Uchaguzi 2020 Jackson Kangoye agoma kumuunga Michael Kembaki Tarime, ashangaa undumilakuwili na uongo wa Bashiru na Polepole

Status
Not open for further replies.
Nafikiri shida kubwa ni uongozi mbovu wa viongozi wa CCM kwani walichohubiri na kutenda ni vitu viwili tofauti
Kamati kuu ya CCM kila mjumbe alikuwa na list yake aliyokula mpunga huku mwenyekiti akiwa na list yake ya rafiki zake mfukoni, mchujo wa kamati kuu ya CCM ni batili umejaa mapungufu urudiwe upya
 
Maumivu ya uteuzi wa wagombea ubunge ndani ya CCM bado unaendelea. Japo wengi hawasemi wazi lakini chini kwa chini kuna mgogoro mkubwa.

Katika Jimbo la Tarime mjini, aliyeongoza kura za maoni ni Jackson Kangoye na aliyemfuatia ni Michael Kembaki ambaye ndio aliyeteuliwa kuwa mgombea ubunge katika jimbo hilo.

Maamuzi hayo hayajapokelewa vyema na Jackson kwani anaamini kama tatizo ni utoaji wa rushwa wote wawili walikuwa wanatoa rushwa, hivyo angeteuliwa mtu mwingine walau angeelewa kwani kilichofanyika hakielewi na hakina maana.

Kama viongozi wetu, kuanzia Rais Magufuli, Dr. Bashiru na Polepole wangekuwa wanasimamia kauli zao basi tungetamani kuona haki inatendeka na kukata wote waliotoa rushwa, kwanini iwe kwangu tu? Alisikika Jackson akiwaeleza watu wake wa karibu.

Hadi sasa Jackson hajapongeza uteuzi wa Bwana Kembaki na yuko radhi kumsaidia Esther Matiko kwa njia zote na kimya kimya.

Maamuzi hayo yameiumiza sana familia ya Kangoye kwa sababu baba yake Jackson, Mzee Ryoba Kangoye amegombea mara 4 bila mafanikio na mwaka 2015 alishindwa na John Heche, hivyo akaamini mwaka huu walau mwanae anaweza kushinda na kuifuta familia machozi.

Viongozi wetu kina Bashiru na Polepole ni waongo na hawapaswi kuaminika tena kwani ahadi zao za kukata wala rushwa wote zilikuwa za upotoshaji na zisizo na ukweli wowote. Alisema, Charles, aliyekuwa mpambe mkubwa wa Jackson Kangoye.

CCM Tarime mara nyingi inashindwa sababu ya migawanyiko Tarime, tunasubiri kuona kitakachotokea mwaka huu 2020 kuona kama yale ya 2015 yatajirudia tena.
Kamati kuu wamekula takrima za mshindi wa pili kwa mujibu wa Le mutuz ambaye alisimama katikati akipokea Rushwa za watia nia kisha kuwapelekea baadhi ya wajumbe wenye uchu na pesa
 
Familia ya Kangonye nimeihurumia sana...kimkakati CCM wangemrudisha wakili heche awapasue mchana kweupe ushindi ni mipango.
Umewahurumia kwani waliahidiwa ubunge na Yesu Kristo? Wajiajiri tu kama sie tunavyojiajiri.
 
Maumivu ya uteuzi wa wagombea ubunge ndani ya CCM bado unaendelea. Japo wengi hawasemi wazi lakini chini kwa chini kuna mgogoro mkubwa.

Katika Jimbo la Tarime mjini, aliyeongoza kura za maoni ni Jackson Kangoye na aliyemfuatia ni Michael Kembaki ambaye ndio aliyeteuliwa kuwa mgombea ubunge katika jimbo hilo.

Maamuzi hayo hayajapokelewa vyema na Jackson kwani anaamini kama tatizo ni utoaji wa rushwa wote wawili walikuwa wanatoa rushwa, hivyo angeteuliwa mtu mwingine walau angeelewa kwani kilichofanyika hakielewi na hakina maana.

Kama viongozi wetu, kuanzia Rais Magufuli, Dr. Bashiru na Polepole wangekuwa wanasimamia kauli zao basi tungetamani kuona haki inatendeka na kukata wote waliotoa rushwa, kwanini iwe kwangu tu? Alisikika Jackson akiwaeleza watu wake wa karibu.

Hadi sasa Jackson hajapongeza uteuzi wa Bwana Kembaki na yuko radhi kumsaidia Esther Matiko kwa njia zote na kimya kimya.

Maamuzi hayo yameiumiza sana familia ya Kangoye kwa sababu baba yake Jackson, Mzee Ryoba Kangoye amegombea mara 4 bila mafanikio na mwaka 2015 alishindwa na John Heche, hivyo akaamini mwaka huu walau mwanae anaweza kushinda na kuifuta familia machozi.

Viongozi wetu kina Bashiru na Polepole ni waongo na hawapaswi kuaminika tena kwani ahadi zao za kukata wala rushwa wote zilikuwa za upotoshaji na zisizo na ukweli wowote. Alisema, Charles, aliyekuwa mpambe mkubwa wa Jackson Kangoye.

CCM Tarime mara nyingi inashindwa sababu ya migawanyiko Tarime, tunasubiri kuona kitakachotokea mwaka huu 2020 kuona kama yale ya 2015 yatajirudia tena.
Hii imekaa vizuri sana.
 
Lazima kutakuwa na wenye vinyongo tena sana japo wakati wa kampeni tutawekana sawa
 
HIVI MFANYABIASHARA ZAKARIA ALISHATOKAAYULE NDIE MNGEMPA UBUNGE HAWA NJAA WALIOBAKIA KULOGANA NA KUNA SUBIRINI
 
Ni mwendo wa bora tukose wote, haiwezekani WajvmBe waniteue mimi halafu halmashauri inikate
Nalog off
 
Kwa hiyo unauona ubora wa ccm kwa ubovu wa vyama vya upinzani?!

Tatizo la kwenu ni kijitahidi kujidharau , inakuwaje chama ambachi kinafahamika chama bora cha kisiasa Africa na bado nyinyi mnakiona hovyo ?

Hebu mtuambie kama dunia nzima inajua na mabeberu wanajua na kutamka kuwa chama bora cha kisiasa ni CCM. Hebu tuambieni nyie mnaekiponda mtuambiie ni chama gani bora ?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom