Iwapo CCM itashindwa Zanzibar, Nini Majaaliwa ya Muungano?

Iwapo CCM itashindwa Zanzibar, Nini Majaaliwa ya Muungano?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Wakati tunaelekea kusherehekea miaka 51 ya Muungano wetu adhimu, kuna taarifa za kushitusha kutoka Zanzibar!.

TAARIFA MUHIMU:
Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Magharibi Unguja kupitia kikao chake kilichomalizika muda huu Kimemvua Uanachama wa C.C.M Mzee HASSAN NASSOR MOYO na hivyo kuanzia sasa Mzee Moyo si mwanachama tena wa Chama Cha Mapinduzi.
moyo+px.jpg

Hassan Nassor Moyo
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
Kama ni kweli hili limefanyika, jee kuna uwezekano sasa CCM ndio imeamua kuuvunjilia mbali huu Muungano wetu adhimu kwa hoja za liwalo na liwe?! kwa sababu hatua hii italeta Chuki kwa Muungano, Wanzanzibari, Wataikataa Katiba Pendekezwa na October, CCM itapigwa chini!. Jee serikali ya CUF itauimarisha huu Muungano au ndio itauvunjilia mbali?!. Na hili likifanyika jee Tanzania bara tutakubali?!

Nakuomba sana Rais JK, hili usilikubali, uamuzi huu ukifika kwenye vikao vyenu vya juu, msikubali kuutekeleza!. Najua huyu Mzee amekuwa akimwaga sumu kuhusu muungano, nawashauri mhudumieni kama ambavyo mnahudumia Aboud Jumbe!. kumfukuza ni makosa!, mmefanya kosa kumfukuza Yusuph Himid, CUF wamemdaka, na sasa anaiumiza sana CCM Zanzibar!, kufanya kosa sio kosa, bali kosa ni kurudia kosa!, msilirudie kosa kama hili Zanzibar, kwa sababu sio tuu CCM itakuwa imejimaliza Zanzibar, bali itakuwa imefanya kosa la uhaini kwa kuweka mazingira ya kuvunjwa kwa huu muungano wetu adhimu!.

Mimi Pasco wa jf, sio muumini wa Muungano huu wa serikalimbili, ni muumini kwa ukweli halisi na ukweli daima wa kihistoria kuwa Zanzibar, ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!, hatihitaji muungano wowote na Zanzibar kwa sababu ni sehemu yetu ya kihistoria kabla hawajaja wavamizi fulani kutoka huko walikotoka, na kuvivamia visiwa vyetu vile, just like that as if wameviokota, ndio maana mawazo yangu kwenye muundo wa muungano, nilipendekeza Muungano wa serikali moja, Zanzibar iwe treated tuu kama mkoa wa Zanzibar wenye wilaya mbili za Uguja na Pemba!. Naamini wale Watanzania halisi, wote hili wataliafiki, ila kuna uwezekano wale vizalia vya wavamizi, ambao sasa wamekuwa naturalized wanaweza kulipinga!, hivyo nashauri kama vipi, turudi kwenye historia tulivyokuwa mwanzo, na wavamizi wote wasiotaka, tuwakusanye, tuwasombe, tuwarudishe kwao kwenye asili yao!.
kwenye hili nimeshauri Kumuepushia aibu ya Kushindwa, CCM isimsimamishe Dr. Shein

Nliwahi kuandika sana kuhusu hiki kinachoitwa Muungano.


Pasco
 
Sitarajii kuona CUF wakiuimarisha Muungano endapo watapata dhamana ya kuiongoza serikali ya Mapinduzi...

Na pia lazima tukubali kuwa CCM ya Zanzibar si CCM ya Bara...

Ndani kabisa ya mioyo yao wanaCCM wa Zanzibar sio wote ambao ni waumini wa muungano...

Nadhani nafasi pekee ambapo CCM Zanzibar itavunjika vipande ni pale tu ambapo CUF watashinda huko na wakaja na hoja ya kuvunja muungano...
 
Pasco; utakusanya wangapi kuwarudisha makwao huko znz?
Je ukimaliza na ukifanikiwa kuwakusanya huko znz kuwasomba na kuwarudisha makwao hayo mabaki ya wavamizi je hiyo kazi itakuwa imeisha huko znz au utaiyendeleza na huku bara kuondoa wavamizi wa kichaga wakisukuma wa nyachusa wakifipa na kiha nk kuwaondoa wavamizi wa dar na kuwarudisha makwao?
 
Pole sana Pasco kama bado unaamini JK na timu yake iliyopo madarakani wana uchungu na nchi yetu.

Suala la kuuvunja Muungano wameshalimaliza siku nyingi, na yote wanayoyafanya ni kujaribu kuwatupia watu changa la macho na kusingizia wapinzani, kwa maana ya CUF na wengine wote wanaodiriki kuuliza kuhusu uhalali wa Serikali ya Muungano kisheria, ya kwamba ndio wanaotaka kuuvunja Muungano.

