G'taxi
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 6,625
- 8,639
Kwa gari binafsi umesema mafuta ya kuzunguka 300klmNItafafanua gharama za kuingia hifadhini kuanzia saa 12 asubuhi Hadi saa 12 Jioni (yaaani day trip) pamoja na Aina za usafiri na gharama zake kama ifuatavyo.
1. Kwa kutumia gari Aina ya LAND CRUISER inayofunguka juu (OPEN ROOF) na inayobeba Hadi WATU WANNE(four passenger seats) gharama ni shilingi 560,000/=. Gharama hizi zinahusisha kukodi gari, mafuta, Kodi ya gari inapoingia hifadhini, chakula Cha asubuhi na mchana, kiingilio Cha watu 4.
Mkiwa kikundi Cha watu 4 hapa Kila mmoja atalipia angalau 140,000/=.
2. Kwa kutumia gari Aina ya LAND CRUISER inayofunguka juu (OPEN ROOF) na inayobeba Hadi WATU SITA (six passenger seats) gharama ni shilingi 700,000/=. Jumla ya watu hapa mtakua 6, endapo mtakua pungufu gharama zitapungua kidogo kwenye chakula na kiingilio hifadhini. Kwa kawaida kiingilio ni shilingi elfu kumi na mbili (12,000/=) Kwa mtu mzima kuanzia miaka 16. Watoto chini ya miaka 5 ni bure. Wastani gharama ya chakula Kwa mtu mmoja ni shilingi elfu kumi (10,000/=) Kwa breakfast na lunch.
Mkiwa kikundi Cha watu 6 hapa Kila mmoja atalipia angalau 120,000/=.
3. Kwa kutumia gari Aina ya HIACE inayobeba Hadi WATU 7 HADI 12 gharama ni shilingi 750,000/=. Hapa mnaweza kuwa kikundi Cha Hadi watu 12, endapo mkiwa pungufu gharama zinaweza kupungua kidogo kama nilivyoelezea hapo juu.
Mkiwa kikundi Cha watu 12, hapa Kila mmoja atalipia angalau 65,000/=.
4. Kwa kutumia gari Aina ya COASTER AU TATA inayobeba wastani wa WATU 13 HADI 30 gharama itakuwa ni shilingi 1,500,000/= (milioni Moja na nusu). Mkiwa pungufu ya idadi hiyo gharama itapunguza kidogo pia.
Mkiwa kikundi cha watu 30 hapa Kila mmoja atalipia angalau 50,000/=.
5. Kwa kutumia gari Aina ya NOAH inayoweza kubeba WATU 2 HADI 6 gharama itakuwa shilingi 450,000/= (laki nne na nusu).
Mkiwa kikundi Cha watu 6 hapa Kila mmoja atalipia angalau 75,000/=.
Kumbuka Gharama hizo ni Kwa jumla na zinabadirikabadirika kutokana na Aina ya gari utakayopenda kutumia. Land Cruisers zinazofunguka juu zinafaa zaidi kwani zinanafasi ya kutosha ndani, madirisha makubwa na zinafika popote ndiyo maana zinagharama kubwa kukodi.
Endapo una gari binafsi utagharamika kununua mafuta ambayo yatatosha kuzungumza angalau 300km. Pia utalipia tozo ya gari kutokana na uzito wake. Gharama nyingine utakazolipa ni za kiingilio kutokana na idadi ya watu utakaokuwa nao na pia utamlipa muongoza watalii (tour guide) Ili akupeleke maeneo wanapopatikana wanyama Kwa urahisi. Gharama za tour guide Kwa siku inategemea a ila Kwa wastani ni shilingi elfu hamsini (50,000/=).
Chakula unaweza andaa chako au ukanunua nje ya HIFADHI kupunguza gharama.
Karibu sana mkuu, unaweza nicheki nikakupeleka wakati wote.
Mnaweza ungana mkawa wengi Ili kupunguza gharama ya mmojammoja.
Kilometer 300 ni nyingi sana,huo ni umbali mrefu sana mbona iwapo nitakuja kwa siku moja tu au mbili,wastani angalau nitembee 90kilometer per day