Kweli wewe huna ulijualo,ngoja tukusaidie kufafanua.Ni hivi hilo swala la WATOTO KUWA NA HAKI SAWA lipo hivi,watakuwa na haki sawa tu kwa ile share ya Baba yao basi.Hata kabla Mengi na mkewe mkubwa hawajafariki tayari hao watoto wakubwa walikuwa wana miliki shares 25%.Ile 75% iliyobaki ilimilikiwa na Wazazi wao kwa maana ya nusu kwa nusu.Hawa wakubwa Mama yao alipofariki wakarithi shares za Mama yao pia.Mpaka hapo unaona nani ana majority shares? Ndiyo maana Jack alikuwa anataka hizi za Mengi apewe yeye peke yake na wanae ndiyo maana kwa Millard Ayo alisema wale wakubwa walisharithi kwa Mama yao kitu ambacho hakiwezekani,hapa sasa point yako inakuja Watoto wote wana haki sawa ya kurithi kwa Baba yao.Kwa maana hiyo hawa Wakubwa watachukua na sehemu ya shares za Baba yao,wakichangaya na zile zao kutoka kwa Mama yao na zao nani anakuwa more powerful?
Ndugu yako Jack alijichanganya tu,alipaswa kuwa na mali zake binafsi wakati Mzee yupo hai,ili watoto wake wanachopata kutoka kwa Baba yao angewaongezea na kile alichonacho yeye Mama yao.Sasa hawa wadogo wanapata kwa Baba tu peke yao wakati wale wakubwa wanapata Kote kwa Mama na Baba yao.Mshauri Jack apambane awatafutie pia wanae ili waje kurithi na kwa Mama yao kama wale wakubwa walivyo rithi kwa Mama na Baba.Tumeelewana?