Umeelezea msimamo wako wa serikali moja, una kila haki ya kikatiba ya kufikiri hivyo, kuna wengine kama mimi tunaofikiri serikali tatu, kwa kuwa hofu kubwa ya wazanzibari walio wengi ni 'kumezwa' na 'kaka mkubwa Tanganyika (wengine wanapenda kumwita Tanzania Bara). lakini mawazo kama yako ama yangu CCM ya JK haitaki hata kuyapa nafasi, kuyasikiliza, kuyajadili na hatimaye kutuacha watanganyika na wazanzibari tuamue kupitia sanduku la kura ambayo ni haki yetu kikatiba.

Liwalo na liwe... Wameshamfukuza uanachama mwasisi Mzee Hassan Nassor Moyo!

La kuvunda halina ubani!!!
 
Last edited by a moderator:
Nchi hizi mbili zitaletewa matatizo na CCM na si vinginevyo, kuna watu wanaiabudu CCM kwa kuwa wanaamini bila ya CCM maisha yao yatafikia ukomo na utawajuwa watu hawa kwa kuona ni kwa jinsi gani wanatumika ,na pia utagundua namna wanavyopewa uluwa na kuvishwa kilemba cha ukoka mfano Sameli Sita,tunaelewa ni kwa jinsi gani Sita alitumika kuvukisha katiba si yeye bali ni nokoa ndio kazi aliyoifanya na leo ametunukiwa fazila.

Kuhusu katiba kwa Zanzibar katiba haipo na wala haitapita ,hilo halina shaka. tusiandikie mate imebaki miezi michache sana CCM kunyongwa huko Zanzibar.
 
Wanabodi,

Wakati tunaelekea kusherehekea miaka 51 ya Muungano wetu adhimu, kuna taarifa za kushitusha kutoka Zanzibar!.

Kama ni kweli hili limefanyika, jee kuna uwezekano sasa CCM ndio imeamua kuuvunjilia mbali huu Muungano wetu adhimu kwa hoja za liwalo na liwe?! kwa sababu hatua hii italeta Chuki kwa Muungano, Wanzanzibari, Wataikataa Katiba Pendekezwa na October, CCM itapigwa chini!. Jee serikali ya CUF itauimarisha huu Muungano au ndio itauvunjilia mbali?!. Na hili likifanyika jee Tanzania bara tutakubali?!

Nakuomba sana Rais JK, hili usilikubali, uamuzi huu ukifika kwenye vikao vyenu vya juu, msikubali kuutekeleza!. Najua huyu Mzee amekuwa akimwaga sumu kuhusu muungano, nawashauri mhudumieni kama ambavyo mnahudumia Aboud Jumbe!. kumfukuza ni makosa!, mmefanya kosa kufukuza Himid, CUF wamemdaka, na sasa anaiumiza sana CCM Zanzibar!, kufanya kosa sio kosa, bali kosa ni kurudia kosa!, msilirudie kosa kama hili Zanzibar, kwa sababu sio tuu CCM itakuwa imejimaliza Zanzibar, bali itakuwa imefanya kosa la uhaini kwa kuweka mazingira ya kuvunjwa kwa huu muungano wetu adhimu!.

Mimi Pasco wa jf, sio muumini wa Muungano, ni muumini kwa ukweli halisi na ukweli daima wa kihistoria kuwa Zanzibar, ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!, hatihitaji muungano wowote na Zanzibar kwa sababu ni sehemu yetu ya kihistoria kabla hawajaja wavamizi fulani kutoka huko walikotoka, na kuvivamia visiwa vyetu vile, just like that as if wameviokota, ndio maana mawazo yangu kwenye muundo wa muungano, nilipendekeza Muungano wa serikali moja, Zanzibar iwe treated tuu kama mkoa wa Zanzibar wenye wilaya mbili za Uguja na Pemba!. Naamini wale Watanzania halisi, wote hili wataliafiki, ila kuna uwezekano wale vizalia vya wavamizi, ambao sasa wamekuwa naturalized wanaweza kulipinga!, hivyo nashauri kama vipi, turudi kwenye historia tulivyokuwa mwanzo, na wavamizi wote wasiotaka, tuwakusanye, tuwasombe, tuwarudishe kwao kwenye asili yao!.

Nliwahi kuandika sana kuhusu hiki kinachoitwa Muungano.
Jee Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano ?!...


Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano?!.


Jee Wajua Kuwa Kuna Uwezekano Tanzania Sii Nchi Halali Kisheria?!.


Bunge Maalum Lapigwa Changa la Macho!? Lapewa"Act of Union" badala ya "Articles of Union!".


Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar: Kumbe Waarabu Hawakufukuzwa Zanzibar!.


Miaka 50 Ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Bado Kuna Maswali Bila Majibu!.


'Karume Hakuyakimbia Mapinduzi ya ZnZ'-Karume


Kama kweli nia ya dhati ni kuimarisha Muungano, Then Twende Kwenye Nchi Moja Serikali Moja!.


Chonde Chonde Rais Kikwete: Msimamo wa CCM wa Serikali Mbili Ndio Utavunja Muungano!.


