It's never too late maadam pumzi ya Mungu ingali ndani yako

It's never too late maadam pumzi ya Mungu ingali ndani yako

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Hata kama ulishajaribu mara nyingi bila mafanikio usikate tamaa! Thubutu kuota tena!

Wanandoa wawili walifanya jitihada kumpata mtoto kwa zaidi ya miaka ya ishirini bila mafanikio. Lakini mwaka wa ishirini na nane wa ndoa yao walifanikiwa kumpata mtoto wao wa kwanza. Kama wangekata tamaa mwaka wa ishirini na tano wa ndoa yao huu ushuhuda usingekuwepo.

Mwanamke mmoja alipofikisha miaka arobaini na tano bila mume, hakukata tamaa ya kuolewa. Kama bahati vile, akiwa na miaka 46 aliolewa na mwanaume anayelingana naye kiumri. Na wote hawakuwa wamewahi kuwa na ndoa wala watoto.

Wakiwa na miaka 48, ndipo mtoto wao wa kwanza alipozaliwa. Wakati ushuhuda huu unatoka, kijana wao wa kwanza alikuwa na miaka 21 na wao wakiwa na miaka 69.

Kanali Sanders alitajirika baada ya kuwa ameshastaafu kazi ya kuajiriwa. Aliianzisha KFC akiwa kwenye umri wa miaka sitini. Ni hiyo biashara ndiyo iliyomtajirisha.

Sikumbuki jina, lakini habari zake zimeandikwa Kwenye moja ya vitabu vya Robert Schuller. Ni za mwanaume mmoja ambaye yeye aligundua kuwa ana kipaji cha kukimbia akiwa na miaka sabini. Aliamua kuanza kufanya mazoezi na kujitosa kwenye mashindano yaliyomfanya aibuke kidedea.

Inawezekana kuna mambo ulitamani uyafanikishe lakini mpaka sasa bado. Kama ni mambo ya muhimu, usiyakatie tamaa. Haijalishi umeshasubiria kwa muda gani, maadam ungali u hai na hujapanga kufa leo, jihimize tena na usonge mbele.

Fursa ulizozimisi ni darasa la kukusaidia kutengeneza fursa zingine.

Haujachelewa maadam hujapanga kuchelewa. Kwa kuwa ungali hai, ukiamua, lolote laweza kutokea litakalobadilisha Historia.

Unaweza kuanza tena kwa sababu it is never too late kwa aliye hai!
 
umeandika kitu cha maana sana
kuna watu wanakatisha wenzao tamaa
mtu akifika 35 tu haoni muelekeo anaanza kuwa mlevi
Nafikiri watu wamekariri!
Mifano waliyo nayo ni ya babu, bibi, mjomba, na ndugu zao wengine wa karibu. Wanafikiri namna pekee ya maisha ni vile walivyoishi watu wa jamii zao.

Watu kama hao wanahitaji "exposure". Itasaidia kubadilisha mitazamo.

Ni kama mfano aliowahi kuutoa Rais Kikwete, kwamba alipokuwa Primary, aliamini watu wote ni Wakwere. Ni baada ya kwenda Sekondari ndiyo aligundua kuwa kuna makabila mengine zaidi ya Wakwere.

Watu wamejijengea mitazamo kulingana na mazingira yao lakini mara nyingi wanaweza wakawa hawapo sahihi.
 
Back
Top Bottom