Uchaguzi 2020 Jackson Kangoye agoma kumuunga Michael Kembaki Tarime, ashangaa undumilakuwili na uongo wa Bashiru na Polepole

Uchaguzi 2020 Jackson Kangoye agoma kumuunga Michael Kembaki Tarime, ashangaa undumilakuwili na uongo wa Bashiru na Polepole

Status
Not open for further replies.
Tatizo la kwenu ni kijitahidi kujidharau , inakuwaje chama ambachi kinafahamika chama bora cha kisiasa Africa na bado nyinyi mnakiona hovyo ?

Hebu mtuambie kama dunia nzima inajua na mabeberu wanajua na kutamka kuwa chama bora cha kisiasa ni CCM. Hebu tuambieni nyie mnaekiponda mtuambiie ni chama gani bora ?
Swali langu ni rahisi sana, ccm ni bora Kwa sababu ya ubovu wa vyama vya upinzani?? Kwenye hoja yako umesema kama ccm ni mbovu je vyama vingine tuviweke wapi? Kwa hiyo una maana ccm nayo ni mbovu lakini imezidiwa ubovu na vya vingine?!!
 
Maamuzi hayo yameiumiza sana familia ya Kangoye kwa sababu baba yake Jackson, Mzee Ryoba Kangoye amegombea mara 4 bila mafanikio na mwaka 2015 alishindwa na John Heche, hivyo akaamini mwaka huu walau mwanae anaweza kushinda na kuifuta familia machozi.
Kwa mtazamo huu kama ni wa kifamilia, Bora alivyotemwa na Chama,

Mtazamo wa kijinga kabisa kuwahi kutokea
 
Maumivu ya uteuzi wa wagombea ubunge ndani ya CCM bado unaendelea. Japo wengi hawasemi wazi lakini chini kwa chini kuna mgogoro mkubwa.

Katika Jimbo la Tarime mjini, aliyeongoza kura za maoni ni Jackson Kangoye na aliyemfuatia ni Michael Kembaki ambaye ndio aliyeteuliwa kuwa mgombea ubunge katika jimbo hilo.

Maamuzi hayo hayajapokelewa vyema na Jackson kwani anaamini kama tatizo ni utoaji wa rushwa wote wawili walikuwa wanatoa rushwa, hivyo angeteuliwa mtu mwingine walau angeelewa kwani kilichofanyika hakielewi na hakina maana.

Kama viongozi wetu, kuanzia Rais Magufuli, Dr. Bashiru na Polepole wangekuwa wanasimamia kauli zao basi tungetamani kuona haki inatendeka na kukata wote waliotoa rushwa, kwanini iwe kwangu tu? Alisikika Jackson akiwaeleza watu wake wa karibu.

Hadi sasa Jackson hajapongeza uteuzi wa Bwana Kembaki na yuko radhi kumsaidia Esther Matiko kwa njia zote na kimya kimya.

Maamuzi hayo yameiumiza sana familia ya Kangoye kwa sababu baba yake Jackson, Mzee Ryoba Kangoye amegombea mara 4 bila mafanikio na mwaka 2015 alishindwa na John Heche, hivyo akaamini mwaka huu walau mwanae anaweza kushinda na kuifuta familia machozi.

Viongozi wetu kina Bashiru na Polepole ni waongo na hawapaswi kuaminika tena kwani ahadi zao za kukata wala rushwa wote zilikuwa za upotoshaji na zisizo na ukweli wowote. Alisema, Charles, aliyekuwa mpambe mkubwa wa Jackson Kangoye.

CCM Tarime mara nyingi inashindwa sababu ya migawanyiko Tarime, tunasubiri kuona kitakachotokea mwaka huu 2020 kuona kama yale ya 2015 yatajirudia tena.
Maamuzi hayo hayajapokelewa vyema na Jackson kwani anaamini kama tatizo ni utoaji wa rushwa wote wawili walikuwa wanatoa rushwa, hivyo angeteuliwa mtu mwingine walau angeelewa kwani kilichofanyika hakielewi na hakina maana.

*********
Mwambie atangulie mwenyewe kwenye ofisi za TAKUKURU zilizo karibu naye atakuta maagizo yangu...

Jinga wahedi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom