ITV ilipofunguliwa mwaka 1994

ITV ilipofunguliwa mwaka 1994

Kumbe itv imenizid umri
Halali [mention]Kelsea [/mention] anikatae[emoji28][emoji28]
Usijiskie vibaya mkuu. Mimi kuna redio ipo hadi leo kwenye room ya mzee ila kila time akiniona lazma la anikumbushe kuwa imenizidi umri 😁
 
Itakuwa ni Misanya Bingi huyo - mzee wa O.

41878325_1856114557816012_8952678072302174208_n.jpg


Aliishia kuwa Mhadhiri wa UDSM kitengo cha Sociology. Ameshafariki.
Asante mkuu.Mwamba alikitendea haki kipindi,apumzike kwa amani.
 
Dodoma Tv ya kwanza kuletwa ilikuwa DTV kama sikosei ilikuwa mwaka 1993-4,ilikuwa inachenga kinoma na hapo wahindi walitupiga heta vibaya wakizuga Kuna vifaa vinatakiwa vifungwe ndani ya TV ili ionekane bila chenga....kipindi ninachokikumbuka sana ni cha mieleka
 
Kuna ile movie ya jamaa anaishi mstuni ana fimbo moja nyeupe ambayo ina weza achanishwa katikati zikawa mbili,nilikua naipenda sana sijui inaitwaje .
 
Mi kipindi nakua nakumbuka ITV ilikua na maigizo ya Mizengwe ya Max na Zembwela, igizo la Mambo hayo akiwepo kina Dokii,Dr cheni Joti na mpoki kama sikosei.
Nawakumbuka kina Mlopelo, Muhogo Mchungu na Mzee Pwagu

Kukawa na Igizo la sayari mziki wake ukawa unaimbwa "Sayari yetu sayarii oooh sayarii[emoji445]" hapo nilikua namuona Johari, Ray, Kanumba, Mzee magari, na Ben, alafu likaja igizo la Jahazi.

Maigizo tulikua tunayaangalia marudio yake siku ya jumamosi mchana yaani siku ya jumamosi inakua Kama siku ya sherehe nawahi kuoga na ninafanya usafi kwa juhudi ili saaa 9 inikute nimeshamaliza kazi zote niangalie marudio.

Alafu jumamosi saa 3 usiku maigizo yanaendelea saa 4 usiku naangalia WWE miereka ya kina DX na John Cena kabla ya igizo kuisha kunakua na matangazo matatu , kulikua na matangazo ya chai jaba na lile tangazo la jambo lotion lotion inakata kiuono balaa
Mimi naitwa jambo kubwaa[emoji445] na wewe jee[emoji445] Mimi naitwa jambo katikatii [emoji445] na wewe jee ? Mimi naitwa jambo ndogoo[emoji445]
Daaaaah Times flies, Times flies.
John Cena wa Juzi... Mieleka enzi hizo Tunawacheki wakina Hulk HOgani ndio wababe wa Mieleka wa wakati huo

Kaole Sanaa Group walishika nchi... Kina Kibakuli....

Sent from my Redmi Note 5 using JamiiForums mobile app
 
Hata EATV (formerly Channel Five) isingekuwa kifo cha yule mtoto wa Mengi, Rodney Mutie Mengi ingefika mbali sana hapa East Africa hasa kwenye burudani kufikia sasa. Dogo alikuwa mbele ya wakati sana

ITV na EATV walibweteka na kukosa ubunifu tofauti na Azam media

IPP kwenye ubora wao walishinda tuzo nyingi sana za kimataifa kipindi kile South Africa kwenye mashindano ya media bora Africa, siku hizi siwasikii kwenye hizo tuzo, inasikitisha sana 😔

Wakati mwingine mishahara yenyewe wanalipwa hadi tarehe 40. Kuna kipindi mishahara ilichelewa ikabidi pesa za Bonite ndio zitumike kuwalipa
 
Back
Top Bottom