Pasco

Siasa za Zanzibar ni tofauti sana, CUF wataendelea kushinda na kupigwa buti na wazungu watakaa kimya sijui CCM walikwisha waambia nini kibaya kuhusu CUF
 
Ndiye Mzee pekee shuhuda wa Muungano aliyebaki na kuendelea kuishi Zanzibar. Ndiye Mzee pekee wa CCM aliyejaa hekima,heshima,msimamo,mvuto na kusikilizwa kule Zanzibar. Mzee Hassan Nassoro Moyo ni mtu wa watu. Hakika,ni moyo wa CCM kule Zanzibar. Ni alama ya Enzi na Enzi. Mwanzilishi na mjenzi wa chama kule Zanzibar. Habari za kuvuliwa uanachama wake nazichukulia kama ni utani tu wa kisiasa na zitakanushwa au kubatilishwa hima.

Mzee Moyo ni mtu wa kipekee. Mzee Moyo anasema,tangu Enzi za Hayati Mwalimu Nyerere, kile anachokiamini kwa ustawi wa chama. Mzee Moyo hang'ati maneno.Ingekuwa kuvuliwa uanachama angevuliwa na Mwalimu. Muungano ni hoja kamahoja zingine. Unazungumziwa na kufikiwa maafikiano. Si jambo la ajabu. Vinajadiliwa vitabu vya Mungu,seuse Muungano wa Tanzania?

CCM,kama bado inajipenda kule Zanzibar, isithubutu kumvua uanachama Mzee Moyo. Sisi ni chama cha kidemokrasia. Tunajadiliana na kuelewana. Tunavumiliana na kukosoana. Si ndiyo? Sera za kufukuzana tuwaachie CHADEMA!!! Sisi hatuziwezi kwakuwa hatuko tayari kwa madhara yake. Labda tujaribu kufukuza mafisadi ndani ya chama,yaani kujivua gamba.

Kuna mambo ya kujaribu, hili lakumvua uanachama Mzee Moyo halifai. Halafu, mbona wa huku Tanzania Bara hawashughulikiwi kama wale wa Zanzibar? Is it a double standard in our beloved party??

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Kila lenye mwanzo halikosi mwisho. Na huu ndio udhihirisho wa mwisho wa ccm. Ni sawa na Chadema leo hii wamfute uananchama Mtei. Hakuna awezaye kuniaminisha kuwa ccm kweli imeshindwa kuyafumbia macho maneno ya huyu mzee. Na umri wake wa miaka 80+ mmmhhhhh kweli ccm sasa ni dhahiri mmefika kikomo chenu. Ni hesabu za muda! Tuendelee kufuatilia!
 
yaan mjukuu anamfukuza babu yake kwenye ukoo!

Babu anajijua kabisa yeye sio MWIZI, lakini anakomaa na UKOO WA PANYA. Acha mapanya buku yamtimue. Ni sawa na jinsi mambwa mwitu yalivyo ukionekana una damu tu yanakutafuna, pole Mzee Moyo unafukuzwa kwenye nyumba ulioyoijenga kwa kuwa ulishindwa kuwalea wanao na wajukuu kwenye maadili, wamekugeuka...
 
CCM wanatapatapa kutafuta mchawi wakati wamejiroga wenyewe kwa matendo yao maovu.
 
Watu wenye busara wanaoongea kwa kujiamini na kusimamia ukweli kwenye maneno wasemayo hua hawana nafasi ndan ya Ccm ila wezi wa mali za Umma wanaachwa ila kwa muasisi wa muungano kufukuzwa Ccm basi mwisho wao Ccm umefika.
 
Maneno ya Mwl Nyerere lazima na karibia ya tatimia, ""upinzani wa kweli katika siasa utatoka ccm"".

Sikutegemea ccm znz ina mafisadi, ila kwa kufukuza huyu mzee msema kweli nime amini ufisadi ndani ya ccm umetamalaki, si bara tu hadi visiwani.

Wanaccm waadilifu wajichunguze wafanye uamuzi sahihi. Chama sasa kimeshikwa na mafisadi wasipo jiondoa wenyewe wataondolewa na mafisadi, imeanza kwa Moyo.

Ni vizuri walio waadilifu kujiondoa na kujiunga kwa wapinzani. Uzuri wenyewe kiasi kikubwa wapinzani wako tayari kuwapokea ili kutimia ule uhabii wa Nyerere. Hawaja chelewa wafanye maamuzi.

Niwa hakikishie kwa kufanya maamuzi ya kujitoa ccm, ccm waadilifu watakuwa wamefanya ukombozi si kwao tu, bali na kwa wanyonge wa nji hii, na pia haya ya takuwa maamuzi yenye hekima kubwa. Wala hawata kuwa wamefanya maamuzi magumu ya kifisadi tunayoimbiwa na kuaminishwa kila uchao humu mitandaoni.


Maana acha bwana! Mafisadi wana maamuzi magumu, hasa pale wanapofikwa na kashfa mzitomzito.
 
Back
Top Bottom