Kwa uelewa wangu mdogo Wa sheria za ndoa kuna machache ya kujiuliza yanayoweza kukupa majibu.
Kwanza, kama Mengi hakumuacha mke wake kwa taratibu zinazotambulika ki mahakama, Je akioa tena iyo ndoa ya pili itakuwa halali? Ndio maana uliona Jacky anaulizwa kama anao ushahidi Wa Mengi kumuacha mkewe akabakia kusema mume wangu aliniambia ivyo unfortunately mahakama hazitumii hearsay kama evidence, ilitakiwa aweke divorce papers mezani.
Pili ambayo ni muhimu na naona wengi hawaizungumzii, Je ndoa zinazozofungwa nje ya nchi kwenye foreign jurisdiction, wanandoa hao wanaporudi nchini iyo ndoa inatambulika kisheria automatically au kuna taratibu lazima wafuate ili ndoa yao itambulike mfano kusajili ndoa yao to the marriage registrar.
Na ata kama ndoa yako itatambulika nchini, lazima ujue in case of a dispute ni sheria zipi za ndoa zitatumika, sheria za nchi mlizofunga ndoa au sheria za nchi ambazo wanandoa wana makazi ya kudumu( permanent residence).
Nilivyoona tu mzee Mengi kampiga huyu slay queen destination wedding nikaamini kweli anao watu wazuri( wanasheria) wanaomshauri vizuri. Inawezekana mama Mercy Mengi kujua izo grounds ndio maana hakutaka kupoteza muda wake na hio ndoa ya mshua.