Jacqueline Mengi: Maneno ya kashfa na kumchafua mume wangu yamesemwa mahakamani, sikubali usuluhishi hadi yakafutwe

Jacqueline Mengi: Maneno ya kashfa na kumchafua mume wangu yamesemwa mahakamani, sikubali usuluhishi hadi yakafutwe

Tupe ushahidi wa Mengi kuachana na Mke wake wa kwanza.

Jack atapewa urithi lakini unaolingana na mchango wake katika utajiri wa Mengi.
Tupe ushahidi wa Mengi kuachana na Mke wake wa kwanza.

Hii kauli mpaka sasa inanipa mawazo. Ina maana kama hawakuachana na mkewe officially kwamba ndoa ya jacky ni batili[emoji119][emoji119]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Millard Ayo amekaa na mwanadada Klynn au Jacqueline Ntuyabaliwe na kuzungumzia tweet maarufu aliyoiweka wiki iliyopita.

Fuatilia mahojiano:

Millard: Ulikutanaje na Reginald Mengi?

JNM: Mara ya kwanza tulikutana kwenye ndege. Tulikuwa tunaelekea London. Tulisalimiana na kubadilishana namba.

Millard: Mengi alipohojiwa na Jeff Koinange alidai kwa alikuita London hukutokea. Akawa anakupigia hupokei. Ni kweli na kwanini?

JNM: Kwanza nilikuwa namuogopa halafu nilikuwa nje ya London hivyo nisingeweza kutoka mwenyewe na kwenda London.

Millard: Unauzungumziaje uhusiano wenu?

JNM: Ulikuwa bora kuliko mahusiano yote niliyowahi kuwa nayo maishani mwangu.

View attachment 1375931

Kwa waliomjua “Reg” alikuwa kijana sana ndani. Tulikuwa tunasafiri sana na kutoka. Tushaenda pamoja show ya Rihanna.

Millard: Alipokutongoza ulitafuta washauri?

JNM: Tulikuwa marafiki kwa muda mrefu wa takribani mwaka 1 kabla ya kuwa wapenzi hivyo sikutafuta mshauri.

Millard: Ulikubali siku hiyo hiyo?

JNM: (Anatabasamu) Sio lazima siku hiyo hiyo ila nilifanya maamuzi mwenyewe.

Millard: Umetimiza miaka 41 hivi karibuni. Je, unatarajia kuolewa tena?

JNM: Ni ngumu kujibu hili swali nikiwa bado nina maumivu ya kufiwa.

Wanasema never say never ila sio lazima kwangu kwani nimeshabarikiwa kupata mume ambaye alikuwa kwa ajili yangu

Millard: Juzi uliandika ujumbe twitter.
View attachment 1375936 Je, ni mara ya ngapi kuzuiwa?

JNM: Kuzuiwa ni mara ya kwanza ila kuna mengi zaidi ya hilo ndo yamepelekea niandike tweet ile

Shemeji wa mume wangu alifariki hivyo nikaenda na watoto na dada yangu kuzika. Baada ya mazishi nikataka kwenda kuweka maua kwenye kaburi la mume wangu.

Mume wangu amezikwa kwenye makaburi ya familia ambayo yako kwenye nyumba ya familia anapoishi Shemeji yangu Benjamin ambaye ni mdogo wa mwisho wa mume wangu.

Tulienda na kukuta geti limefungwa hivyo tukagonga. Mlinzi akaja na kukataa tusiingie akisema lazima nimuombe Benjamin kuingia. Haijawahi kutokea na tumewahi kwenda mara nyingi hivyo nilipata hasira tukaanza kujibishana.

Iliniuma sana kwa sababu watoto walikuwa wanasikia. Wakaanza kulia. Ilinikwaza sana.

Wakati marehemu mume wangu amefariki tulipata mzozo wa wapi azikwe.

Hatukuwa na nyumba kule Machame hivyo tulikuwa tukienda tunafikia kwenye nyumba ya familia ambapo Benjamin anaishi kwa sababu ndiye mtoto wa mwisho wa kiume. Mume wangu akataka ajenge nyumba ili tukifika tuwe huru.

Baada ya sisi kujenga nyumba yetu, mume wangu aliniambia kuwa anataka azikwe pale.

