Itapendeza zaidi kuomba radhi, kulinda hadhi ya kuendelea kuitwa mama

T2020

Senior Member
Joined
Jul 15, 2020
Posts
158
Reaction score
361
Mama omba radhi Watanzania kauli yako ya kusubiri kwanza kufufua uchumi ndiyo turuhusu marekebisho ya katiba na mikutano ya kisiasa hii umechemka.

1. Utachukiwa kuliko hata JPM
2. Utapoteza heshima ya kuitwa mama
3. Utazalisha akina Sabaya na Makonda wengi kuliko JPM
4. Unaweza kuwa Rais wa mwisho kutoka Z'bar
5. Mataia ya nje walioanza kukuunga mkono watakugeuka ndani ya muda mfupi
6. Wanufaika wa utawala wa JPM wataungana na wapinzani kukushambulia
7......

Nitaendelea nachaji simu kwanza.
 
Mama kweli akizingua kwenye matakwa ya wananchi anaweza kuchukiwa mara mbili ya alivyochukiwa Magufuli.

Maana calculations anazozifanya Samia ni kudhani kuwa anaweza kuituliza nchi hii kwa kurekebisha makosa ya Magufuli na kujenga uchumi imara peke yake na kwamba suala la katiba mpya linaweza kusubiri tu.

Kwenye kurekebisha makosa ya Magufuli yuko sahihi, kwenye kujenga uchumi yuko sahihi ila kwenye ishu ya katiba mpya amekosea tena amekosea kwelikweli.

Tatizo ninaloliona ni kuwa

1. Anaweza kujikuta anafikia hatua serikali yake ni unpopular sana na sasa ili kudhibiti sauti za wananchi basi naye akajikuta anarudi kulekule kwenye kufanya mambo yaleyale ambayo wananchi waliyoyachukia sana kwenye utawala wa Magufuli ya ubabe, ukatili, uongo mkubwa, propaganda kubwa, kununua wanasiasa kwa kuwahonga pesa na vyeo ili wamuunge mkono, na kuzidisha uonevu ili kunyamazisha sauti za wananchi wanaotaka mabadiliko nchini. Sasa akianza kufanya hayo atachukiwa mara kumi na kwa kuwa yeye siyo Bandidu kihulka kumfikia Magufuli, hatoweza kudhibiti hiyo hali, kimsingi anaweza kusababisha machafuko nchini.

2. Uchumi ni suala endelevu, halina mwisho wa ujenzi wake, Iwapo Atashindwa kumeet expectations za wananchi kwenye maisha mazuri na uchumi mzuri atakutana na hasira mbili, hasira za wananchi kunyimwa katiba yao wanayoitaka na hasira ya uchumi mbaya. Ilifikia hatua hii atakosa kitu cha kuwatuliza wananchi nacho!. kutegemea economic reform ukaachana na political reform, unakuwa unakuwa unacheza kamari, maana huo uchumi ukibuma basi unakuwa huna kadi ya kisiasa ya kutuliza joto hapo ni hatari.
 
Mama kweli akizingua kwenye matakwa ya wananchi anaweza kuchukiwa mara mbili ya alivyochukiwa Magufuli.

Maana calculations anazozifanya Samia ni kudhani kuwa anaweza kuituliza nchi hii kwa kurekebisha makosa ya Magufuli na kujenga uchumi imara peke yake na kwamba suala la katiba mpya linaweza kusubiri tu.

Kwenye kurekebisha makosa ya Magufuli yuko sahihi, kwenye kujenga uchumi yuko sahihi ila kwemye ishu ya katiba mpya amelosea tena amekosea kwelikweli.
Tatizo ninaloliona ni kuwa

1. Anaweza kujikuta anafikia hatua serikali yake ni unpopular sana na sasa ili kudhibiti sauti za wananchi basi naye akajikuta anarudi kulekule kwenye kufanya mambo yaleyale ambayo wananchi waliyoyachukia sana kwenye utawala wa Magufuli ya ubabe, ukatili, uongo mkubwa, propaganda kubwa, kununua wanasiasa kwa kuwahonga pesa na vyeo ili wamuunge mkono, na kuzidisha uonevu ili kunyamazisha sauti za wananchi wanaotaka mabadiliko nchini. Sasa akianza kufanya hayo atachukiwa mara kumi na kwa kuwa yeye siyo Bandidu kihulka kumfikia Magufuli, hatoweza kudhibiti hiyo hali, kimsingi anaweza kusababisha machafuko nchini.

