Itapendeza zaidi kuomba radhi, kulinda hadhi ya kuendelea kuitwa mama

Sasa huyo Magufuli aliyeua na kutesa watu yupo wapi? Hata huyu mama akiua wapinzani kwamba mwisho wake ni nini? Tatizo watu wengi wanadhani suala la katiba mpya ni la wapinzani peke yao. Hebu nikuulize swali, Tume ya Jaji Warioba ilipozunguka nchi nzima kupata maoni ya watu nchi nzima walikuwa wanazungumza na wapinzani peke yao? Katiba mpya ni maoni ya wapinzani? Mna matatizo sana
 
Amina
 
Mkuu, unaonekana ni jasiri sana, omba viongozi wako muandamane mkiwa na madai yenu ya msingi sio kelele za kwenye keyboard tu hapa.

Yaani nyie majamaa huwa mnahisi watanzania million 60 wanawakilishwa na nyie watu 50 kwenye mitandao ya kijamii. Tena mnafikia mahali mnahisi kila mnachotaka mtimiziwe as if mko pekeenu. Ndio maana nasema hayati alkuwa akiwapiga spana mpaka mkatulia tuliii.

Lastly, kuhusu kufa, ni nani amekuambia hayati amekufa sababu ya kuwapiga spana nyie msiojua mnataka nini?
Kiufupi TZ ya mitandaoni sio ya huko mtaani acheni kujifariji..
 
Kama nyie"wengi" ambao hamkubaliani na "kelele za watu wachache wa kwenye key board" mnajiamini, kwanini msilete katiba mpya na tume huru ya uchaguzi twende tukapige kura. Kwanini mnaogopa katiba mpya na tume huru wakati nyie mpo "wengi". Mwenye akili angeweza jiuliza hilo.
Halaf kwanini uwe na mawazo mtu akikupinga inabidi "apigwe" au "auawe"? Huyo Magu aliyepiga watu risasi na kuwapoteza watu ili alinde madaraka yake yuko wapi?
 
Unajichosha bure. CCM ni sikio la kufa. Tunasubiri tamko la Kamanda Siro. Tuendelee kupayuka: KATIBA MPYA!!!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…