Aliyewahi kuwa Mwanamuziki Nchini na ambaye ni mke wa Marehemu Regnald Mengi, Jacqueline Mengi maarufu kama K-Lyinn amedai kuzuiwa kuingia kwenye kaburi la mumewe, Reginald Mengi
Bila kusema ni nani anaowazungumzia, kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter ameandika “Nimenyamaza kwa mengi sana tu. Mmefikia hatua ya kunizuia mimi na wanangu kuingia kwenye kaburi la mume wangu.”
Ameendela na kuandika “Tunafukuzwa eti mpaka tuombe ruhusa ya kuingia kwenye kaburi la mume na Baba wa watoto wangu. Nimechoka, sitakubali kuendelea kuona wanangu wakisononeka na sitakaa kimya.”
Reginald Mengi ambaye alikuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP alifariki dunia Mei 2, 2019 na kuacha mke (Jacqueline Mengi) na watoto wanne ambao ni Regina, Abdiel, Jayde na Ryan. Watoto hao amezaa na Mercy Mengi pamoja Jackline Mengi
View attachment 1365926
BAADHI YA MAONI YA WADAU:
View attachment 1365927
View attachment 1365928
View attachment 1365929
View attachment 1365930
View attachment 1365931
View attachment 1365932