Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Kwa hiyo tukiendelea kumtaka mama aheshimu Katiba naye atatuundia kikosi chake cha wasiojulikana.Dawa yao inachemka.
Atakae jaribu kumkwamisha rais tutashuka nae jumla jumla
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa hiyo tukiendelea kumtaka mama aheshimu Katiba naye atatuundia kikosi chake cha wasiojulikana.Dawa yao inachemka.
Atakae jaribu kumkwamisha rais tutashuka nae jumla jumla
Yamemfikisha wapi ?! Rais wa hovyo kuwahi kutokea TanganyikaNdio
ama Hayati aliwaonyeshaje?.
kwa unafki
Hii pressure mbona kwa Hayati mliufyata?.
Inawezekana kupitia matendo mabovu kipindi cha hayati ndo watu wameona kuna hitaji la haraka kupata katiba bora.kwasababu mabadiliko toka kwenye kibovu kwenda kwenye kizuri hayana mwisho.kwahiyo kama ukuliona hitaji jana haimaanishi hautaliona hitaji leo.Ata sasa hakuna anayempa rais wa sasa pressure bali watu wanatoa mawazo yao.Ur acting as if Mama katawala miaka 2
mbona kwa Hayati hamkumpa hii pressure?.
Wanafki sana nyie..
mmekaa bila hio Katiba miaka 6 leo fyuu fyuu
Muacheni Mama
Mngekua mnaitaka kweli mngekomaa na Hayati
Walioshuka na watu wako wapi sasa ?!Dawa yao inachemka.
Hatuyumbishwi na hatutetereshwi, Sisi wananchi tutaendelea kumuunga mkono Mheshimiwa rais ili tupate maendeleo aliyotuahidi.
Atakae jaribu kumkwamisha rais tutashuka nae jumla jumla
Huo uchuro wala hautatokea,ni dua la mwewe,maza hatazalusha sabaya wala makonda hakuna mtu atakayekamatwa hovyo wala kupigwaMama omba radhi watanzania kauri yako ya kusubiri kwanza kufufua uchumi ndiyo turuhusu marekebisho ya katiba na mikutano UA kisiasa hii umechemka.
1. Utachukiwa kuliko hata JPM
2. Utapoteza heshima ya kuitwa mama.
3. Utazalisha akina Sabaya na Makonda wengi kuliko JPM
4. Unaweza kuwa Rais wa mwisho kutoka Z'bar.
5. Mataia ya nje walioanza kukuunga mkono watakugeuka ndani ya muda mfupi.
6. Wanufaika wa utawala wa JPM wataungana na wapinzani kukushambulia.
7......
Nitaendelea nachaji simu kwanza.
Kama mnaitaka sana hio Katiba shindeni uchaguzi muitengenezeYamemfikisha wapi ?! Rais wa hovyo kuwahi kutokea Tanganyika
Mbona kipundi cha jpm mlikua hamdai katiba , mwacheni mama achape kazi katiba tulionayo iko vizuri tuRais Samia alikiri kwamba kasi ya ukuaji wa uchumi imedondoka kutoka 7% mpaka 4.7% kipindi ambacho JPM “alisimimamisha” matumizi ya Katiba huku akiomba apewe muda
Did it work? Nop. Sasa huyu Rais Samia anataka kutuambia nini? Anadhani issue ya kukuza uchumi ina deadline?
Huyu asiitwe tena Mama. Aitwe Rais Samia tu
Utashinda chaguzi zinazoporwa kwa mitutu ?!. Wewe hata shule ulienda kweli ?!Kama mnaitaka sana hio Katiba shindeni uchaguzi muitengeneze
au anzeni japo kwa kuweka ukomo wa Mwenyekiti kwanza huko Chadema
Hili bandiko liwekewe pin, haya uliyosema yatatokea yote. Mwaka 2025 mama atakuwa unpopular at both sides ( wapinzani na CCM) kiasi kwamba atakuwa hana wa kumuunga mkono zaidi ya wazanzibar wenzake. Maana watu wengi waliokuwa wanamuunga mkono sasaiv walikuwa ni wapinzani, na sasa ameshaanza kuwapotezaMama kweli akizingua kwenye matakwa ya wananchi anaweza kuchukiwa mara mbili ya alivyochukiwa Magufuli.
Maana calculations anazozifanya Samia ni kudhani kuwa anaweza kuituliza nchi hii kwa kurekebisha makosa ya Magufuli na kujenga uchumi imara peke yake na kwamba suala la katiba mpya linaweza kusubiri tu.
Kwenye kurekebisha makosa ya Magufuli yuko sahihi, kwenye kujenga uchumi yuko sahihi ila kwenye ishu ya katiba mpya amekosea tena amekosea kwelikweli.
Tatizo ninaloliona ni kuwa
1. Anaweza kujikuta anafikia hatua serikali yake ni unpopular sana na sasa ili kudhibiti sauti za wananchi basi naye akajikuta anarudi kulekule kwenye kufanya mambo yaleyale ambayo wananchi waliyoyachukia sana kwenye utawala wa Magufuli ya ubabe, ukatili, uongo mkubwa, propaganda kubwa, kununua wanasiasa kwa kuwahonga pesa na vyeo ili wamuunge mkono, na kuzidisha uonevu ili kunyamazisha sauti za wananchi wanaotaka mabadiliko nchini. Sasa akianza kufanya hayo atachukiwa mara kumi na kwa kuwa yeye siyo Bandidu kihulka kumfikia Magufuli, hatoweza kudhibiti hiyo hali, kimsingi anaweza kusababisha machafuko nchini.
