Sheria zipoSheria pia ni tatizo unamwajibisha mtu kwa kutumia sheria ipi wakati haipo.
Itungwe kwanza ili iwe rahisi kuwawajibisha wanaoikiuka.
Sheria zipoSheria pia ni tatizo unamwajibisha mtu kwa kutumia sheria ipi wakati haipo.
Itungwe kwanza ili iwe rahisi kuwawajibisha wanaoikiuka.
Wakija kukusanya pesa ya taka kwako, kabla hawahazoa taka.Watu wanalipa taka
Sema ukusanyi wa taka
Umekuwa mmbovu
Watu huko wanalalamika
Miezi 3 gari la taka halijapita
Ova
Ila hiyo ya kuchoma taka ingekaziwa!
Kwengine huku taka marafuku kuchoma,hata kuanika nguo kwenye kamba ulizofua mbele ya nyumba yako marufuku Anika nyuma huko
Kuna sheria ndogo ndogo zinafuatiliwa
Ova
Hoja yangu ni kuchoma taka hovyo mitaani.
Sheria haipo iwekwe kwanza.
Sipo huko!Wakija kukusanya pesa ya taka kwako, kabla hawahazoa taka.
USIWAPE
Unaleta maelezo mengi.Sipo huko!
Kwanini wakusanyaji taka hawafati ratiba yao,waliyoweka,au ndiyo jiji wanawazingua kwenye kuwalipa fedha wakandarasi wa taka kwa wakati
Kingine kwanini lile dampo wasiliboreshe liweze kuingilika kwa urahisi
Ova
Mkuu kuna wengine wanafanya maksudi kabisa.Wasimamizi wa sheria hizo nyakati zingine ni changamoto aidha kwa kutozijua au uzembe wa kutozisimamia.Uchomaji vitu/takataka hovyo,sauti kubwa za muziki au vipaza sauti/PA mitaani bila vibali/maelekezo sahihi ni changamoto kubwa.
NB:Wakizisimamia hizo sheria vizuri msiwaue kama yule Mtendaji wa Ludewa aliyeuawa na mchoma mkaa/mharibu miti na mazingira(suala bado lipo mikononi mwa sheria).
Environmental (Solid Waste Management) Regulations, 2009 ibara ya 30.Hoja yangu ni kuchoma taka hovyo mitaani.
Sheria haipo iwekwe kwanza.
Kuna mambo yapo, kama VIASHIRIA VYA UMASIKINI.Mambo mengi mtaani yanayofanyika kisheria ni makosa
Kama hayo ya kuchoma takataka, kutupa takataka,
Kupiga muziki
Kuuza mamantilie
Kuuza vitafunio, genge, duka au biashara yoyote bila kibali cha wataalam husika na serikali.
Tukisema Sheria ifuatwe kama ilivyo mambo yatakuwa magumu hapa.
Hiyo watu kugoma kulipa nakunga mkonoUnaleta maelezo mengi.
Kama kwako hawajazoa taka usitoe pesa ya taka.
Suala la mzabuni hajalipwa na Jiji ni mambo ya Jiji, walipeana kazi wenyewe wanajuana.
Bado haina cover situation niliyopendekeza hayo ni maeneo maalum yaliyotengwa kwa kutupa taka.Environmental (Solid Waste Management) Regulations, 2009 ibara ya 30.
Sheria hazitungwi kama unavyotaka, yaani uambiwe usichome moto hovyo, au usichome moto barazani kwako.Bado haina cover situation niliyopendekeza hayo ni maeneo maalum yaliyotengwa kwa kutupa taka.
Mimi nazungumzia uchomaji taka holela katika makazi ya watu kwa maeneo ambayo sio rasmi kwa utupaji taka.
Hiyo ni tafsiri yako hakuna kifungu cha namna hiyo.Sheria hazitungwi kama unavyotaka, yaani uambiwe usichome moto hovyo, au usichome moto barazani kwako.
Hiyo sheria, kuanzia section 22, inataka serikali za mitaa ziwe na eneo la kutupa taka. Ndio maana taka zinakusanywa kimtaa, sijui labda vijijini.
Yaani huruhusiwi kuwa na taka nyumbani kwako, mnakusanya kila baada ya muda mfupi. Maana yake ukichoma taka umevunja sheria.
Sasa kama huruhusiwi kuchoma maeneo ya kukusanya taka, utachoma taka wapi? Wakati huruhusiwi kukusanya taka eneo lisilo rasmi.