barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,880
Yule mwanadada mwanamitindo kwa jina la Jackline Cliff amemwandikia barua mtangazaji Millady Ayo kutokea gerezani katika visiwa vya Macao alipofungwa kwa kosa la kukamatwa na madawa ya kulevya akiwa njiani kuyasafirisha kuyapeleka nchini China.
Ndani ya barua hiyo Jackline Cliff hajataka haswaa kuelekezea kuwa amefungwa kifungo cha miaka mingapi,amesema tu atakuwa gerezani kwa miaka kadhaa,katika barua hiyo Jack Cliff anasema amejutia kwa kiasi kikubwa kosa alilolifanya la kuwa msafirishaji wa mdawa ya kulevya,anaumia sbb kwa kufungwa kwake amewaumiza watu wengi,wakiwemo marafiki na ndugu,baada ya kuwa gerezani amefumbuka macho na kujijua kuwa yeye ni nani haswaa,analijutia kosa hilo na anaamini Mungu,marafiki,jamaa na wanafamilia watamsamehe.
Jackline anasema anajuwa kuna watu wengi wanamuhukumu na kumsema vibaya,wanamuandika magazetini na kumchafua,lkn kosa lilishatokea na hana namna ya kulibadilisha,anaomba Mungu endelee kumsimamia kwani tayari amejutia makosa yake,gerezani kumemfundisha mambo mengi na kujua hasa rafiki wa kweli ni nani na rafiki asiye wa kweli ni wa namna gani.Jackline anawashukuru wale wote wanaoendelea kumtakia kheri ktk kipindi hiki kigumu cha kukaa gerezani
Katika barua hiyo Jack ameishukuru sana familia yake kwa kuwa pamoja naye na kujitolea kumpa ushirikiano,ametoa shukrani kwa rafiki yake aliyemtaja kwa jina la "H",huyu amekuwa pamoja naye siku zote za matatizo,amewashukuru marafiki zake kama KADINDA MARTIN kwa kuendelea kuwa pamoja naye,pia ametoa shukrani nyingi sana kwa Mtanzania anayeitwa WABOGOJO aliyeko huko ambae amekuwa akimtembelea kila wiki na kumpa moyo,Jack anasema WABOGOJO kwake amekuwa kama malaika aliyeshushwa toka mbinguni kuja kumsaidia,maana hufika kila week bila kuchoka gerezani na kumsalimia.
Jack anasema anamkumbuka sana JUX ex-boy friend wake,anakumbuka nyakati nzuri walizokuwa nazo,anajisikia huzuni sana kwa kumkosa JUX na anajua jinsi alivyomuumiza na kumsababishia maumivu ya moyo,hana zaidi cha kusema juu ya JUX,amesikia juu ya mahusiano yake mapya ya kimapenzi,hawezi kumkataza maana ana uhuru huo,lkn bado ataendelea kumkumbuka na hayo yanayotokea ni sehumu tu ya maisha(Ikumbukwe kuwa JuX kwa sasa anatoka na Vanessa Mdee).Jackline Cliff anasema anamshukuru JUX kwa yote na hata kwa "support" anayompa..na kwa kweli amemkumbuka sana.
Mwisho Jack Cliff anatoa rai kwa watu wote kutomuhukumu vibaya na kumuona kama hafai kabisa katika jamii,kwani yeye hatakuwa wa kwanza wala wa mwisho kukamatwa na kufungwa sbb ya madawa ya kulevya,wanaomwandika vibaya na kumsema vibaya hana cha kuwazuia kwani kama maji yalishamwagika hayawezi kuzoleka.
Link ya kusikiliza barua hiyo hii hapa
Source:Amplifaya ya Millady Ayo 16/02/2016(Picha zilizoambatanishwa ni kwa msaada
Wa Maktaba ya mtandaoni)
=====
- Pia soma: Jackline Cliff amwandikia barua Millard Ayo toka Gerezani
- Mrembo maarufu akamatwa na unga (developing...)
- Taarifa ya ubalozi wa Tanzania nchini China kuhusu Jackie Cliff kukamatwa na madawa ya kulevya
- Mrembo mbaroni kwa dawa za kulevya Uwanja wa Ndege
- Jackline Cliff amwandikia barua Millard Ayo toka Gerezani