Itatokea nini tukiamua tusilipe deni la Taifa Tsh Trilioni 100?

Itatokea nini tukiamua tusilipe deni la Taifa Tsh Trilioni 100?

Mwigulu Nchemba ameshawaambia mambo ya uchumi muachieni yeye, na nyie mjikite kujadili mambo ya waganga wa kienyeji
82072BD6-ECC6-4154-ACFA-C1B85D2ED3B0.jpeg
 
Deni la taifa halilipiki, na hii ni kwa nchi yoyote yenye madeni. Deni litaendelea kukua kwa sababu ya riba. Kuna madeni mengine ni miaka 50 iliyopita na mengine tunakopa sasa tutalipa marejesho kwa miaka 50 ijayo. Na hakuna nchi yoyote yenye mpango wa kumaliza/kupunguza deni. Ni mwendo wa kukopa na kulipa hadi Yesu atakaporudi.
 
Ulishawai ona tembo, Simba na twiga wakipanda ndege ww? Lazima hao wanyama tuliwaweka rehani au tunaweza ambiwa ushoga uwe ndo habari ya town
Nasemaje, kama Simba na Tembo watapandishwa ndege potelea mbali, wacha waende wote, watazaliana wengine, ila hakuna tena kulipa hili deni, limeshakuwa toxic, riba inazidi deni halisi sasa...
 
Kwanza kabisa deni la Taifa ni tofauti na deni la kampuni kwa sababu Taifa huwezi kulipeleka mahakamani yaani hakuna mahakama ya madeni ya Nchi

Kwa hiyo utabembelezwa tu kulipa na ukishindwa unapewa zingine

Sasa kwa nchi za kimasikini na sio Africa pekee bali nchi nyingi wanaokopa wanagawana nusu na nusu inaingizwa kwenye miradi na huko inakutana na majizi mengine

Ndio maana mtakaa kila siku kukatikiwa Umeme wakati wajanja walishaomba hela za mitambo ya umeme wakala

Nchi zetu hazina wazalendo maana hata mtoto wa kiongozi anafundishwa kuiba
 
Mh.SAMIA na MWIGULU si mpo humu njoeni mjibu hili swali
Sasa Wewe econometrician,unashindwa kutoa jibu kwa swali jepesi hilo, Wakati wewe ndiyo mbobevu wa data analysis za ecomics? Tumia linear algebra, linear regression testing and analysis kuelezea namna gani foreign debt inavyoweza kuamsha au kuua uchumi wa Nchi yako [emoji1787][emoji1787] au?
 
Back
Top Bottom