Itashangaa "LATRA isipoifungia kampuni ya mabasi ya Shabiby.

Itashangaa "LATRA isipoifungia kampuni ya mabasi ya Shabiby.

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Kila siku kampuni hii, inazalisha vifo na walemavu. Nitashangaa kama LATRA. haitawatendea haki Watanganyika.

Suala la usalama na usimamizi wa kampuni hii ya mabasi limekuwa ni tatizo kubwa kwa muda mrefu. Ni zuri kwamba serikali imekuwa ikiangalia hali hii, lakini inaonekana kwamba bado hakuna hatua madhubuti zilizochukuliwa kutatua matatizo haya.

LATRA, ambayo ni chombo cha usimamizi wa usalama wa uchukuzi, inapaswa kushiriki kikamilifu katika kuchunguza na kutatua changamoto hizi. Vilevile, serikali inapaswa kuchukua hatua kali dhidi ya kampuni hii ya Shabiby ikiwa imeshindwa kuirekebisha na kuhakikisha usalama wa abiria.

Ni muhimu pia kwamba umma wetu unapewa habari kamili kuhusu matatizo haya na hatua zinazochukuliwa ili kuhakikisha usalama wa usafiri wa umma. Ukiwa na maoni yako kuhusu suala hili, nina furaha ya kujadili zaidi.
 

Attachments

  • VID-20240807-WA0021.mp4
    5.2 MB
Kila siku kampuni hii,inazalisha vifo na walemavu. Nitashangaa kama LATRAhaitawatendea haki Watanganyika.
Ndio kampuni inayopewa tenda bila ushindani wowote kubeba WABUNGE na kamati za bunge kwa zaisi ya miaka 20.
Yani Shabibi anakopa benki na ana uhakika wa kurudisha mkopo maana kila bunge yeye ndio anabebq kamatizote kuzururisha nchi nzima.

#Niko hapa, hata kukemewa hakemewi.
 
Ajali za barabarani zinachukua sana roho za Watanzania halafu wala hatustuki zaidi ya kuleta siasa tu.

Hawa madereva wengi ni wajinga sana huku barabarani na askari wetu wamejikita kukusanya posho tu na kudeal na michongo barabarani huko.
 
Pole sana kwa waliopoteza wapendwa wao.

Lakini, bila shaka makosa ya barabarani huadhibiwa kwa kufuata sheria za barabarani bila kuhusisha hisia za hasira, majonzi au chuki.

Unajua, Shabiby anaweza pata ajali kwa makosa ya watumiaji wengine wa barabara au changamoto za ubora wa barabara, sisi tukabaki kumlaumu tu kwa kuwa "huwa anapata ajali".

So, tuache sheria zifuate mkondo wake
 
Kila nikienda Dodoma huwa sina bus lingine la kupanda zaidi ya hili... huu nahisi nimeskia ajali mbili za bus hili but all in all ajali huwa zinatokea mkuu.
Li barabara lenyewe libovu hilo la dodoma, lina mabonde mabonde kama yote. Bado pia ina madereva vichaa na wanaokimbia sana kuliko barabara yeyote nchini kwa sasa. Shabiby unaweza kuta hana hata makosa kwenye ajali zote hizo.
 
Li barabara lenyewe libovu hilo la dodoma, lina mabonde mabonde kama yote. Bado pia ina madereva vichaa na wanaokimbia sana kuliko barabara yeyote nchini kwa sasa. Shabiby unaweza kuta hana hata makosa kwenye ajali zote hizo.
Sure, ukitaka uende kwa mwendo wa kawaida upande zile za VIP au za kawaida ila ukutane na dereva wa kubeba stafu.
 
Yaani naona hio ajali ilivyotokea. Nyingi huwa zinatokea au watu kukoswakoswa. Nishashuhudia mbili zikitokea mbele yangu.
Gari ya tatu mbele yangu inajiandaa kukata kulia, wakati mnaisubiri anatokea mpuuzi nyuma na haraka zake anakupita anaenda kuikuta gari inayokata imeshaingia kulia hivyo anaitandika ubavuni.
 
Back
Top Bottom