Baada ya kifo chake nilisema wish ya marehemu ila familia ilipinga. Katika kuepusha shari nilikubali.

Sasa nahisi haya yanatokea kwa sababu sikusikiliza aliyoyataka.

Millard: Unasema umenyamaza kwa mengi. Ni yapi hayo?

JNM: Baada ya Mengi kuumwa Dubai walikuja Regina(mtoto wa kwanza wa marehemu Mengi) na Benjamin

Baada ya mume wangu kufariki moja ya maneno yaliyokuwa yakisemwa ni kuwa mimi ndiye niliyemuua.

Tulikuwa na Balozi wa Tanzania kule na alishauri Benjamin akifika Tanzania azungumzie suala lile kwa ukweli au uongo wake ili “kuclear air” kwa sababu mengi alikuwa mtu wa watu na maneno kama yale ni hatari watu wanaweza hata kuniua

Benjamin alipofika Tanzania hakuzungumza lolote. Ilinikwaza lakini nikapotezea.

Baada ya mazishi wosia wa marehemu ukaletwa ukasomwa tukamaliza. Sikumuona tena Benjamin

Mume wangu alitaja watu 4 wa kusimamia mirathi. Baada ya muda nikasikia Benjamin na mtoto wetu mkubwa wamepinga wosia Mahakamani.

Nilitegemea sisi ni familia hivyo wangekuja tuyazungumze.

Kitu kilichonikwaza ni kwamba lazima unapopinga wosia ueleze sababu; Benjamin ameeleza mambo ambayo kwa jinsi nilivyomjua mume wangu ambaye alifanya kzo hadi mwisho wa maisha yake si ya haki.

Ni maneno ambayo nisingetarajia mtu angeyasema kuhusu mtu aliyefariki ambaye hawezi kujitetea. Sio haki

Millard: Ulitafuta viongozi wa familia?

JNM: Kiongozi wa familia ndiye Benjamin.

Baada ya msiba kwisha niliumwa mguu sikuweza kutembea wiki 3. Katika kipindi hicho waliitisha mkutano wa familia nikawaambia naumwa. Walikutana hivyo hivyo.

Nimewaeleza viongozi wa kanisa. Sina pengine pa kukimbilia.

Millard: Ulisema umechoka, nini umepanga kufanya?

JNM: Nimeamua kuwa nitaongea kama hivi. Wanangu wana umri mdogo sana, miaka 7. Hawakukaa na baba yao kwa muda mrefu. Maneno yaliyoandikwa na uncle wao mahakamani chini ya kiapo ni mabaya na yatawaumiza. Kwa sababu lazima yatakuja kujulikana. Hivyo naongea ili wajue kuwa si ya kweli na mimi kama mama yao nilitumia nafasi yangu kumtetea mume wangu.

Millard: Kesi ya mirathi mahakamani imeisha?

JNM: Haijaisha na mimi wala watoto bado hatujaingia kuwa part ya kesi.

Millard: Kama familia mmekuwa mkipenda sana privacy na kufanya mambo yenu mbali na public eye. Huoni umekosea kwa kuweka tweet ile?

JNM: Mambo yakishaenda mahakamani sio siri tena. Mtu yeyote anaweza kuyaaccess. Familia hukaa na kujadili, mahakama ni last resort.

Millard: Uhusiano wako na watoto wenu wakubwa uko vipi?

JNM: Siwezi kuzungumzia uhusiano wa watoto na baba yao ila mimi nimeishi na Reginald miaka 9. Abdiel alikuwa anakuja mara kwa mara pale nyumbani hivyo nimemzoea. Regina hakuwa anakuja hivyo sikupata namna ya kuzoeana naye.

Millard: Documents zilizovuja mtandaoni zikidaiwa kuwa ndio wosia wa Mengi ambamo hata dada yako ametajwa ni za kweli?

JNM: Mume wangu alikuwa anapenda kusema “Watoto wote ni wangu awe amezaa Jacqueline au Mercy” hivyo alitaka wapate haki sawa. Haki zote walizopata wakubwa kama kusomeshwa na kadhalika alipata wadogo wapate.

Kuhusu Wosia

Nimeulizwa sana na watu private kuhusu wosia. Sijui nini alikuwa anawaza alipoandika wosia ule ila naweza kusema kuhusu maongezi tuliwahi kuwa nayo kama mke na mume.

