TANZIA Jackson Makwetta (Mbunge na Waziri wa zamani) afariki dunia

Pia aliwahi kuwa waziri wa elimu enzi hizo nikiwa chekechea
 
Usiiseme serikali tu hata katika jamii zetu misiba yawatu wenye nacho Ndio watu wanaishobokea hiyo ni nature ya binadamu
 

Ni kwa sababu alikuwa mbunge kwa muda mrefu na hakutumia uwaziri wake kuiba mali ya umma ili kupeleka miradi ya maendeleo kwa wananchi kwa fedha za ufisadi kama wenzake waliokamata nyadhifa hizo;
 
Very very sad news. Pumzika kwa amani Mzee wetu na poleni sana wanafamilia, ndugu na marafiki.

NB: Tangazo la kifo toka ofisi ya Waziri mkuu wametumia neno 'Bwana'! Kwanini hawakutumia 'Ndugu' badala ya Bwana? Marehemu alikuwa true 'ndugu' na alikuwa kati wa watu wachache walioamini (na kuishi) dhana ya undugu. Rekebisheni hili nyie watu wa ofisi wa Waziri Mkuu.
 

ni makosa ya kibinadamu,ni mambo ya kawaida muhimu alikubali kushindwa,hakujiingiza ktk matendo ya kuchakachua kura!
 
Alifanya nini huyo Jackson Makweta aliyekuwa waziri miaka 25, zaidi ya kwamba hakuiba, "amejengewa nyumba na watoto wake."

Ana legacy gani huyu waziri.
 
Poleni sana wote tulioguswa na Msiba huu,
Poleni Watoto, Familia, Ndugu na Jamaa, Marafiki, Wananchi wa Njombe, Wananchi na Watanzania na Watu wote.
Kazi ya Bwana Haina Makosa, Bwana alitoa, Na Bwana ametwaa na Jina la Bwana na lihimidiwe.
Tumuenzi kwa kuendeleza Mazuri aliyoyaacha.
Amein Amina Amen.



Ni aliyekuwa mbunge wa huko Njombe na waziri katika serikali ya awamu ya kwanza na ya pili Mhe. Jackson Makwetta amefariki dunia jioni ya leo.

Alazwe pema peponi

Chanzo: Ndugu wa karibu na marehemu.
 

Kuna wakati wananchi wanapotezwa na kampeni Chafu ni kuwasamehe (Ufinyu wa Mawazo) Huyu Mzee alikuwa Mwadilifu na Mtu wa Haki...Hata hao waliosema kuwa wamemchoka na kumzomea dhamira zao lazima zinawagharimu kwa sasa.....Ndio Binadamu wengi tulivyo.... Ukweli unabaki wazi kuwa amelitumikia Taifa la Tanzania kwa uadilifu mkubwa sana...RIP Mzee wetu mwadilifu kabisa, Pole kwa wanafamilia, Mungu awape nguvu na subira.
 
Pamoja na kuwa na mawaziri kibao wa elimu kama akina Mayagila, Mgonja, Kapuya, Mungai n.k, marehemu Makweta ni bora kuliko wote. Namkumbuka sana kwa kuanzisha mtihani wa kidato cha pili.

Poleni sana wafiwa, RIP Makweta, J.

Bila kutafuna maneno Marehemu Kighoma Ali Malima ni waziri wa kwanza wa Elimu TZ aliebadilisha mfumo wa majina kwenda mfumo wa namba ktk mitihani ya sekondari baada ya kugundua ubaguzi na uchujaji wizarani!

Huyu ni Waziri bora kabisa alieiongoza Wizara ya elimu miaka ya 80 na kuleta mageuzi makubwa ktk wahitimu na kusababisha lawama kubwa toka upande wa pili na kumshinikiza Rais Mwinyi kumbadilishia Wizara!
 
Kwa wanaonielewa wamenielewa; unafiki wa viongozi wetu kwenye misiba kama hii upo pale pale ndugu yangu; Na sitabadilisha kauli yangu;

Hakuna aliekuelewa ndio maana kimya! sasa maana yako ni nini kuipakazia CCM kuwa huwa inajipendekeza tu kwa mafisadi pale wanapokufa kwa mazishi ya kitaifa? swali langu bado hujajibu! Jee, Mwalimu nyerere alizikwa kwa heshima zote zinazostahili tena yalikuwa ya kimataifa maana maombi yalianzia ktk makanisa ya Uingereza! sasa yeye nae kwa maoni yako alikuwa fisadi? naomba jibu hapa ili nikuelewa!

Natanguliza shukrani mkuu!
 

Jibu langu ni kwamba CCM ya sasa haina utamaduni wa kuwaenzi viongozi ambao walikuwa ni waadilifu; mifano ipo mingi, na inatakuwa ulitambue hilo badala ya kuja na mifano ya sokoine, nyerere na kawawa; natamani ningeelezea jinsi gani Mzee Makweta, licha ya kuwa muaminifu, mwadilifu na mzalendo kwa nchi yake ameteseka sana kutokana na kutekelezwa katika kipindi chote cha ustaafu wake hadi uhai wake ulipochukuliwa na Mola; Haina maana kwamba ni jukumu la chama na serikali kutunza kila kiongozi, bali kuna mengine ya aibu ambayo sina haja ya kuyajadili; Na sio yeye tu, orodha ni ndefu na mifano hai ni mingi; naomba niliachie hili suala hapa, na tukubaliane tu kutokubaliana, vinginevyo ningependa kurudia tena - sitabadilisha kauli yangu ya awali;
 
''mbele ya kifo hautambi, kifo ni kiboko yao''...
RIP Dr Remmy
 

Kama unazungumzia kuenziwa baada ya kustaafu sio CCM tu iliyowasahau wastaafu wao hata vyama vya upinzani kama CDM vilimsahau Mzee Brown Ngululupi, Bob Makani waanzilishi wa CDM na kuwakumbuka tu pale walipofariki huku wakimuenzi Mzee Edwin mtei pekee na kumpa umuhimu wa pekee kwa kutolea maoni pinzani maamuzi ya viongozi halali wa chadema na kutia shaka kwamba huenda Chadema wana agenda ya siri!
 

Sizungumzii suala la kuenzi mtu, kwani utawaenzi wangapi? Suala ni kuto-wathamini katika nyakazi ambazo ilitakiwa kuwathamini, hasa wanapohitaji msaada hata juu ya madai yao ya haki kama vile pension, n.k; pia Mzee Makweta Serikali haikuwa na sababu yoyote ya maana ya kumwacha aingie katika ustaafu katika hali aliyokuwa nayo bila ya kumwangalia kama wenzake wengi waliotumikia nchi yao walivyoangaliwa, hasa wale wa kipindi cha 2000 na kuendelea; Nisingependa kujadili sana suala hili kwani mimi sina ukaribu wowote na familia ya marehemu lakini yaliyomkuta mzee huyu taarifa zake zilikuwa wazi; nadhani tuachane na huu mjadala kwa manufaa ya familia yake;
 

This is how this country (our government) treats those who work honestly, letting them die like dogs. Td
 
Mchamuzi watu wengine hawakuelewi hivi kwanini huyu hawakumpeleka India badala yake wakamuacha ajifie Muhimbili? Then tuseme serikali injali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…