Itanigharimu kiasi gani kutalii katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti?

Itanigharimu kiasi gani kutalii katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti?

NItafafanua gharama za kuingia hifadhini kuanzia saa 12 asubuhi Hadi saa 12 Jioni (yaaani day trip) pamoja na Aina za usafiri na gharama zake kama ifuatavyo.

1. Kwa kutumia gari Aina ya LAND CRUISER inayofunguka juu (OPEN ROOF) na inayobeba Hadi WATU WANNE(four passenger seats) gharama ni shilingi 560,000/=. Gharama hizi zinahusisha kukodi gari, mafuta, Kodi ya gari inapoingia hifadhini, chakula Cha asubuhi na mchana, kiingilio Cha watu 4.
Mkiwa kikundi Cha watu 4 hapa Kila mmoja atalipia angalau 140,000/=.

2. Kwa kutumia gari Aina ya LAND CRUISER inayofunguka juu (OPEN ROOF) na inayobeba Hadi WATU SITA (six passenger seats) gharama ni shilingi 700,000/=. Jumla ya watu hapa mtakua 6, endapo mtakua pungufu gharama zitapungua kidogo kwenye chakula na kiingilio hifadhini. Kwa kawaida kiingilio ni shilingi elfu kumi na mbili (12,000/=) Kwa mtu mzima kuanzia miaka 16. Watoto chini ya miaka 5 ni bure. Wastani gharama ya chakula Kwa mtu mmoja ni shilingi elfu kumi (10,000/=) Kwa breakfast na lunch.
Mkiwa kikundi Cha watu 6 hapa Kila mmoja atalipia angalau 120,000/=.

3. Kwa kutumia gari Aina ya HIACE inayobeba Hadi WATU 7 HADI 12 gharama ni shilingi 750,000/=. Hapa mnaweza kuwa kikundi Cha Hadi watu 12, endapo mkiwa pungufu gharama zinaweza kupungua kidogo kama nilivyoelezea hapo juu.
Mkiwa kikundi Cha watu 12, hapa Kila mmoja atalipia angalau 65,000/=.

4. Kwa kutumia gari Aina ya COASTER AU TATA inayobeba wastani wa WATU 13 HADI 30 gharama itakuwa ni shilingi 1,500,000/= (milioni Moja na nusu). Mkiwa pungufu ya idadi hiyo gharama itapunguza kidogo pia.
Mkiwa kikundi cha watu 30 hapa Kila mmoja atalipia angalau 50,000/=.

5. Kwa kutumia gari Aina ya NOAH inayoweza kubeba WATU 2 HADI 6 gharama itakuwa shilingi 450,000/= (laki nne na nusu).
Mkiwa kikundi Cha watu 6 hapa Kila mmoja atalipia angalau 75,000/=.


Kumbuka Gharama hizo ni Kwa jumla na zinabadirikabadirika kutokana na Aina ya gari utakayopenda kutumia. Land Cruisers zinazofunguka juu zinafaa zaidi kwani zinanafasi ya kutosha ndani, madirisha makubwa na zinafika popote ndiyo maana zinagharama kubwa kukodi.

Endapo una gari binafsi utagharamika kununua mafuta ambayo yatatosha kuzungumza angalau 300km. Pia utalipia tozo ya gari kutokana na uzito wake. Gharama nyingine utakazolipa ni za kiingilio kutokana na idadi ya watu utakaokuwa nao na pia utamlipa muongoza watalii (tour guide) Ili akupeleke maeneo wanapopatikana wanyama Kwa urahisi. Gharama za tour guide Kwa siku inategemea a ila Kwa wastani ni shilingi elfu hamsini (50,000/=).
Chakula unaweza andaa chako au ukanunua nje ya HIFADHI kupunguza gharama.

Karibu sana mkuu, unaweza nicheki nikakupeleka wakati wote.
Mnaweza ungana mkawa wengi Ili kupunguza gharama ya mmojammoja.
Kumbe siyo garama sana
 
Sasa hizi kodi tunalipa ngap..
Umetoka kigamboni na kagar kako...daraja unalipia...
Umeenda sheli..kodi unalipia..
Umefika serengeti..kodi ya uzito wa gari
Bado uweke mafuta ya 300km..
Kulala unalipia..
Kula unalipia..
Bado swala ajipitishe umfyeke ulipie...
Aaassshh
 
Baba,mama na watoto wawili ni familia ya watu wanne sio watatu 😇😎
Asante Kwa kufafanua kiongozi.
Kwa familia ya watu WANNE (watoto umesema ni chini ya miaka mitano) safari ya siku moja pamoja na kulala(1 day & 1 night) kwa kutumia gari Aina ya Landcruiser itawagharimu jumla shilingi laki saba (700,000/=). Hii inamaanisha kuwa mtakaa ndani ya HIFADHI Kwa masaa 24 pekee. Yaani mkiingia saa 2 asubuhi itabidi mtoke kabla ya saa 2 kesho yake.
Endapo mkitaka kukaa zaidi gharama zitaongezeka kiasi.
 