Alinieleza kuwa baada ya kuachana na mkewe waligawana mali. Sijui ni kwa kiasi gani lakini let us say 50/50. Mkewe alibaki na watoto wawili, hivyo alisema kuwa shares za watoto wakubwa ziko huko ingawa walikuwa na shares zao binafsi. Hata mama yao alipofariki wao ndio warithi. Hivyo wameshapata mgao wao.

Ule wosia uliosambaa mtandaoni ndio wosia halisi ambao tuliufungua.

Wosia unasema share zake zote zilizobakia katika kampuni alizokuwa nazo akiwa kwenye ndoa ya kwanza zigawanywe kati ya mapacha wetu.

Zile za makampuni aliyoanzisha baada ya kutengana na mkewe zigawiwe kwangu na wanetu wawili (Jaden na Ryan).

Millard: Ni kweli umepata asilimia 50 ya mali?

JNM: Hapana

Millard: Lakini inasemekana amekuachia sehemu kubwa sana ya mali zake na kwamba uliinfluence hilo

JNM: Mimi na Reginald hatukuwahi kuzungumzia urithi. Ukiishi na mtu unayempenda, the last thing unataka kuongelea ni yeye kufa. Sikuwahi kumuuliza eti ukifa itakuwaje kwani sikujua yupi kati yetu atatangulia.

Millard: Wakati kesi ya mirathi inaendelea mahakamani, ni vitu gani unasimamia hivi sasa?

JNM: Hakuna hata kitu kimoja ninachosimamia. Vinasimamiwa na watoto wetu wakubwa.

Millard: Kuna maneno yanazunguka kuwa umekataa kufanya usuluhishi. Ni kweli?

JNM: Wakati mume wangu yuko hai sikuwahi kujua kuhusu mgogoro wowote. Baada ya kufariki na wao kwenda mahakamani kuna watu wamenifuata. Wengine ni marafiki wakubwa wa marehemu. Nimekuwa nikisema napenda kupatana ila kabla ya kupatana, yake maneno yaliyozungumzwa kuhusu Reginald akiwa yuko kaburini hawezi kujitetea yafutwe na yaondolewe.

Mume wangu ambaye alijiheshimu, alijijengea jina lake na kufanya kazi miaka yote hadi karibu na kifo chake eti sababu ya mali achafuliwe akiwa hawezi kujitetea? Siwezi kukubali na mtu pekee wa kumtetea ni mimi.

Mali igombewe ila sioni sababu ya kumchafua mume wangu.
Millard: Ukweli wa yaliyotokea Dubai ni upi? Inadaiwa ulimpeleka Mengi kwenye hospitali ambayo si ile anayotibiwa kila mara

JNM: Mume wangu hakuwahi kutibiwa Dubai. Alikuwa na umri ulioenda lakini hakuwa mtu wa kuugua mara kwa mara. Alianguka ghafla tukiwa hotelini na tukaelekezwa na wafanyakazi wa hoteli hospitali ya kumpeleka. Hivyo huo ni uongo!

Millard: Ni mara ya ngapi mlikuwa mnaenda Dubai?

JNM: Mara nyingi tumeenda huko. Hata engagement yetu ilikuwa Dubai. Hata new year 2019 tulikuwa huko.

Millard: Kuna taarifa zilisambaa kuwa ulikuwa na uhusiano na jamaa fulani ambaye ni kijana sana na kwamba huku ulikuwa kwa ajili ya ndoa tu ila moyo wako ulikuwa kwa huyu kijana

JNM: Haya maneno yamesemwa baada ya mume wangu kufariki. Nikabaki najiuliza why yasisemwe akiwa hai kama kweli hao watu waligundua?

Millard: Unamfahamu huyo jamaa?

JNM: Namfahamu. Ni mtu anafahamika mjini.

Millard: Una mawasiliano naye?

JNM: Namfahamu miaka mingi, ni mtu ameishi Tanzania miaka mingi. Alikuwa Darling enzi hizo wanafadhili show za urembo. Sijawahi kuwa kwenye mahusiano naye

Millard: Baada ya uvumi huo alikutafuta?

JNM: Hapana. Hatuna uhusiano wa namna hiyo wa kutafutana.

Millard: Comments za mtandaoni zina effects gani kwako?

