Iwapo CCM itashindwa Zanzibar, Nini Majaaliwa ya Muungano?

CCM wameamua kumpiga konzi Kinyago.
Kumfukuza Moyo ndani ya CCM haitawazuia wanaopinga muungano kuendelea kuupinga.
 
Ndipo pa kushangaa hapo

Mzee Tupatupa

Unashangaa?Mjuku anamwambia Babu yake hata yeye angezaliwa kwanza angemzaa.Ndiyo vijana wetu wa kidigitali.Sasa Mzee Tupatupa unaongelea demokrasia CCM?Hivi huko ipo DEMOKRASIA bila CHAPAA?

Ukipata jibu sahihi.
 
Mkuu Watu8, usemayo ni kweli, kuna mahali niliwahi kuandika humu kuwa nchi inakabidhiwa by verting not by voting, jee kama ni kweli huko Zanzibar, kila siku huwa CUF inashinda, lakini haikabidhiwi nchi kutoka na huu huu wasiwasi wa CUF kuuvunja muungano!, jee nini kitafanya hii October ndio wakabidhiwe?!.

Pasco
 
Mkuu Mwiba, hebu na tuasume usemayo ni kweli, kuwa baada ya miezi michache, CCM inanyongwa huko Zanzibar, kuna hili swali huwa nawauliza lakini mnakwepa kulijibu, ikitokea ni kweli CUF ndio imeshinda Zanzibar, inategemewa ni nani ndie atakayeutangaza huo ushindi wa CUF?!, na ni nani atakayeikabidhi hiyo nchi kwa CUF?!. Kwa lunga nyingine ni nani anayeshikilia maajaliwa ya CUF kukabidhiwa nchi ya Zanzibar, huku inaeleweka fika kuwa kuna hatari kwa mustaka bali wa muungano?!.

Pasco.
 
Muungano utadumu bila kujali ni chama gani kitashinda. Tunatakiwa kufikiria nje ya 'box' ili kuuendeleza muungano wetu. Unaweza usiwe wa aina tuliyoiona nayo (serikali mbili) lakini nina hakika hakuna atakayetaka uvunjike. Tatizo kubwa ni kwamba tumeaminishwa kwamba muungano ni lazima huwe wa serikali mbili na lazima ziwe chini ya chama kimoja - ambacho Ukiangalia kwa matendo siyo kimoja bali viwili!
 

Hehehe Kilaza haya ya Zanzibar tuachie Wazanzibar wenyewe. Hakuna hata sehem moja ktk history inayoonesha kwamba Moyo alikuwa na role ktk mapinduz bali alikuwa ni mnufaikaji wa mapinduzi kama sisi tuliozaliwa badala ya hapo. Ndio maana aliupata unaibu waziri kwa sababu ya elimu yake na hakuwa na role kwenye vuguvugu la mapinduzi
 
Ccm ni sawa na gari linalotembea huku oil ikiwa inavuja !!!
 
Siasa za Zanzibar ni tofauti sana, CUF wataendelea kushinda na kupigwa buti na wazungu watakaa kimya sijui CCM walikwisha waambia nini kibaya kuhusu CUF
Mawazo ya wazungu waseme ni kama bado unatawaliwa vile! Kwa nini wzungu waseme?
 
Wengi wanadhani sababu zilizotolewa ni kweli, ukweli ni kuwa sisi tulisema humu kuwa October CCM, itapigwa chini Zanzibar!, Octobe ndio hii, CCM imeshindwa Zanzibar!, hatua ya kuufuta uchaguzi ni hofu ya CUF wanaweza kuuvunja huu muungano wetu adhimu!.

Is this justifiable?

Pasco
 

Pasco huwa unaandika kiutani ila mada zako nyingi huwa unayoandika yanakuja kutokea kweli,ni kweli CCM wanaogopa Seif anaweza akavunja muungano na Seif ameipata hii nguvu baada ya kuwa kwenye serikali (Makamu wa Rais) na anazijua siasa za Zanzibar kuliko Shein tofauti na kina Karume na Salmin
 
kaka Pasco kama muungano ni wa haki kwa nini ccm waogope kuwakabidhi cuf zanzibar kwani ni ccm tu ndo wana haki miliki au uchungu na muungano kuliko watanzania zaid ya milion 45 na zaid ya milion 1 ya zanzbar kama watanzania pamoja na mm kwenye katiba ya warioba tulitaka serikali 3 wao ni nani wa kutupangia mm naamini ccm ni kindi la watu kama 20 tu ndo wanaweza kupingana na maamuzi ya watanganyika na wazanzbar mm ninacho sema kama wakati umefika bhasi uwez kupingana na vyakat sasa walikuwa wanawadhulimu cuf miaka yote bt for nw dunia itawakatalia na wengine watajikuta ICC marekani ameanza sasa tusubili wengine mzee wangu VUTA-NKUVUTE wambie ndugu zako wa lumumba hakuna marefu yasiyo na ncha l
 
Last edited by a moderator:
muungano bara hautusaidii sana, wazanzibar wanatakiwa wao wenyewe wajue dhamani ya muungano, zaidi ya yoote Maalim Seif ndio chanzo cha chokochoko zote za kiasiasa zanzibar kila uchaguzi unapofanyika, imefika wakati sasa aachane na siasa apumzike aachie kizazi kipya
 
............
 
Kwa utawala wa huyu Amiri Jeshi Mkuu aliyepo, hili sasa linawezekana!.
Pasco
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…