mnaohitaji katiba mpya anzisheni chama na kwenye ilani yenu ya 2025 muweke hicho kipengele cha katiba mpya, mbona rahisi sana.
Hizi kelele za katiba mpya ni kelele za wanasiasa wajinga wanaotaka urahisi wa kuingia ikulu kwa huruma ya chama tawala CCM...Hakuna mahala duniani dola inapatikana kirahisi mjifunze hili vinginevyo kila siku mtakwama na kulialia..
Yule jamaa ametuongoza miaka 6 mpaka ametwaliwa na mwenye mamlaka yake, hakuna aliyesimama barabarani kuidai hiyo katiba mpya zaidi ya hawa "keyboard warrior"....na yule jamaa alikuwa analala kwa amani kabisa..
Narudia tena, dola haipatikani kirahisi, msitegemee huruma ya CCM ili eti mpate dola. Tumieni akili zenu zote, maarifa na nguvu kuitafuta dola sio huruma za mtawala na chama chake... Hata kuupata huu uhuru tulio nao leo kuna watu waliteseka, kufa, kuumizwa nk ndio mkoloni akaamua kutuacha huru..Leo mnataka dola huku mnakunywa kahawa na wengine wako busy kutwa kucha humu JF na mitandaoni...Kazeni matako mpate dola, mbadilishe katiba, mruhusu mikutano ya kisiasa, mruhusu ushoga live, muwaweke watu lockdown, nk....