Italia yaipiku China kwa idadi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa wa Covid 19

Italia yaipiku China kwa idadi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa wa Covid 19

digba sowey

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
8,926
Reaction score
17,880
Wakuu hamjambo?

Nimekuwa nafuatilia kuhusu hili gonjwa la Corona kwa wataliano, naona linawapukutusha kama mti unavyopukutisha majani wakati wa kiangazi.

Idadi ya vifo inasoma 400+ kila siku,angalia hii record ya vifo kwa Jana na Leo, ambapo Jana tu uliua watu 475. Leo hii watu takribani 425 wamekufa.

Mungu awarehemu, maana kwa sasa wanawazidi wachina kwa visa vya vifo, ambapo china Ina record ya 3,225 lakini wataliano idadi inasoma 3,405

Screenshot_20200318-204940~2.jpeg


Inaripotiwa kuwa hadi kufikia leo Alhamisi idadi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa wa Covid 19 imefikia 3405 huku vifo vipya 427 vikitokea leo.

Aidha, idadi hiyo ya vifo nchini Italia inaipiku ile ya China ambapo vifo vilivyotokea ni 3245 tangu iliporipotiwa kwa muathirika wa kwanza mwishoni mwa waka jana.

Hivyo kwa msingi huo, inaonesha kuwa mpaka kufikia sasa taifa la Italia ndilo lililoathirika zaidi na virusi vya Corona ukilinganisha na China ambako ndiko virusi hivyo vilianzia.
1584643050673.png

===
Italy on Thursday overtook China’s coronavirus death toll, with 427 new fatalities taking its total since the first case was registered in February to 3,405.

China has officially reported 3,245 deaths since registering the first infection at the end of last year.
 
Hii ni hatari sasa Italy imeipiku China kwa idadi ya vifo baada ya leo vifo 400+ kuongezeka.
Hivi sababu pekee ni kuwa Italy wana idadi kubwa ya wazee? Najiuliza sehemu zingine za ulaya mbona hapapo hivyo.... Au kuna sehemu walienda wrong....All in all tusiwabeze sana coz huku kwetu ndo imepiga hodi.
God bless Italy
God bless Africa
God Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
-Senior citizens
-Wanapenda kawahawa saana hawa jamaa na migahawa ya pombe....
 
Back
Top Bottom