JNM: Nilivyoanza uhusiano na mume wangu yalizungumzwa mengi sana. Ila mimi ni public figure huwa napuuza. Kuna mambo yanaumiza.

Nilivyopoteza mume nilipoteza kila kitu. Nilikutana na Reginald wakati baba yangu anaelekea kufariki. Yeye ndo alinizuia nisijiue baada ya baba kufariki. Alikuwa Mume, Baba, Rafiki na kila kitu.

Hivyo maneno haya wakati amefariki sikujali wala kuelewa kwa sababu hakuna maumivu yangezidi yale niliyokuwa nayo. Nilikuja kuyaelewa baadae sana. Nimeamini kuna binadamu wana roho mbaya.

Millard: Umewahi kujiuliza kwanini wakuhusishe na jamaa huyo out of nowhere?

JNM: Nisingependa kujihangaisha na kile kitu. Watu hawana jema, leo hili, kesho lile. Hivyo nimeaccept tu labda ni chuki au kuna sababu nyingine.

Millard: Ikitokea kwenye kesi hujapata kiasi fulani kikubwa cha mali itakudisturb?

JNM: Kinachonidisturb ni namna jina la mume wangu linavyokashifiwa. Kwanza mali yenyewe si kwamba nyumba moja inakatwa katikati, ipo mali ya kutosha sana.

Kinachouma ni kuwa aliyezitafuta anakashifiwa na kuchafuliwa.

Millard: Suala la dada yako kutajwa kwenye mirathi hujalizungumzia

JNM: Mume wangu alitaja wasimamizi 4 wa mirathi ambao wawili ni ndugu na wawili ni wa kwenye kampuni. Dada yangu aliwekwa kama reserve endapo mmoja kati ya waliotajwa atakataa nafasi au kufariki.

Millard: Unasema mumeo alikusaidia usijiue kipindi baba yako amefariki?

JNM: Baba yangu alikuwa kila kitu kwangu, sikuwa na watoto wakati huo. Alipofariki sikutaka kuishi bila yeye. Mume wangu alinisaidia kupita kipindi kile kigumu. Na pia 2012 alinipa watoto. Nawapenda wanangu na wananipa sababu ya kuishi.

Mimi na baba yao tuwapenda sana na tulitaka watimize ndoto zao na watimize ndoto zetu kwao.

Millard: Ni kweli wanasomea nyumbani?

JNM: Hapana. Wanaenda shuleni.

Millard: Nani kimbilio lako katika magumu unayopitia?

JNM: Huwa naongea na dada yangu, sometimes nakaa kimya, sometimes naongea na marafiki. Nina marafiki wanajali sana, hata nisiposema lolote huwa wanakuja kukaa na mimi.

Millard: Nyumba mliyojenga Machame bado una access nayo?

JNM: Ndio. Mume wangu aliniruhusu kusimamia ujenzi. Nilitimiza ndoto zangu katika ile nyumba.

Millard: Ni kweli mzee alikuwa hana pesa akataka muende Zanzibar lakini ukaforce muende Dubai?

JNM: Maisha ya mume na mke ni private lakini nadhani ukiwa maarufu watu watataka kuingia hadi ndani kwenu.

Safari ile ilikuwa kwa ajili ya watoto. Reginald aliwapenda sana watoto. Alitaka kila wakiwa likizo tusafiri. Tulienda Zanzibar ila akahisi hawakuenjoy vilivyo kwani tulikuwa sehemu ya kimya sana. Akasema twende Dubai ili waenjoy zaidi. It was his idea.

Millard: Wewe ni mke wa bilionea. Je, unaenjoy maisha kama watu wanavyodhani?

JNM: Siwezi jua wanadhani nini hivyo siwezi kuzungumzia hilo

Millard: Wanadhani unakula bata siku nzima

JNM: Mimi ni mama hivyo ukiwa mama una majukumu mengi. Napenda kuongea, kucheza na wanangu. Muda wangu mwingi ni kwa ajili yao.

Baada ya hapa walifanya chitchat za hapa na pale.

===== END=====​
MAHAKAMA ipo kivukoni, haipo JF, njoo hata kwangu room no. 76 masjala kuu nikupe ushuri.
Hao akina Nancy Sumari na wakili wako wanakupoteza, wanaogopa kukwambia ule wosia haukukidhi vigezo na hivyo ni sawa na haupo, oops
 
Tupe ushahidi wa Mengi kuachana na Mke wake wa kwanza.

