Jackie cliff: Sipendi kuona Tanzania ikiyumba kwenye suala la mitindo

Jackie cliff: Sipendi kuona Tanzania ikiyumba kwenye suala la mitindo

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
MWANAMITINDO wa Bongo aliyepo nyuma ya nondo huko Macau, Hong Kong nchini China akitumikia kifungo cha miaka sita baada ya kukutwa na hatia ya kubeba madawa ya kulevya ' unga', Jacqueline Fitzpatrick Cliff ' Jack Patrick' ametuma ujumbe mzito kwa mashabiki wake.

Mwanamitindo wa Bongo , Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick' akiwa chini ya ulinzi China. Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili, rafiki wa karibu wa Jack ambaye hakupenda jina lichorwe gazetini, alisema kwamba mwanamitindo huyo amekuwa akimuandikia barua mara kwa mara lakini safari hii ametaka ujumbe wake uwafikie Watanzania.

"Amesema watu wasimhurumie kuhusu kufungwa, amesisitiza sana juu ya suala mavazi na mitindo.

Amesema hapendi kuona Tanzania inayumba katika masuala ya mitindo ambayo yeye alikuwa akiiamini kwamba ni kazi ambayo inaweza kuwaingizia kipato watu wengi, " alisema rafiki huyo wa karibu.

‘Jack Patrick' akipozi. Rafiki huyo alizidi kuweka wazi kuwa mara nyingi Jack hapendi kuwaambia juu ya maisha ya jela kwani hapendi kabisa kuwapa watu simanzi bali anapenda watu wajue anaishi maisha ya kawaida.

"Mara nyingi Jack hapendi kabisa kueleza maisha ya jela , hapendi kuwaumiza wat , anachopenda ni kujua nini kinachoendelea katika fasheni, " alisema rafiki huyo wa Jack.

Rafiki huyo alisema kuwa Jack bado anaagiza nguo ambazo alikuwa akipenda kuvaa hasa lineni nyeupe na kuwataka watu wahisi kama yupo masomoni na atarejea tu akiwa salama.

Jack alikamatwa Desemba 19, mwaka jana akiwa amebeba madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 1. 1 katika Uwanja wa Ndege wa Macau akitokea Bangkok, Thailand kuelekea Guangzhou, China.
 
Attachments

  • 1411372850231.jpg
    1411372850231.jpg
    43.7 KB · Views: 1,485
Kama kazi hiyo ya uanamitindo inauwezo wa kuwaingizia kipato watu wengi kama anavyosema, mbona yeye alilowea kwenye madawa ya kulevya????

Yaani awaumize watu.kwa maisha yake ya jela wakati yeye kawaumiza watu kwa kusafirisha madawa ya kulevya???? Khaaaaa

Atarejea ndio ila aache upunda....
 
hajapata mchumba huko jela? mwambie yule mtoto juha sijui anayeishi kwa mama yake amechukuliwa
 
Hizi story za huyu Imelda wa GPL mimi uwa naona ni za kutunga halafu sources zake uwa eti chanzo chetu kilicho karibu na mhusika, ambacho hakikutaka kuwekwa hadharani..
Yani uwa wanatunga story ili wauze mtu yuko jela awaze mitindo kwanza story yenyewe haina mashiko
 
Hahahaa haaaa
 
Hahahaaaa..eti chanzo cha karibu ambacho hakikutaka kuwekwa hadharani
 
Hizi story za huyu Imelda wa GPL mimi uwa naona ni za kutunga halafu sources zake uwa eti chanzo chetu kilicho karibu na mhusika, ambacho hakikutaka kuwekwa hadharani..
Yani uwa wanatunga story ili wauze mtu yuko jela awaze mitindo kwanza story yenyewe haina mashiko

Ukimuona jinsi alivyo na story zake za umbea umbea ni tofauti
 
Hizi habari za jela wanazitoaga wapi jamani?
 
Hizi story za huyu Imelda wa GPL mimi uwa naona ni za kutunga halafu sources zake uwa eti chanzo chetu kilicho karibu na mhusika, ambacho hakikutaka kuwekwa hadharani..
Yani uwa wanatunga story ili wauze mtu yuko jela awaze mitindo kwanza story yenyewe haina mashiko

mpenzi.....
we hujamiss jack na swagger zake kwa red carpet.
Alikuwa anavaa kweli anawaka tena nguo zake disposable(harudii).
 
Anaeumia ni Jux na wazazi sie wengine walaaaa hata akidanja,angeongelea ajira bora hayo mavazi tutayala mfyuuuuu kaa huko huko uzae tuchina

Ndo namshangaa , kwanza wengine tulikuwa tushamsahau, jux mwenyew hana habar naye, mfyuuu eti tufikirie yupo chuo atarudi, tena angejua jinsi mastaa wenzie wasivyompenda maana bi dada alizid mashauzi
 
Ndo namshangaa , kwanza wengine tulikuwa tushamsahau, jux mwenyew hana habar naye, mfyuuu eti tufikirie yupo chuo atarudi, tena angejua jinsi mastaa wenzie wasivyompenda maana bi dada alizid mashauzi

Tumkumbuke kwa lipiiii?? Si unaona eti anaongelea mitindo yaan akili yake ipo anapopitishiwa tule tupipi twa drugs
 
Back
Top Bottom