Itatokea nini tukiamua tusilipe deni la Taifa Tsh Trilioni 100?

Hivi ikatokea tukaamua tu tuwaingize mjini haya mabeberu yanatukopesha mamikopo kwa fujo kama ugomvi na tusiwalipe tu, watatufanya nini kwani? Ukiacha kukamata ndege, watafanya nini?
Sasa utafanyaje biashara na dunia mkuu. Maana leo hii ukitaka kulipia mzigo china tunaomba TT bank kuu kupitia bank yako. na zote zinaombwa federal bank pale New York then ndio mzigo unaenda kwa wenyewe. Sasa bila hiyo unafanyaje jombaa.
 
Nani kakwambia hakuna mahakama ya madeni ya nchi

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Misri miaka mingi iliyopita walizingua kulipa madeni waliyodaiwa na UK na France. France na UK wakaenda wakachukua mfereji wa Suez na wakamuweka waziri wao wa fedha kuhakikisha deni linalipwa. Sijui sasa wanaweza fanya nini.
Nahisi hapa kwetu wataweka waziri wao wa fedha kwenye bwawa la Nyerere, umeme unit 1 tutauziwa buku, hadi deni liishe...
 
Sasa utafanyaje biashara na dunia mkuu. Maana leo hii ukitaka kulipia mzigo china tunaomba TT bank kuu kupitia bank yako. na zote zinaombwa federal bank pale New York then ndio mzigo unaenda kwa wenyewe. Sasa bila hiyo unafanyaje jombaa.
Muulize Salaah anavyowaagizia wafanyabiashara mizigo duniani kote, na hakuna hata 100 inayopitia benki kuu
 
1: Kampuni ya TANESCO ipo chini ya JAPAN nini nini uko...
2: Bandari ipo chini ya ARABIC/ AMERICAN nini nini uko...
3: Gas asiliia chini ya ...
4: Serengeti NP ......
huo ndio mfano wa ulipaji mikopo
 
Hivi ikatokea tukaamua tu tuwaingize mjini haya mabeberu yanatukopesha mamikopo kwa fujo kama ugomvi na tusiwalipe tu, watatufanya nini kwani? Ukiacha kukamata ndege, watafanya nini?
Dawa ya deni ni kulipa
Nafikiri ungeshauri pamoja na mengine, tujumuishe miradi mikubwa ya kukuza ajira na kuongeza Kodi ili deni lijilipe lenyewe (lisitegemee makusanyo mengine ya ndani)
Mf; kiwanda kama cha matairi, viwanda vya madawa nk
 
Hivi mtu unakopa trillion 2 kwa ajili ya chanjo feki zilizo expire za Corona.., hivi hilo deni hata lina tija kwanza? Maana yake hatukuwa na haja ya kukopa in the 1st place
 
Muulize Salaah anavyowaagizia wafanyabiashara mizigo duniani kote, na hakuna hata 100 inayopitia benki kuu
Mzee HIV wewe unafikiria Salah ndio agent pekee bongo nini. Au unafikiria kabla ya Salah watu walikuwa wanafanyaje. Mtu akishakuzid kikazi njoo na njia mbadala ya kumkabili sio umbea mzee. Watu waliokuwa wanaenda china tangu miaka ya 1999 wanajua umuhim wa hawa waarabu. Wana makando yao ndio Lakin hakuna mfanyabiashara asiyejua umuhim wa hawa jamaa sokon.
 
Sawa, turudi kwenye mada...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…