2. Uchumi ni suala endelevu, halina mwisho wa ujenzi wake, Iwapo Atashindwa kumeet expectations za wananchi kwenye maisha mazuri na uchumi mzuri atakutana na hasira mbili, hasira za wananchi kunyimwa katiba yao wanayoitaka na hasira ya uchumi mbaya. Ilifikia hatua hii atakosa kitu cha kuwatuliza wananchi nacho!. kutegemea economic reform ukaachana na political reform, unakuwa unakuwa unacheza kamari, maana huo uchumi ukibuma basi unakuwa huna kadi ya kisiasa ya kutuliza joto hapo ni hatari.
Naunga mkono hoja kabisaSio utashi wa mama.
Ni msimamo wa CCM, chama kilichomuweka pale.
Hapa kuwa na uchaguzi ulikuwa ni uchafuziUtashinda chaguzi zinazoporwa kwa mitutu ?!. Wewe hata shule ulienda kweli ?!
Tumemtukana sana Magufuli humu jamii forum mpaka akamkamata Maxence Melo atoe true id za watu humu. Tumemtukana Magu na hajafanya chochoteMama kawatuliza hadi mmeanza mkosea adabu sio?
Hv mngeweza kumuambia Hayati maneno ya hivi?.
Msisahau na yeye ana madaraka yaleyale
Shindeni uchaguzi mtengeneze hio katibaTumemtukana sana Magufuli humu jamii forum mpaka akamkamata Maxence Melo atoe true id za watu humu. Tumemtukana Magu na hajafanya chochote
Kipindi cha Jpm kuna watu tulisema kua kama kweli Jpm ni kiongozi mzuri basi ajitahidi atengeneze mifumo thabiti ya uendeshaji nchi ili ata siku akiondoka nchi iende kwenye misingi aliyoiweka,sasa kwasababu hakufanya hivyo ndo maana umetaja baadhi ya mambo ya ovyo yaliyofanyika kipindi chake sasa leo hayupo kwahiyo kuna uwezekano pia hiyu aliyepo akafanya aidha mazur au mabaya kabisa kwa sababu nchi bado haina mifumo na miongozo thabiti.Sasa tunakua ni nchi ya leo hivi kesho vile kutegemea tu rais kaamkaje.kwahiyo kama kweli ana nia njema na hili taifa basi ni vyema akaweka mambo mazuri kwa ajili ya nchi ili ata atakapoondoka nchi iendelee vyema.Na muda mzuri wakufanya jambo ni kipindi watu wanalizungumzia kwasababu hakuna aijuaye kesho.Nafikiri unapaswa ujiulize swali moja, hivi hill neno mama mwanzilishi ni nani mpaka akaitwa mama? Kwa nini umama wake ushuke hadhi? Unafikiri wewe na wenzako mutampa thamani kwa sababu ya kupewa katiba mpya?
Kwa hiyo mlitaka mama baada ya JPM kufa aanze mchakato wa katiba mpya, are you sure kwa akili yenu mungemuona wa maana? Leo tunashuhudia vitu ambavyo vikitokea ambavyo havikutokea ndani ya miaka sita iliyopita, wafungwa wanatoka magerezani, vyombo vya habari vinaanza kuwa huru, wafanyabisha wanaanza kutabasamu, safari ya matumaini imeanza, lakini nyinyi bado mnatafuta namna ya kumkera na kumtafuta kama huyu mwanamke anaweza kuwa mkali?
Hata Yohana alipokuwa gerezani aliuliza maswali kama yenu, Yesu ndiye au asubiriwe mwingine, Yesu akamwmbia, sasa vipofu wanaona na viwete wameanza kutembea heri mwenye kuamini. Yohana pia alikuwa na haraka ya kutoka gerezani. Kumbuka watanzania wengi tupi kwenye hili gerezani la katiba, na katika ni jambo nyeti sana.
Iweni na subira kama mama alivyosema, kwani tupo wengi pia tuliopata tumaini kwa Huyu mama na hatuko tayari kuona akiyumbishwa, kwa sabaabu tumeiona nia njema aliyonayo. Narudia iweni na subira, iweni na subira, mama ameinjika chungu kiko jikoni ni dalili kwamba kila mtu atakula lakini unataka kutumbukiza mkono kushinikiza chakula kupakuliwe kabla hakijaiva. Tutakuunguza mdomo tena mtaunguzwa midomo tena sana ili hata chakula kikipoa kwenu kibaki kuwa chamoto ili musiwe na hamu hata ya kula, endeleeni kuwa na tabia kama ya watoto waliokataliwa tangu matumboni mwa mama zao.
Wewe ndo uliufyata. Maana tumemtukana humu miaka yote. Usitutie kwenye kundi lako la wajinga na waogaNdio
ama Hayati aliwaonyeshaje?.
kwa unafki
Hii pressure mbona kwa Hayati mliufyata?.
Ukikua utaelewa tu haya mambo.katiba tulionayo iko vizuri tu..
Mkuu mbona unaongea nadharia sana?Hili bandiko liwekewe pin, haya uliyosema yatatokea yote. Mwaka 2025 mama atakuwa unpopular at both sides ( wapinzani na CCM) kiasi kwamba atakuwa hana wa kumuunga mkono zaidi ya wazanzibar wenzake. Maana watu wengi waliokuwa wanamuunga mkono sasaiv walikuwa ni wapinzani, na sasa ameshaanza kuwapoteza
Mambo mengine yamekuzidi uwezo wa kufikiri.uwezo wako kuvaa dera .kwanza nenda kabadili nguo ya ndani uku sio sehemu yako.Pumbavu sana hawa ndezi.
Wanataka twende nao hivi hivi kindezi ndezi.
Yaani jambo limekubaliwa, mnaambiwa Nipeni muda nishughulikie wao wameng'ang'ania tu ujinga ujinga.