Unachosema ni ukweli kabisa lakini kutokana na mazingira ya kuwafikia hao nyani ndipo tofauti zinapojitokeza. Pengine inakua bure, pengine unalipia. Kwa mfano, Mimi nilieko Serengeti haiwezi kuwa bure kuja HUKO udsm kuwaona hao nyani. Lazima nigharamike, nilipe nauli, chakula na hata kulala.
Karibu Serengeti Mkuu!
Akati huyo nyani ukienda hapo udsm unawaona bure kabisa.
 
Naunga mkono hoja,

Kwa hizo gharama,
watanzania wengi kuzimudu Ni changamoto.

Wengi wanazeeka mpk wanakufa hawajatembelea vivutio vya ndani.
Kwa mtanzania kuingia hifadhini gharama ni elfu kumi na Moja na mia nane (11,800/=). Hiyo ni tozo ya kiingilio tu. Tatizo ni kwenye usafiri ndugu. Hapo ndipo zinapojitokeza gharama ambazo wengi hawazimudu.
Serikali Haina magari kiivo kusema ndo yatumike kukuzungusha kutalii. Endapo yangekuwepo ya kutosha labda gharama zingepungua zaidi.
 
Asante mkuu. Nilikuwa na ndoto za kuja huko nikitokea SONGEA... Sasa bahati mbaya tumepigwa na kitu kizito. Mbolea ni 107000mfuko. Na mahindi ni elf33gunia. . Ngoja nilime kwanza misimu 10 tena ya mvua
Hahahah misimu 10 ni mingi sana mkuu, Fanya msimu mmoja tu. Karibu sana!
 
Sasa hizi kodi tunalipa ngap..
Umetoka kigamboni na kagar kako...daraja unalipia...
Umeenda sheli..kodi unalipia..
Umefika serengeti..kodi ya uzito wa gari
Bado uweke mafuta ya 300km..
Kulala unalipia..
Kula unalipia..
Bado swala ajipitishe umfyeke ulipie...
Aaassshh
Epuka yote hayo kwa kukaa ndani tu.
 
Mimi nikija na familia na gari langu..natakiwa nilipe 50k tu boss....nipewe mtu anizungushe siku nzima...
BTW, hao watu tunaowalipa si watumishi wa umma?
Hiyo 50k inaweza kuwa tozo ya gari tu mkuu, mtu wa kukuzungusha itabidi uongeze angalau 50k nyingine. Na Chakula uzingatie pia.
Wafanyakazi wa serikali hawausiki kukuzungusha, ni watu binafsi kama sisi yaani tour guides.
Karibu tukuhudumie. 0625818341
 
Muda wote utaenjoy. Kuanzia mwezi wa sita Hadi wa kumi na Moja ndipo Kun wazungu wengi. Lakini siyo maeneo yote ya HIFADHI kwani Serengeti ni kubwa sana ni vigumu kuitembelea yote Kwa siku moja. Mara nyingi wazungu wqnapenda kufuatilia uhamiaji wa nyumbu, kwahiyo inawezekana kuitembelea maeneo mengine ambapo kunakuwa hakuna nyumbu kwani watu wanakuepo wachache.
Gharama ya kulala hostel ni 5600 Kwa usiku ila inakua kama bweni mnalala watu wengi, lodge gharama zinaanzia 20,000 Hadi 1,000,000 na campsite gharama hazitofautiani sana na za lodge.
Kwa safari ya siku moja Kwa budget ya kawaida andaa angalau kuanzia 800,000.
Karibu sana, unaweza nicheki Kwa namba hii nikupe muongozo zaidi....0625818341.
Gharama ya siku moja laki nane? Hii ndo inasababisha mzungu anaweza kuizungumzia Serengeti au Ngorongoro kuliko mwenyeji

Yaani mTanzania anazaliwa mpaka anakufa hajawahi kufika Serengeti au amepita na na Cost line bus la Musoma- Arusha
 
Back
Top Bottom