greenwoods
JF-Expert Member
- Sep 21, 2020
- 2,328
- 3,955
Dah! Nasoma huu uzi uku natokwa na machozi.pumzika rais wangu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji106]Kaka Watanzania wengi ufahamu wao ni mdogo sana kumambanua Mambo. Muda mwingi tumekua watu wa Majuto.
Mimi niseme ukweli 2015 siku mpigia Ndugu Magufuli. Kutokana na Siasa za Upinzani na waliyotuaminisha kwamba nchi yetu inaibiwa sana na serikali ya chama cha Mapinduzi imeshindwa kudhibiri wizi na ufisadi unaopelekea Umaskini na mateso mengi kwa wananchi wake.
Na kumbuka siku huyu bwana Alipotangazwa ulikua Msiba mzito sana kutokana na Matokeo kutoka tofauti na Matarajio yetu.
Lakini Na kumbuka baada ya kuanza kuona jitihada za dhati kabisa Ambazo huyu Mzalendo wa ukweli kabisa kuanza kufanya Taratibu nilianza kumpenda na kumwelewa.
Maana wale Ambao walituaminisha Ufisadi ndio wakageuka wapinga mema Aliyoyafanya Huyu Mzalendo wa Kweli kabisa.
Kaka Mimi nimekaa nikawaza sana juu ya jambo hili kwa nini Mungu Ameliruhusu?
Nikapata jibu 1
Watanzania wameikanyaga Lulu Ambayo Mungu Alitupatia. Hawa kuona Thamani Yake na wamekufuru hivyo Mungu Ameamua kuchukua Lulu Yake ili tupate tulichokua tunakitaka na kukataa MTU Mwema kama huyu.
Nimalizie kwa kusema
Kila jicho litamwombolezea na kusema heri kama siku za Magufuli zingerudishwa tunge Mzunguka na Kumbariki kwa Matendo Yake Mema Aliyotutendea. Muda utaongea.
[emoji106]Mungu akubariki mkuu.... tuombeane uzima tuliomtukana jana tutamhitaji kesho.
Rais sio Mungu ni binadamu mwenye kasoro zake kama ilivyo kwako na kwangu.
JPM alikuwa na mapungufu yake kama binadamu. Alikuwa mthubutu, mpenda nchi yake na mpenda watu wa hali ya chini.
Muda ni wakati hata miezi sita haipiti tutamhitaji.
Uliyoyaandika hapa hata kwa akina Maalim Seif, Mandela, Nyerere tuliowaanzishia michakato ya uana kheri yanawahusu?
Huyu bwana chini yake wamekufa wengi kwa Corona. Achilia mbali kina Ben na kina Azory.
Huo ndiyo ulio ukweli mchungu.
Tulipo ashukuriwe mola mwanzo mpya barakoa na social distancing ziwe kipaumbele.
Faida zipi za pamoja unazozisema wewe.Mimi ni mchaga alitutenga sana lakini bado,shida inakuja nani atakuwa nafuu? Jibu hakuna waliobaki wote ni mzigo tu.
Ukitanguliza mapenzi binafsi huezi kama ana maana kwako ila angalia faida za pamoja ndio utamuona ni mtu tofauti sana.
Hao si kitu kwako?Au kuna nafsi ya thamani na isiyo ya thamani?.VIP wasiojulikana?kwa hyo wewe umeona ben na azory ujaona aliyoyatenda huyu kiongoz acheni unafk aiseeee
Hakuna kitu kinauma kama majuto,majuto yanauma zaidi sababu yanakuja baada ya muda kupita. Hakuna aliewahi kurudisha nyuma muda akafanikiwa. Nyakati za Yesu alipingwa sana japo alisaidia wengi, aliponya wengi lakini bado alionekana si kitu. Baada ya kufa ndio walijua kuwa hakika alikua mwana wa Mungu.
Toka nipate akili sikuwahi kuona kiongozi mwenye uthubutu kama Magufuli, hakuwa muoga, alikua mkali na aliogopeka na kila mtu. Mwaka 2015 kabla ya ufunguzi maoni ya Watanzania wengi walitaka kiongozi mkali, ili asimamie vizuri mali zao na aache kucheka na wezi.
Magufuli alijitahidi sana kutimiza hilo, serikalini kulikuwa na nidhamu ya kweli, mnyonge alipata furaha lakini kama ujuavyo katika dunia hii hutaweza kumridhisha kila mwanadamu. Magufuli hakuwa malaika asiwe na kasoro, pamoja na kasoro yake alimizia mengi kuliko matarajio ya wengi.
Harakati za kumpiga vita mitandao ni kubwa sana kuliko mitaani, hali ya kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja sio powa sana lakini ameimarisha miundombinu. Online Tanzania hatakiwi wakati Wakenya waliomba awe rais wao.
JK akitukanwa sana lakini alikumbukwa baada ya muda mfupi. Magufuli ni jiwe walilolikataa waashi lakini litakuwa jiwe kuu la pembeni muda si mrefu.
Miradi kama SGR, mwendo kasi Mbagala, kujenga mji mkuu Dodoma n.k vinaweza kusimama au kuchukua muda mrefu kama kiongozi anaeingia hatavaa viatu vyake vizuri. Binafsi naamini Magufuli atakumbukwa zaidi ya marais wote Tanzania.
Neno lako ni zito mnooo kulibeba yahitaji nguvu ya MunguMungu akubariki mkuu.... tuombeane uzima tuliomtukana jana tutamhitaji kesho.
Rais sio Mungu ni binadamu mwenye kasoro zake kama ilivyo kwako na kwangu.
JPM alikuwa na mapungufu yake kama binadamu. Alikuwa mthubutu, mpenda nchi yake na mpenda watu wa hali ya chini.
Muda ni wakati hata miezi sita haipiti tutamhitaji.