Iwapo CCM itashindwa Zanzibar, Nini Majaaliwa ya Muungano?

Ndio wale aliowataja marehemu Mtikila kuwa wanaugua ugonjwa wa Epodomia - ni unyani
 
Hii ndio sababu aliyeshinda hakupewa!.
Nawatakia mapumziko mema ya leo siku ya Muungano.

Pasco
 
Leo siku ya Muungano sio vibaya Tukijikumbusha mambo ya Muungano wetu adhimu ambao tutaulinda kwa gharama yoyote.

Nawatakia Muungano mwema.
P.
 
Na ndio maana ccm haitaki kutoa Zanzibar nje ya chama chao,wanatumia jeshi na vyombo vya dola
 



Muungano kwa nje unapicha kama ni wa hiari lakini Muungano wa Tanzania sio wa hiari kwasasa yaani hata asilimia 90% ya Wanzanzibari wakisema leo hawataki muungano hautavunjika huo ndiyo ukweli.
 
Mkuu kumbe unatamani muungano wa serikali moja yaani serikali moja ya JMT? Safi Sana ila wapenda madaraka hawako tayari kuyapoteza hivyo tusahau hilo kwa sasa.
 
Ccm haijawahi kushinda Zenji
 
Leo Tarehe 26 April, 2020 ni sikukuu ya Muungano, sikukuu hii ndio sikukuu muhimu kuliko hata uhuru kwasababu hii ni siku JMT ilipozaliwa. Lakini kutokana na janga hili la Corona, siku hii inaadhimishwa kimya kimya.
Naawatakia Muungano mwema huku nikisisitiza
Nautakia huu muungano wetu adhimu udumu milele na hivyo kukitokea yoyote anayetaka kuuchokoa muungano, namshauri chokochoko amchokoe pweza, muungano hutauweza kwasababu tutaulinda kwa gharama yoyote.
Nawatakia muungano mwema.
P
 
Mwanasiasa mkongwe na mwasisi wa Mapinduzi Zanzibar, Hassan Nassor Moyo amefariki usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake mkoani Tanga
Duh...!.
Huyu ndiye shuhuda pekee wa kusainiwa muungano wetu adhimu, aliyebaki kuwa hai.
Kifo hiki maana yake mashuhuda wote wa kusainiwa kwa The Articles of The Union Between Tanganyika and Zanzibar, wametangulia mbele ya haki.
Iwapo CCM itashindwa Zanzibar, Nini Majaaliwa ya Muungano?
RIP Mzee Hassan Nassor Moyo.
Inna lillah wainna ilayhi rajiuna

P
 

Tunapoelekea Uchaguzi Mkuu naungana na wewe, kuwa baada ya uchaguzi, Tanzania yaweza kuwa nchi moja yenye Dola moja (Serikali, Mahakama, na Bunge) au muungano wa nchi mbili zenye Serikali tatu (Serikali ya Muungano = Serikali ya Tanganyika + Serkali ya Mapinduzi Zanzibar).

Kitachotokea baada ya Uchaguzi Mkuu, iwapo:
• ACT Mzalendo (kwa maana ya Maalim Seif) kushinda uchaguzi huo (kitu ambacho ni ndoto) atataka Muungano wa Serikali Tatu, la Tanzania haitatawalika kimuungano.
• CCM ikashinda, itambue na kukubali kuwa imefika wakati wa kutokuendelea na Muungano wa Serikali mbili. Hili ni muhimu kwa kuimarisha muungano na kuitambulisha duniani kuwa Tanzania ni nchi moja.

Kwa misingi hiyo, ni busara kurejea kwenye Rasimu ya Katiba ya Warioba, uli kupitisha yaliyopendekezwa (Serikali moja au tatu). Muungano wa Serikali mbili kwa kizazi kipya ni mtihani mkubwa kwa ustawi wa Tanzania kama nchi moja. Kizazi kipya hakina mtazamo kama wa waasisi wa muungano.
 
Muungano ubaki kwenye mambo ya muungano kama makubaliano yalivokuwa. Matatizo yanasababishwa na bara kutaka kufanya mambo nje ya muungano, kama mahakama, uchumi na forodha, nk.

Muungano utadumu tukiuheshimu!
 
Huyu bwana anapenda makala ndefu sana lakini zisizo na maana, kitu ambacho angeweza kupiga summary kwa paragraph nne yeye kuandika msaafu kabisa.

Angekuwa mchungaji angekuwa anaomba saa nzima hadi watu wanaishia kula kiporo.

Muungano upo kikatiba haijalishi chama gani kinatawala upande upi wa muungano na kama ikitokea settings zikagoma si unakufa tu, kuna miungano mingi hapa duniani iliishakufa na maisha yanaendelea.
 
Mkuu mbona unaota ndoto za mchana ? CCM hakuna kushindwa
 
Nisicho kijua Huu Muungano wetu Ukifa leo (Hatuombei) Raisi wa Tanzania Itakuwaje??
Naomba Wajuzi Mnifahamishe!
 
Nawatakia maadhimisho mema ya sikukuu ya muungano.
Paskali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…