Itungwe sheria kuzuia uchomaji wa Taka ngumu mitaani

Stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Posts
40,051
Reaction score
51,217
Naishauri serikali kuu na zile za mitaa kutunga sheria kuzuia uchomaji wa taka ngumu mitaani.

Unakuta baadhi ya mitaa kuna mashindano ya kuchoma taka ngumu.

Unakuta taka zina nailoni mbali mbali na materials nyingine ambazo zinaweze kuwa na madhara ya kiafya kwa wakazi wa maeneo hayo.
 
Itungwe mara ngapi?Nenda kwa Mtendaji wa mtaa/kata/Afisa Afya wa kata akupe shreia ya afya na mazingira,makatazo,maelezo na adhabu zake.Za siku nyingi tu katika serikali za mitaa 1982 na serikali kuu pia.
Nimeipitia hiyo sheria nilichoshauri hakipo.
 
Siku nyingine ukikuta wanafanya hayo mashindano ya uchomaji takataka/taka ngumu au hata nyepesi mitaani bila utaratibu hitajika uwaeleze kwamba ni kosa kisheria.Wasipofundishika una haki ya kuwashitaki.Ajabu sana na inaonesha sheria za mamlaka za miji kuhusu afya,utunzaji na usafi wa mazingira hawajui.
 
Itungwe mara ngapi?Nenda kwa Mtendaji wa mtaa/kata/Afisa Afya wa kata akupe shreia ya afya na mazingira,makatazo,maelezo na adhabu zake.Za siku nyingi tu katika serikali za mitaa 1982 na serikali kuu pia.
Basi kuna uzembe kwenye kufuatilia utekelezaji. Kuna watu na uchomaji moto ni kama Masai na Sime
 
Basi kuna uzembe kwenye kufuatilia utekelezaji. Kuna watu na moto ni kama Masai na Sime
Wasimamizi wa sheria hizo nyakati zingine ni changamoto aidha kwa kutozijua au uzembe wa kutozisimamia.Uchomaji vitu/takataka hovyo,sauti kubwa za muziki au vipaza sauti/PA mitaani bila vibali/maelekezo sahihi ni changamoto kubwa.
NB:Wakizisimamia hizo sheria vizuri msiwaue kama yule Mtendaji wa Ludewa aliyeuawa na mchoma mkaa/mharibu miti na mazingira(suala bado lipo mikononi mwa sheria).
 
Basi kuna uzembe kwenye kufuatilia utekelezaji. Kuna watu na uchomaji moto ni kama Masai na Sime
Kilichomo kwenye sheria ni kuhusu utaratibu wa kutoa vibali vya kuchoma taka kwa makampuni binafsi na taasisi.

Nachoshauri hapa hakipo kwenye sheria.
 
Tatizo sio wachomaji tatizo ni magari ya taka ya manispaa je yanapita kwa wakati huko mitaani? Hii nchi imeharibika kila kona.
 
Mambo mengi mtaani yanayofanyika kisheria ni makosa
Kama hayo ya kuchoma takataka, kutupa takataka,
Kupiga muziki
Kuuza mamantilie
Kuuza vitafunio, genge, duka au biashara yoyote bila kibali cha wataalam husika na serikali.

Tukisema Sheria ifuatwe kama ilivyo mambo yatakuwa magumu hapa.
 
Sheria pia ni tatizo unamwajibisha mtu kwa kutumia sheria ipi wakati haipo.

Itungwe kwanza ili iwe rahisi kuwawajibisha wanaoikiuka.
 
Mambo mengi mtaani yanayofanyika kisheria ni makosa
Kama hayo ya kuchoma takataka, kutupa takataka,
Kupiga muziki
Kuuza mamantilie
Kuuza vitafunio, genge, duka au biashara yoyote bila kibali cha wataalam husika na serikali.

Tukisema Sheria ifuatwe kama ilivyo mambo yatakuwa magumu hapa.
Hoja yangu ni kuchoma taka hovyo mitaani.

Sheria haipo iwekwe kwanza.
 
Nimeipitia hiyo sheria nilichoshauri hakipo.
Ni lazima kuna sheria inayokataza. Sheria zetu nyingi tulirithi kwa wakoloni na walikuwa wame-cover karibu kila kitu kwenye maisha ya kila siku.
 
Naishauri serikali kuu na zile za mitaa kutunga sheria kuzuia uchomaji wa taka ngumu mitaani.

Unakuta baadhi ya mitaa kuna mashindano ya kuchoma taka ngumu.

Unakuta taka zina nailoni mbali mbali na materials nyingine ambazo zinaweze kuwa na madhara ya kiafya kwa wakazi wa maeneo hayo.
Sheria ipo.

Taka kuchomwa ni KIASHIRIA cha UMASIKINI cha ENEO lako. Wanafanya wanachoweza eneo libaki safi.

Watu hawalipi USHURU wa TAKA.

TAKA haziwezi kujipeleka DAMPO.
 
Mambo mengi mtaani yanayofanyika kisheria ni makosa
Kama hayo ya kuchoma takataka, kutupa takataka,
Kupiga muziki
Kuuza mamantilie
Kuuza vitafunio, genge, duka au biashara yoyote bila kibali cha wataalam husika na serikali.

Tukisema Sheria ifuatwe kama ilivyo mambo yatakuwa magumu hapa.
Ila hiyo ya kuchoma taka ingekaziwa!
Kwengine huku taka marafuku kuchoma,hata kuanika nguo kwenye kamba ulizofua mbele ya nyumba yako marufuku Anika nyuma huko
Kuna sheria ndogo ndogo zinafuatiliwa

Ova
 
Hoja yangu ni kuchoma taka hovyo mitaani.

Sheria haipo iwekwe kwanza.
Sheria ipo na inakataza, pengine wewe mpaka uone neno ''kuchoma taka mitaani na majumbani''? Kna sheria tena nyingi tu eg illegal waste disposal, environmental pollution, au public nuisance under municipal by-laws and environmental regulations.
 
Sheria ipo.

Taka kuchomwa ni KIASHIRIA cha UMASIKINI cha ENEO lako. Wanafanya wanachoweza eneo libaki safi.

Watu hawalipi USHURU wa TAKA.

TAKA haziwezi kujipeleka DAMPO.
Watu wanalipa taka
Sema ukusanyi wa taka
Umekuwa mmbovu
Watu huko wanalalamika
Miezi 3 gari la taka halijapita

Ova
 
Back
Top Bottom