali ya kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja sio powa sana lakini ameimarisha miundombinu. Online Tanzania hatakiwi wakati Wakenya waliomba awe rais wao.

JK akitukanwa sana lakini alikumbukwa baada ya muda mfupi. Magufuli ni jiwe walilolikataa waashi lakini litakuwa jiwe kuu la pembeni muda si mrefu.

Miradi kama SGR, mwendo kasi Mbagala, kujenga mji mkuu Dodoma n.k vinaweza kusimama au kuchukua muda mrefu kama kiongozi anaeingia hatavaa viatu vyake vizuri. Binafsi naamini Magufuli atakumbukwa zaidi ya marais wote Tanzania.
 
Mungu akubariki mkuu.... tuombeane uzima tuliomtukana jana tutamhitaji kesho.

Rais sio Mungu ni binadamu mwenye kasoro zake kama ilivyo kwako na kwangu.

JPM alikuwa na mapungufu yake kama binadamu. Alikuwa mthubutu, mpenda nchi yake na mpenda watu wa hali ya chini.

Muda ni wakati hata miezi sita haipiti tutamhitaji.
Neno lako ni zito mnooo kulibeba yahitaji nguvu ya Mungu
 
Back
Top Bottom