Mi kipindi nakua nakumbuka ITV ilikua na maigizo ya Mizengwe ya Max na Zembwela, igizo la Mambo hayo akiwepo kina Dokii,Dr cheni Joti na mpoki kama sikosei.
Nawakumbuka kina Mlopelo, Muhogo Mchungu na Mzee Pwagu
Kukawa na Igizo la sayari mziki wake ukawa unaimbwa "Sayari yetu sayarii oooh sayarii🎶" hapo nilikua namuona Johari, Ray, Kanumba, Mzee magari, na Ben, alafu likaja igizo la Jahazi.
Maigizo tulikua tunayaangalia marudio yake siku ya jumamosi mchana yaani siku ya jumamosi inakua Kama siku ya sherehe nawahi kuoga na ninafanya usafi kwa juhudi ili saaa 9 inikute nimeshamaliza kazi zote niangalie marudio.
Alafu jumamosi saa 3 usiku maigizo yanaendelea saa 4 usiku naangalia WWE miereka ya kina DX na John Cena kabla ya igizo kuisha kunakua na matangazo matatu , kulikua na matangazo ya chai jaba na lile tangazo la jambo lotion lotion inakata kiuono balaa
Mimi naitwa jambo kubwaa🎶 na wewe jee🎶 Mimi naitwa jambo katikatii 🎶 na wewe jee ? Mimi naitwa jambo ndogoo🎶
Daaaaah Times flies, Times flies.