2. Uchumi ni suala endelevu, halina mwisho wa ujenzi wake, Iwapo Atashindwa kumeet expectations za wananchi kwenye maisha mazuri na uchumi mzuri atakutana na hasira mbili, hasira za wananchi kunyimwa katiba yao wanayoitaka na hasira ya uchumi mbaya. Ilifikia hatua hii atakosa kitu cha kuwatuliza wananchi nacho!. kutegemea economic reform ukaachana na political reform, unakuwa unakuwa unacheza kamari, maana huo uchumi ukibuma basi unakuwa huna kadi ya kisiasa ya kutuliza joto hapo ni hatari.
I feel like baadhi ya watu hawana shukrani na wana pupa sana

si heri hata hajakataa?
 
Mama kawatuliza hadi mmeanza mkosea adabu sio?
Hv mngeweza kumuambia Hayati maneno ya hivi?
Msisahau na yeye ana madaraka yaleyale
Acha ujinga, naona umejiunga JF majuzi tu. Wengine humu tulikuwa tunamkoma huyo kichaa kama kawaida toka asukumiziwe madaraka yanayomzidi kimo. Ni vile tu alikuwa anahatamia vyombo vya habari sawa na jogoo kuhatamia mayai...wapi na wapi!

Hakuwa na sifa, busara wala hekima na hungeweza kumtofautisha na mnyama wa porini asiyekuwa na habari na sheria, taratibu, kanuni wala ustaarabu kama binadamu. Usije ukaniambia na mama ana mpango wa kuzifuata nyayo zake mwandazake!

JPM anawazoom tu na kusema hiiiiiiiiiiii mmeanza kunikumbuka mapema hii 🙂
Thubutu! huko aliko bila shaka yoyote anajuta na kuteseka kwa kipigo anachokipata wakati sisi huku tunalala usingizi mwororo baada Corona kutukomboa na hila zake.
 
Acha ujinga, naona umejiunga JF majuzi tu. Wengine humu tulikuwa tunamkoma huyo kichaa kama kawaida toka asukumiziwe madaraka yanayomzidi kimo. Ni vile tu alikuwa anahatamia vyombo vya habari sawa na jogoo kuhatamia mayai...wapi na wapi!

Hakuwa na sifa, busara wala hekima na hungeweza kumtofautisha na mnyama wa porini asiyekuwa na habari na sheria, taratibu, kanuni wala ustaarabu kama binadamu. Usije ukaniambia na mama ana mpango wa kuzifuata nyayo zake mwandazake!
Usione tarehe ya kujiunga ukadhani tumekuja humu juzi

Anyways.. naona kama Mama anaharakishwa sana wakati ashaonyesha yuko tofauti
 
Rais Samia alikiri kwamba kasi ya ukuaji wa uchumi imedondoka kutoka 7% mpaka 4.7% kipindi ambacho JPM “alisimimamisha” matumizi ya Katiba huku akiomba apewe muda

Did it work? Nop. Sasa huyu Rais Samia anataka kutuambia nini? Anadhani issue ya kukuza uchumi ina deadline?

Huyu asiitwe tena Mama. Aitwe Rais Samia tu
 
Nobody had the balls kumdai Magu katiba leo ndo mmezipata sio?
 
Ni mpumbavu pekee anayeweza kimuomba Samia alete katiba mpya huku CCM na SAMIA wakijua fika Katiba inawabeba wao kuendelea kutawala.

Hamna kitu kina kuja kirahisi lazima ziwepo kafara,anzisheni maandamano yasiyo na kikomo watu wafe wengine waumizwe.kuimba kwa maneno hadi dunia inaisha hakuna katiba itakayoletwa
 
Heheh sasa mngepambana na mwenzenu mwenye nazo..mmezubaa hadi ameresti in peace
Point haikuwa issue ya kupewa Katiba mpya ama la, ni kuhoji tu logic eti kwamba Rais anahitaji kupewa muda zaidi na kususpend baadhi ya haki za raia ili tu apate muda wa kusimamisha (kuinua) uchumi.

It is a lame excuse na haina mantiki yoyote
 
Hayo ni ya watu wa upande mmoja, mimi nataka matokeo ya utekelezaji wa mkataba baina ya serikali na wananchi. Mkataba huo unataka wananchi walipe kodi, halafu serikali iwajengee miundo mbinu na huduma za jamii na isimamia sheria kama zilivyoandikwa vitabuni.

Serikali ikishindwa kutekeleza huo mkataba ndipo nitalalamika ila wakiutekeleza, au wakionyesha nia thabidi ya kuutekeleza, nitakuwa nao: uwongo sitaki!
 
Point haikuwa issue ya kupewa Katiba mpya ama la, ni kuhoji tu logic eti kwamba Rais anahitaji kupewa muda zaidi na kususpend baadhi ya haki za raia ili tu apate muda wa kusimamisha (kuinua) uchumi.

It is a lame excuse na haina mantiki yoyote
Three months vs 6 yrs
What is illogical?

its obvious isnt it
Muache tu unafki
 
Back
Top Bottom