Nimeongelea kwa general view ya ulimwengu, sijaongelea upanda wa mengi na wakeze.
Anyway kwa upande wa mengi mwenye Mali ndo huamua nani apate. Anaweza amua nyima watoto wake akampa kimada ili hali kama aliandika wosia wa namna hiyo.
General view ya ulimwengu au Mtuzamo wako?
Hivi unazani watu wana amua amua tu?
We jiulize pamoja Mengi alikuwa na matatizo na marehemu mke wake,lakini bado kampuni zote zilikuwa zinashikiliwa na wanae,apo ndio uone Mengi anawaamini na kuwapenda wanae kuliko kitu chochote sababu anajua machungu waliyoyapitia ktk kutafuta mali.
Sizani kama Mengi aliamua hivyo sababu ukitizama ,Mengi aliwaandaa watoto wake tokea wakiwa wadogo waje kuendesha biashara zake sababu anajua hawata msaliti.
Mimi na kwambia siku zote sisi wanaume tuna waamini sana watu tulianza kutafuta nao,nina watu watatu na wafahamu wawili wanajeshi mmoja alikuwa jangili miaka ya 97 .Hawa wanajeshi wawili walikuwa na nyumba ndogo baada ya kustaafu wamerudi kwa wake zao mafao yao wamewapa wake zao na wote walizaa nje mmoja kishavuta na mali zake zote kampa mke mkubwa.
Sasa huyu jangili kesi yake inataka kufanana na Mengi alikuwa na mali nyingi mno nyumba magari,mabasi mashamba nk,yy naye alitengana na mke wake wa ndoa akaenda kwa nyumba ndogo,kazaa nae akamjengea Nyumba.
Wakati mzee anaumwa mke mkubwa alisikia akaenda kumuomba yule mke mdogo kwamba amwache basi amuuguze mumewe yule mke mdogo akakataa.
Siku mzee kavuta watu wakazika mzee kumbe ana mwanasheria wake ambaye wanandugu wanamfahamu,amesoma usiha pale mke mdogo na mtoto wake mwakaambulia nyumba wanayo kaa na magari mawili,mali nyingine zote kapewa mke mkubwa na wanawe,bi mdogo pale pale akazimia,kuamka wenzake washaondoka.
"Uliyetafuta naye kuni ndiye wakuota naye moto"
Tuiachie mahakama wao ndio wamuuzi wa mwisho.