Itengenezwe application tupige kura kwa Simu zetu tusipotezeane muda

Itengenezwe application tupige kura kwa Simu zetu tusipotezeane muda

Hehe watashinda kivipi tena, wakati hii ndo itakua mtelezo kwa CCM .....muulizeni Odinga anajua purukushani za kura za kielektronic
Bc kwa namna yoyote ile lazima ccm ishinde
 
Hivi wafrika ni lini tutadhamini muda wetu

Kwenye foleni saa kadhaa eti nasubiri nimpigie diwani kura.

Twendeni na technology inavyotaka watu wapige kura wakiwa nyumbani ofisini

Serikali inapoteza fedha nyingi eti kuweka mawakala waandikishe watu wachague wenyeviti!!!!

Hii SI sawa zaidi ya watanzania 30 mls wanamiliki simu za mkononi tuzitumie kuchaguana.
Ccm hatutaki hayo matekinolojia yenu..

Kama hutaki kwenda kujiandikisha acha usipige kura tutashinda tu uende usiende kujiandikisha tutashinda tu.
 
CHADEMA HAWATAKI VIJANA WAJIANDIKISHE, JE WANAWAOGOPA KWENYE UCHAGUZI?

Sauti za Chadema sasa zinapaza malalamiko yasiyo na mashiko, wakidai kwamba Tume ya Uchaguzi (NEC) inaandikisha wanafunzi kwa lengo la kuwaandaa kupigia kura CCM. Ukweli ni kwamba, kila kijana mwenye miaka 18 ana haki ya kikatiba kujiandikisha na kupiga kura.

Hii siyo mbinu ya kisiasa bali ni utekelezaji wa sheria, kwani vijana waliozaliwa mwaka 2006, wakiwemo wa umri wa miaka 17 mwaka huu, watafikisha miaka 18 ifikapo mwakani. Je, Chadema wanataka kuwanyima haki zao kikatiba?

Chadema wanatakiwa kuelewa kuwa kila aliyeandikishwa ameonesha kitambulisho kinachoonesha umri wake halali. Kuibua tuhuma za "kuandikisha watoto" bila kutoa ushahidi wa vitambulisho ni mbinu ya kisiasa ya kutengeneza mazingira ya kujiondoa mapema au kutafuta kisingizio endapo watashindwa tena mwakani. Tumeona mbinu kama hizi mara kadhaa—wakishindwa, hukimbilia kusema "tulibambikiwa."

Nani anaweza kuwazuia vijana wenye ari na shauku ya kushiriki kikamilifu katika uchaguzi? Hili si swali la wafuasi wa CCM bali ni ishara ya hofu ndani ya Chadema, wakijua kuwa kizazi cha sasa kinatambua haki zake na hakitadanganywa kirahisi. Wanapojaribu kupinga ushiriki wa vijana, wanaonesha wazi kuwa hawataki sauti za kizazi kipya zisikike.

Kwa kifupi, malalamiko ya Chadema si hoja ya msingi bali mbinu ya kuwatisha vijana na kuwapotezea imani katika mchakato wa uchaguzi. Uchaguzi si mchezo wa kuigiza bali ni nafasi ya kila raia, awe kijana au mzee, kuamua hatma ya taifa kupitia sanduku la kura.

Kama Chadema wana hofu ya kushindwa, basi wanapaswa kujipanga na kuja na sera bora badala ya kutengeneza visingizio visivyo na msingi.
 
Duuuh!,...kupiga kura nako kwataka moyo sana,...
 
Mie siwezi kupot
Ajiraumu sana Mimi kupiga kura yangu 2010 Kisha kikwete akaipora nimeshaapa Kwa mbingu na ardhi sitokaa nipoteze muda wangu.sasa Hivi na utaratibu Huwa naenda kabisa niliko zaliwa najiandikisha huko ambapo Nina uhakika 100% sitaenda kupiga kura pia kuondoa buguza Kwa michawa Huwa nawaambia tu sijajiandikishia huku rafiki yangu nitaenda kijijn kupiga kura .mimi siwezi kupoteza Tena muda eti napiga kura no no no
 
Kwa style hii lazima Chadema washinde mana vijana wengi wana access ya internet na simu ila hao hao hawawezi Kwenda kupanga foleni kupiga kura, Mm mwnyw tangu nmejiandikisha sijawahi na sitokaa nipige kura.
True
 
Bado tunajikongoja kutoka kwenye ujima,,zama za mawe za kati na kunya porini
 
Back
Top Bottom