Hii kauli mpaka sasa inanipa mawazo. Ina maana kama hawakuachana na mkewe officially kwamba ndoa ya jacky ni batili[emoji119][emoji119]

Sent using Jamii Forums mobile app

Kisheria mwanaume aliyeoa hasa ndoa ya Kikristo hawezi kuoa mwanamke mwingine bila kutangua ndoa ya kwanza. Tena iwepo divorce document inayothibitisha hayo. Vinginevyo ndoa ya pili itakuwa batili.
 
Tupe ushahidi wa Mengi kuachana na Mke wake wa kwanza.

Jack atapewa urithi lakini unaolingana na mchango wake katika utajiri wa Mengi.
Kuhusu Mengi kuachana na mke wake hiyo inajulikana sana lbd kama hizo talaka/nyaraka hazipo.Na wala sio madam au huyo Jacky tu kaspend nao wapo wengi ila aliamua kutulia na JackJack. Pesa atapata maana kashazaa tayari na watoto ni wadogo na haitakwepeka kuwa ile ni damu ya Mengi. Sijaona kosa lake lbd hapo kwenye huo wosia ndipo alipoharibu. I hope mahakama /ukoo utafanya maamuzi sahihi juu ya hizo mali
 
Kisheria mwanaume aliyeoa hasa ndoa ya Kikristo hawezi kuoa mwanamke mwingine bila kutangua ndoa ya kwanza. Tena iwepo divorce document inayothibitisha hayo. Vinginevyo ndoa ya pili itakuwa batili.
Nipo curious mbona ile ndoa haikuwekewa pingamizi na Mama Mercy alikuwa hai?
 
Zaidi ya million mia moja kwa mwezi.
Kama sikosei mama mercy alimwambia mengibkama unataka kuoa hiko kimwanamke chako basi tukubaliane utakua unanilipa dola elf 45 kwa mwezi. Hii ilikua komesha. [emoji23][emoji23][emoji119][emoji119] baada ya mama kufariki mengi akajua ameutua mzigo kumbe na yeye safari ikafika. Muda utafichua kila kitu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuhusu Mengi kuachana na mke wake hiyo inajulikana sana lbd kama hizo talaka/nyaraka hazipo.Na wala sio madam au huyo Jacky tu kaspend nao wapo wengi ila aliamua kutulia na JackJack. Pesa atapata maana kashazaa tayari na watoto ni wadogo na haitakwepeka kuwa ile ni damu ya Mengi. Sijaona kosa lake lbd hapo kwenye huo wosia ndipo alipoharibu. I hope mahakama /ukoo utafanya maamuzi sahihi juu ya hizo mali
U are right. Very. Ile kuzaa ndo itambeba. Kuhusu divorce hapo kidogo niko gizani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuhusu Mengi kuachana na mke wake hiyo inajulikana sana lbd kama hizo talaka/nyaraka hazipo.Na wala sio madam au huyo Jacky tu kaspend nao wapo wengi ila aliamua kutulia na JackJack. Pesa atapata maana kashazaa tayari na watoto ni wadogo na haitakwepeka kuwa ile ni damu ya Mengi. Sijaona kosa lake lbd hapo kwenye huo wosia ndipo alipoharibu. I hope mahakama /ukoo utafanya maamuzi sahihi juu ya hizo mali

Ukienda mahakamani huendi kuongea mambo yanayojulikana, bali unaenda kutoa vielelezo/ushahidi kisha sheria inaangaliwa. Unajua kinachofanya ndoa ionekane imevunjwa ukiwa mahakamani? Au unadhani ukiachana na mtu kila mtu kivyake ndio mtakuwa mmeachana? Unajua kuna tofauti baina ya kuachana na kutengana?

Nani alikuambia kuzaa ni sababu pekee ya kupata pesa mahakamni?
Huyo Jack anahofia jambo gani kuhusu malezi ya watoto wake aliozaa na Marehemu Mengi, nani alimuambia hawatalelewa?
Unajua nini kinafanya kesi iwe mahakamani?

Kwenye Wosia hajaharibu maana ndicho kitu/ ushahidi pekee alionao. Unafikiri kama anatamaa ya kupata zaidi angefanya nini?

