ITV ilipofunguliwa mwaka 1994

ITV ilipofunguliwa mwaka 1994

Kikosi kazi enzi hizo cha ITV na redio One
IMG_0759.jpg
 
Mmmh hii sikupata kusikia.
Au mlikuwa mnalipia Cable TV yaani huduma ya kupata matangazo ya TV stations kupitia cable?
TV kwa maana ya ile device sidhani kama iliwahi kulipiwa kwa mtindo huo.
Nasubiri majibu ya wengine.
Enzi hizo tulikua tunaweka antena za kipepeo unapata ITV murua kabisa. sitasahau siku nilitaka kuchoma nyumba.

Kisa; antena ya kipepeo ilikua haileti signal vizur so TV ikawa inaonesha mchele mchele na picha kwa mbali japo ilikua na msaada wa Booster. Mimi kwa utundu wa udogo si nikakonect konect booster mbili nikidhani zitasaidia kuleta signal vizur ili nizifaidi family matters, daah ile kwenda kuwasha soketi boosters zililipuka balaa moshi tu ndani na nilikua peke yangu mpaka saketi breaker ikakataa kabisa.
Jioni mzee wangu karudi anasema humu ndani hakuna umeme au umekatika? Nikamwambia umekatika wakati najua kilichotokea huku natetemeka, mbona kwa jilani upo? Kuja kugundua nilitaka kuunguza nyumba nakumbuka siku ile niliwalaza watu giza mpaka kesho yake mafundi wakaja. Mzee alinimindi balaa sana Misemo kama stupid stupid alizisema nyingi kwa kumindi. Ila sikuwaga nakoma.
Beautiful old days.
 
Tujikumbushe lile tukio la mbeya ilikuwa 96-97
"mwenye kikombe Aya,mwenye dumu Aya,kila mtu alibeba mafuta ajuwavo basi mwengine kaingia na tamaa kuchukua betri ndipo moto ukawaka "
Mbeya ili tukio
View attachment 2477761
Ile habari ilimpa umaarufu sana mzee Rainfred Masako 🤣🤣🤣


Mwenye sufuria hayaa 😅
 
Kampuni ya IPP Limited mwaka 1994 inatambulisha chaneli ya Analog kwa jina ITV kupitia masafa ya mawimbi ya kawaida kipindi hiko.

Na kipindi hiko ndio mtaa mzima tumenunua TV ya PANASONIC TX iliyotoka 1993 sikumbuki model ikiwa ya rangi.

Kipindi hiko Tv inafunguliwa saa 8 au 10 sikumbuki ila inafungwa saa sita usiku.

Ndipo nilipo jua series kama:
*Family Matters
*Perfect Strangers
*fresh prince of bel air
*The V

Na matangazo kama :
*Revlon
*cocal cola

Kipindi hiko unaamka usiku kushuhudia ngumi za Mike Tyson.

Ila kuna dada mmoja ni kama mwarabu au muhindi fulani alikuwa ndo mtu wa kwanza ITV wanafungua ndo anaonekana sana. Hivi yupo wapi miaka 30 sasa.

Wenye kuijua ITV vizuri

[mention]pasco mayala [/mention] ni moja ya watu wenye kuijua ITV
Mimi miaka hiyo bado niko kijijini kwetu Namanyere home kwetu hatukuwa hata na radio ya mbao hivyo hayo mambo ya "Tivii" nimekuja kuyajua ukubwani nilipokuja mjini
 
Mi kipindi nakua nakumbuka ITV ilikua na maigizo ya Mizengwe ya Max na Zembwela, igizo la Mambo hayo akiwepo kina Dokii,Dr cheni Joti na mpoki kama sikosei.
Nawakumbuka kina Mlopelo, Muhogo Mchungu na Mzee Pwagu

Kukawa na Igizo la sayari mziki wake ukawa unaimbwa "Sayari yetu sayarii oooh sayarii🎶" hapo nilikua namuona Johari, Ray, Kanumba, Mzee magari, na Ben, alafu likaja igizo la Jahazi.

Maigizo tulikua tunayaangalia marudio yake siku ya jumamosi mchana yaani siku ya jumamosi inakua Kama siku ya sherehe nawahi kuoga na ninafanya usafi kwa juhudi ili saaa 9 inikute nimeshamaliza kazi zote niangalie marudio.

Alafu jumamosi saa 3 usiku maigizo yanaendelea saa 4 usiku naangalia WWE miereka ya kina DX na John Cena kabla ya igizo kuisha kunakua na matangazo matatu , kulikua na matangazo ya chai jaba na lile tangazo la jambo lotion lotion inakata kiuono balaa
Mimi naitwa jambo kubwaa🎶 na wewe jee🎶 Mimi naitwa jambo katikatii 🎶 na wewe jee ? Mimi naitwa jambo ndogoo🎶
Daaaaah Times flies, Times flies.
 

Attachments

  • 20230111_205041.jpg
    20230111_205041.jpg
    27.8 KB · Views: 32
Mwenye ungo kipindi hiko anaogopeka. Sisi tuliokulia mitaa ya Sinza inayoanzia kijiweni kwenda mpaka mlimani na Mikocheni tulikuwa tunawaona watu matajiri sana.
Kipindi HICHO. Naona unarudia-rudia kipindi ''hiko''
 
Back
Top Bottom