Jackline Cliff amwandikia barua Millard Ayo toka Gerezani

Jackline Cliff amwandikia barua Millard Ayo toka Gerezani

barafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
6,739
Reaction score
32,880
image.jpeg
image.jpeg



image.jpeg


Yule mwanadada mwanamitindo kwa jina la Jackline Cliff amemwandikia barua mtangazaji Millady Ayo kutokea gerezani katika visiwa vya Macao alipofungwa kwa kosa la kukamatwa na madawa ya kulevya akiwa njiani kuyasafirisha kuyapeleka nchini China.

Ndani ya barua hiyo Jackline Cliff hajataka haswaa kuelekezea kuwa amefungwa kifungo cha miaka mingapi,amesema tu atakuwa gerezani kwa miaka kadhaa,katika barua hiyo Jack Cliff anasema amejutia kwa kiasi kikubwa kosa alilolifanya la kuwa msafirishaji wa mdawa ya kulevya,anaumia sbb kwa kufungwa kwake amewaumiza watu wengi,wakiwemo marafiki na ndugu,baada ya kuwa gerezani amefumbuka macho na kujijua kuwa yeye ni nani haswaa,analijutia kosa hilo na anaamini Mungu,marafiki,jamaa na wanafamilia watamsamehe.

Jackline anasema anajuwa kuna watu wengi wanamuhukumu na kumsema vibaya,wanamuandika magazetini na kumchafua,lkn kosa lilishatokea na hana namna ya kulibadilisha,anaomba Mungu endelee kumsimamia kwani tayari amejutia makosa yake,gerezani kumemfundisha mambo mengi na kujua hasa rafiki wa kweli ni nani na rafiki asiye wa kweli ni wa namna gani.Jackline anawashukuru wale wote wanaoendelea kumtakia kheri ktk kipindi hiki kigumu cha kukaa gerezani

Katika barua hiyo Jack ameishukuru sana familia yake kwa kuwa pamoja naye na kujitolea kumpa ushirikiano,ametoa shukrani kwa rafiki yake aliyemtaja kwa jina la "H",huyu amekuwa pamoja naye siku zote za matatizo,amewashukuru marafiki zake kama KADINDA MARTIN kwa kuendelea kuwa pamoja naye,pia ametoa shukrani nyingi sana kwa Mtanzania anayeitwa WABOGOJO aliyeko huko ambae amekuwa akimtembelea kila wiki na kumpa moyo,Jack anasema WABOGOJO kwake amekuwa kama malaika aliyeshushwa toka mbinguni kuja kumsaidia,maana hufika kila week bila kuchoka gerezani na kumsalimia.

Jack anasema anamkumbuka sana JUX ex-boy friend wake,anakumbuka nyakati nzuri walizokuwa nazo,anajisikia huzuni sana kwa kumkosa JUX na anajua jinsi alivyomuumiza na kumsababishia maumivu ya moyo,hana zaidi cha kusema juu ya JUX,amesikia juu ya mahusiano yake mapya ya kimapenzi,hawezi kumkataza maana ana uhuru huo,lkn bado ataendelea kumkumbuka na hayo yanayotokea ni sehumu tu ya maisha(Ikumbukwe kuwa JuX kwa sasa anatoka na Vanessa Mdee).Jackline Cliff anasema anamshukuru JUX kwa yote na hata kwa "support" anayompa..na kwa kweli amemkumbuka sana.

Mwisho Jack Cliff anatoa rai kwa watu wote kutomuhukumu vibaya na kumuona kama hafai kabisa katika jamii,kwani yeye hatakuwa wa kwanza wala wa mwisho kukamatwa na kufungwa sbb ya madawa ya kulevya,wanaomwandika vibaya na kumsema vibaya hana cha kuwazuia kwani kama maji yalishamwagika hayawezi kuzoleka.

Link ya kusikiliza barua hiyo hii hapa


Source:Amplifaya ya Millady Ayo 16/02/2016(Picha zilizoambatanishwa ni kwa msaada
Wa Maktaba ya mtandaoni)

=====
 
Labda kama itakuwa Milard ameihariri hiyo barua, otherwise sioni dhumuni au lengo la barua...ni kama tu aliona kalamu na karatasi, basi akaona aandike chochote.na sijui ni utafiti gani aliofanya na kujiridhisha kuwa Watanzania watapenda kusikia hayo kutoka kwake.

Ukiisoma/ukimsikiliza Milard ni kama walengwa wakuu ni hao kina Jux, Milard, familia yake n.k.

Mimi nilidhani kama mtu anakamatwa akiweka sumu kwenye chakula cha mwingine kwa lengo la kumdhuru....basi siku akiomba kuongea na ndugu wa Mdhurikaji atawaambia ukweli wa mambo ulivyokuwa.....wapi alianzia...lengo lilikuwa ni nini? ni nani wapo/walikuwa nyuma ya nia yake hiyo...ni mara ngapi alifaulu kuwekea mtu sumu bila kukamatwa, na alinufaikaje baada ya kufanikisha lengo...anajisikiaje akisikia aliyewahi kumpa sumu ameshapoteza maisha au maisha yake yameharibika na kwa sasa hajiwezi kwa lolote.....akitoka atafanya nini kuhakikisha hakuna wengine wataangamia kutoka kwa watu kama yeye n.k.

Other wise alichofanya asingeita ni barua kwa Watanzania, na ni bora tu angekaa kimya na siku akitoka jela na kutua uwanja wa Ndege Dar anyanyue kidole cha kati na kusema "wote mliochonga nawapa dole"
 
Kwangu punda sina huruma nae aseee Mungu anajua fikra zangu sina sababu za kudanganya,Punda ni wabinafsi wanaojali mafanikio yao tu bila kujali athari kwa wanaowapelekea.

Kuna story ktk zile story za vijiweni, kuwa kuna punda wa kibongo aliibukia afganstan kubeba mzigo! Babu Muuza ngada, alipigwa na butwaa kumuona punda mtu mweusi, akataka kujua anaupeleka wapi, babu alipogundua kuwa jamaa anauleta Africa, babu alilia sana, akasikitika, inasemekana babu alimwambia niko radhi nikupe mzigo bure, lkn peleka USA, huko Africa unaenda kuu ndugu zako wasio na hatia!
 
ametambua na kukiri kosa...hivo ndo inavotakiwa....
 
Back
Top Bottom