Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Nikiri wazi kuwa sijawahi kufikiria wala kuwazia wala kutizamia wala kuota wala kutarajia wala kuona Eti Lissu akichukua Fomu ya Kuomba Kuongoza CHADEMA kama Mwenyekiti wake Taifa.
huu ni utani ,huu ni Mzaha anaoufanya Lissu kwa sababu hana uwezo huo wa kuongoza CHADEMA. kwa sababu kuiongoza CHADEMA siyo suala la makelele, mihemuko, ukurupukaji, uropokaji na Jazba.Ni suala la akili kubwa za kiuongozi, utulivu na hekima ambazo kwa bahati mbaya lissu hajajaliwa kuwa navyo.
Embu Sikilizeni na Tulieni niwapeni Darasa kidogo kuwa itakuwa ni Uwendawazimu na ukichaa wa hali ya juu kabisa ikiwa wana CHADEMA watathubutu na kukubali kumpa Lissu nafasi ya kuwa Mwenyekiti wake Taifa.
Ni hivi Lissu Hana busara, hana hekima, hana subira, hana uvumilivu, hana kifua cha uongozi, hawezi kuwa mtu wa Mwisho pale pasipo kuwa na mtu juu yake wa kumuongoza Njia. Lissu hajakomaa kiuongozi kushika nafasi hiyo nyeti kwa chama kikuu cha upinzani kinachomhitaji mtu makini, mvumilivu na mtulivu aina ya Mwamba Mbowe.
Pia, Soma:
• Tundu Lissu atangaza nia ya kugombea nafasi ya uenyekiti CHADEMA
Kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA ni kazi Ngumu sana kuliko hata kazi ya kugombea Urais zoezi ambalo linafanyika kwa muda mfupi tu. kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA ni kazi nzito, kazi ya msalaba, kazi ya Mateso, kazi ya kujitoa mhanga, kazi ya kukubali kupoteza mali zako, jasho lako, kuvuja Damu yako, kukosana na kukimbiwa na watu, kuogopwa hata kupigiwa simu na baadhi ya watu wa serikalini au hata kupewa nafasi ya kuzungumza na kuonekana ni adui wa usalama, Amani na utulivu wa Taifa.
Leo hii huyu lissu ambaye alikuwa analia lia kila siku kudai hela zake za matibabu, mara stahiki zake za ubunge anaweza vipi kuvumilia kupoteza Mabilioni ya pesa, vitega uchumi na Biashara zake?
Mumewahi kumsikia wapi Mwamba Mwenyewe na jabali la Siasa za Upinzani katika ukanda huu wa Afrika mashariki akilia, kupiga makelele na kulalamika na kuomba huruma hadharani ya kutaka alipwe?
Lini mmewahi kusikia Mwamba Mbowe akipigania maslahi yake binafsi badala ya maslahi ya chama chake na watanzania? Lakini Lissu kwa uroho wake wa pesa, tamaa na ufisi wa kutaka mapesa alikimbia hata kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kile kilichoitwa kufuatilia na kutaka kufungua kesi kupitia mawakili wake ili alipwe mabilioni ya Pesa na kampuni ya mawasiliano. Maana yake anajijali sana maslahi yake binafsi kuliko hata ustawi wa chama chake.
Lissu huyu aliyekuwa akikimbia kimbia kwenda na kuishi uhamishoni anaweza vipi kuiongoza CHADEMA chama kikuu cha upinzani katika nyakati ngumu kama alivyofanya Mwamba Mwenyewe Mbowe?
Kama anaogopa kufa na kukimbia ni vipi anaweza wapa matumaini wafuasi wake ilihali yeye yupo nje ya nchi akinywa mipombe na minyama na kujipost Utafikiri mtu aliyepotea na anatafutwa?
Lini mmewahi kuona Mwamba Mbowe akikimbia Nchi yake? Lini mmewahi kuona Mwamba akitorokea mipakani au kujificha kwenye balozi za kigeni kama alivyofanya Lissu 2020? Kwanini Mwamba Mbowe hakimbii na kuwatelekeza wafuasi wake?
Mwamba amekubali liwalo na liwe na yupo tayari kufia katika ardhi ya Tanzania aliyozaliwa kwa sababu anajua na kufahamu ya kuwa ukiwa kiongozi unapaswa kuwa mbele ya unaowaongoza wakati wa hali ngumu ili kuwapa matumaini na morali ya mapambano,anafahamu kuwa amebeba dhamani kubwa mabegani mwake.
Unajua kuwa kiongozi wa upinzani kwa Nchi za kiafrika ni kubeba msalaba na gharama mbalimbali huku ukipenda na kutanguliza mbele maslahi ya Taifa lako. Ndio Maana Mbowe Mwamba Mwenyewe amekubali kulipa gharama nyingi sana kwa yeye kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA.
Ni ulimi, akili, maarifa, hekima, diplomasia, uongozi na ushawishi mkubwa alionao Mwamba Mbowe uliomfanya Lissu kurejea hapa Nchini baada ya vikao vingi kufanyika na yeye akiwa kiongozi kwa upande wa CHADEMA.
Lissu ni mtu mwenye mihemuko, mropokaji, mwenye kujaa jazba, hasira, ukurupukaji, asiye na staha wala subira wala uvumilivu wala hekima wala kifua cha kiuongozi wala ushawishi kweye taasisi mbalimbali na watu mbalimbali kama ilivyo kwa Mheshimiwa Mwamba Mbowe jabali la siasa za Upinzani.