Jack sio kwamba asingepewa urithi na wale ndugu na watoto wa Mengi sema yeye anachotafuta ni kupata zaidi.
 
Tatizo mkuu hujaelewa unayemtetea unamtetea kwa kipi. Jack anataka mali zote za Mengi ziwe zake yaani ITV na kila kitu(hata nyumba wanazoishi watoto wakubwa wa Mengi kama ni za Mengi watolewe ziwe za jack na sio wanawe wadogo). Ndugu hawajawahi kumnyima urithi ila yeye ndie anayetaka awadhulumu.

Yeye jack anaona wale watoto wakubwa hawana haki yoyote kwa Mengi
Kuhusu Mengi kuachana na mke wake hiyo inajulikana sana lbd kama hizo talaka/nyaraka hazipo.Na wala sio madam au huyo Jacky tu kaspend nao wapo wengi ila aliamua kutulia na JackJack. Pesa atapata maana kashazaa tayari na watoto ni wadogo na haitakwepeka kuwa ile ni damu ya Mengi. Sijaona kosa lake lbd hapo kwenye huo wosia ndipo alipoharibu. I hope mahakama /ukoo utafanya maamuzi sahihi juu ya hizo mali
 
Ukienda mahakamani huendi kuongea mambo yanayojulikana, bali unaenda kutoa vielelezo/ushahidi kisha sheria inaangaliwa. Unajua kinachofanya ndoa ionekane imevunjwa ukiwa mahakamani? Au unadhani ukiachana na mtu kila mtu kivyake ndio mtakuwa mmeachana? Unajua kuna tofauti baina ya kuachana na kutengana?

Nani alikuambia kuzaa ni sababu pekee ya kupata pesa mahakamni?
Huyo Jack anahofia jambo gani kuhusu malezi ya watoto wake aliozaa na Marehemu Mengi, nani alimuambia hawatalelewa?
Unajua nini kinafanya kesi iwe mahakamani?

Kwenye Wosia hajaharibu maana ndicho kitu/ ushahidi pekee alionao. Unafikiri kama anatamaa ya kupata zaidi angefanya nini?

Jack sio kwamba asingepewa urithi na wale ndugu na watoto wa Mengi sema yeye anachotafuta ni kupata zaidi.
U finished it all

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo mkuu hujaelwa unayemtetea unamtetea kwa kipi. Jack anataka mali zote za Mengi ziwe zake yaani ITV na kila kitu(hata nyumba wanazoishi watoto wakubwa wa Mengi kama ni za Mengi watolewe ziwe za jack na sio wanawe wadogo). Ndugu hawajawahi kumnyima urithi ila yeye ndie anayetaka awadhulumu.

Yeye jack anaona wale watoto wakubwa hawana haki yoyote kwa Mengi
Ila kama wale housegirls wa mengi walisema jacky huwa ana ukichaa basi inawezekana kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Angempenda Mengi angependa na ndugu zake, yeye alikua na maslahi yake, ndugu za Mengi wamemu expose hivyo anachukia...

asanteeee bonge la mama ndo maana nadeclare upendo wangu juu yako forever and ever amen
 
Kuhusu Mengi kuachana na mke wake hiyo inajulikana sana lbd kama hizo talaka/nyaraka hazipo.Na wala sio madam au huyo Jacky tu kaspend nao wapo wengi ila aliamua kutulia na JackJack. Pesa atapata maana kashazaa tayari na watoto ni wadogo na haitakwepeka kuwa ile ni damu ya Mengi. Sijaona kosa lake lbd hapo kwenye huo wosia ndipo alipoharibu. I hope mahakama /ukoo utafanya maamuzi sahihi juu ya hizo mali
Umewashitaki wamachame sita, wameweka mawakili na wamechafuliwa mitandaoni kwamba wanataka kumpora mali aliyekuwa mke wa marehemu alafu WAAMUE KWA BUSARA? WAPALESTINA WA MACHAME MKUU?

JAQ ana mali na kampuni yake ya fanicha, watoto wanasomeshwa na fedha za marehemu, yye akitombeshe tu huko na aolewe maana bado ni mtoto mdogo na hamu ya kufanywa mapenzi anayao sana tu
 
Back
Top Bottom