Lissu na siasa zake za kutaka jino kwa jino atamuongoza na kumshawishi nani amuunge mkono? Watanzania wa leo hawapo tayari kurejea majeraha ya kufa, kuachwa na ukilema na kuumizwa kwa sababu ya siasa za mtu anayeshindwa kutumia sayansi ya siasa.
Watanzania kiasili hawapendi siasa za jino kwa jino au vurugu zinazoweza kupelekea kupoteza maisha na kumwaga Damu zao. Ndio Maana lissu alipowaambia waandamane 2020 walimgomea katakata.
Mwamba Mbowe ni mtu sahihi kwa CHADEMA kwa sasa kuliko wakati mwingine wowote ule kwa sababu Mwamba ni Mtu anayekipenda CHADEMA kwa dhati ya Moyo wake. Lissu haipendi CHADEMA bali anapenda Maslahi yake kwa kuitumia CHADEMA kama chambo.
Ndio maana hata uchaguzi uliopita hakupiga kura kusaidia chama chake kupata ushindi maana hana uchungu nacho hata kikifa tu.
Mbowe ni mtu na kiongozi mwenye ushawishi mkubwa sana ndani na nje ya chama chake. Ni mtu anayeaminika na unayeweza kumuanini na kupanga naye mipango, mikakakti na hata kuridhiana. Lissu hana ushawishi ndani ya CHADEMA na hata nje ya CHADEMA.
Hii ni kutokana na mdomo wake unaongea bila breki wala kipimo wala mipaka wala kujua yeye ni kiongozi wala aongee nini na wakati gani na kipi asiongee hadharani bali kwenye vikao rasmi tu au faragha. Lissu huwezi kupanga naye siri au mikakati halafu siri na mikakati hiyo isivuje.
Lissu ni mkubwa kiumri ila bado sana kukomaa, amejaa mihemuko utafikiri watoto wa sekondari hususani wa kidato cha pili na tatu. Hana utulivu kabisa wa kiuongozi kuweza kuongoza chama, hana umakini katika kauli zinazotoka kinywani pake, akichokonolewa kidogo tu kwa mtego unaona namna anavyo lipuka kila kitu.
Mdomo wa lissu utakisambaratisha na kukipasua CHADEMA vipande vipande kama kioo, mdomo wa lissu utakigawa chama, Lissu ni mtu wa majivuno, dharau sana, hawezi kuvuna mwanachama yeyote yule kutoka chama kingine. Lissu ni mbaguzi sana na ndio maana anafanya wengi wamchukie.
Atafanya kazi ya kuwatukana watu, kupandikiza chuki, kuleta maneno ya kibaguzi ndani ya chama na hata nje.
Ni hatari na hasara kubwa sana kwa chama kama CHADEMA kuwekwa mikononi Mwa Lissu. Hakuna kitu atakacho ipatia CHADEMA wala kuiongezea zaidi ya kuidhoofisha, kupoteza wanachama wake, kuivuruga, kupoteza ushawishi wa chama, kuleta taswira kuwa ni chama cha vurugu. Lissu hana uwezo wa kuwaleta pamoja wanachama wote na wenye mitizamo tofauti tofauti na kuishi nao kwa pamoja kama ambavyo Mwamba amefanya kwa miaka yake yote ya uongozi wake.
Mwamba Mbowe amekuza viongozi wengi sana na kuibua vipaji vya viongozi wengi sana tangia wakiwa vijana ambao wengine sasa wapo hadi serikalini mfano akina Mheshimiwa David Silinde, David Kafulila, mtela Mwampamba, profesa Kitila Mkumbo, Patrobas Katambi, Joshua Nasari, peter Lijuakali, Godwin Mollel, Vicent Mashinji Walikuwepo serikalini pia akina Juliana Shonza, Mwita Waitara, Pauline Gekul na wengine wengi sana.
Mwamba Mbowe Ameishi na kufanya kazi na watu wenye akili za kila aina na kwenda nao vyema sana. Ametukanwa matusi ya kila aina na wale aliowakuza na kuwabeba mabegani mwake lakini bado amebakia kuwa mtulivu sana.Ikumbukwe ya kuwa muogope sana mtu ambaye ametoka leo upinzani akaanza kutukana sana matusi ya huko alikotoka na wote aliowaacha huko.
Kwa sababu siku Moja anaweza kukutukana matusi ya Nguoni hata wewe uliyempokea. Kwa hiyo cha msingi ni kuchora msitari ya wapi aishie kujua na nini na nini afahamu na kipi asifahamu wala kufahamishwa au kushirikishwa.
CHADEMA mpeni Mwamba Heshima yake kwa kumpigia kura nyingi za ndio na kumpa faraja na matumaini ya kuwa mpo naye na mnathamini mchango wake kwa chama chenu. Bila Mbowe kusingekuwa na CHADEMA na hata hao wanaomtukana na kumkejeri wasingepata nafasi ya kufahamika kabisa.
Wengine tumewafahamu wakiwa CHADEMA na hata walipokuja CCM tukawapa nafasi baada ya kuona uwezo wao wakiwa CHADEMA.hiyo yote ni kazi ya Mikono ya Mwamba Mbowe aliyewakuza na kuwapigania japo Malipo yake Ameishia Kutukanwa.
Japo najua mwenye akili Timamu dhamira yake itamhukumu Mwenyewe akiwa Mwenyewe chumbani kwake. Mwamba Mbowe ni Mwanadamu kama tulivyo wanadamu wengine na wala siyo Malaika na katika uwanadamu wake amepigana na kuipigania CHADEMA kwa jasho na Damu na bado anao uwezo na ndiye chaguo sahihi la kuendelea kuiongoza CHADEMA.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.